mkuu kumbe upinzani ulikuwepo from those days!! leo ndani ya bunge la ccm ukifanya upinzani kidogo waitwa msaliti -- wakowapi waliohoji na kuikaba serikali koo? nakumbuka nikiwa mdogo mbunge machachari tuntemeke aliweka shilling kwenye bajeti moja na kuikwamisha kwa siku 3 mfululizo -- ikabidi mwalimu ampigie simu wayamalize!!Tumtemeke Sanga na Abel Mwanga pia walikuwepo. Nyakati hizo ilikuwa raha. Walimnyima mzee wa Msasani usingizi kipindi hicho.
leo hii kina lissu wakimbana spika kidogo tu, serikali inalialia eti wakorofi/ watukutu- yaani spika na naibu wake wanatuondolea radha ya bunge wananchi tunataka bunge li-flow...nguvu ya hoja itawale yaani ni sawa na refa kupiga piga filimbi bila sababu za msingi.
nakumbuka nikiwa mdogo nilisimuliwa eti Tumtemeke Sanga (RIP), alipopata degree yake ya 7, mwalimu akamuulza "Temeke wataka kazi ipi? Tumtemeke akamjibu "kama hiyo ya kwako" ( sina uhakika ila wengi mnajua hii story)