Tujikumbushe vya zamani kidogo, vimepotelea wapi hivi?

Tujikumbushe vya zamani kidogo, vimepotelea wapi hivi?

Mkuu ongeza na "makida makida" sana mabinti walipenda sn huu mchezo na ulivuma sn kitambo iko...walikuwa wakiruka kwa kutumia mpira mwembamba wa manati km sikoseiBila kusahau 'bilingeba yoyo bilingeba yo..tunamuomba talentboy atuoneshe maringo yke bingilibingili mpaka chini"...,...aisee!Ila mkuu hii si ilibidi uipelleke kule 'chit chat' hii.

Hahahahahaha mkuu ni kitambo kinyama
 
kuna ule wimbo wa mama kapika ugali na mfinyango wa nyama ya dede ya dede yaaaa! na ule katoka shamban na mkungu wa ndizi, kipindi hicho shule mnasoma kitabu cha hawafu mwenye nguvu, mkicheza football unavaa kiatu mguu m1 kingine unampa mwingine.

Mkuu kwa kweli tumetoka mbali sana mnacheza mpira wengne wanavua shati wanacheza vifua wazi hadi raha
 
Bu bubu hasemi mi mimi mdogoo go gogo la mti ti tina na mjuba baba mkali lindi ina vita ta ta hahahaha long time

Mganga wa mchezo wa tausi aliitwa nani Kalumanzila lala salama mama wa kambo mbona wanitesa sasa naondoka ka kaa peke yako koma kunipiga gari la baba ba baba mzazi zi zizi la ng'ombe mbe mbele ya nyumba mba mbali na mungu Mungu mkubwa bwawa la samaki ki king majuto to tone la maji jitu la kale le lenye midevu vu vumbua dhahabu bu bubu hasemi mi mi mdogo gogo la mti ti tina mjuba ba bahari ya hindi ndi hindi la kuchoma ma macho yanaona mbali li mbali na upeoo o ondoka upesi........utaendelea

Nakumbuka nilipokua naimba huu wimbo leo palivyo noma

Hahaha mama wa kambo, mbo mbona wanitesa, sa sasa naondoka, ka kaa peke yako, ko koma kunipiga, ga gari la jeshi, shi shingo ya mtu, tu tundu la nyoka, ka karibu na wewe, we wembe wa kucha, cha chakula kitamu, mu Mungu mkubwa.....

inaanza iv"ko koma kunipiga,ga gari la baba,ba baba mzazi,zi zizi la ng'ombe,mbe mbele ya nyumba,mba mbali na wewe,we wembe wa kucha,cha chakula kichafu,fu fuvu ka kale..umenikumbusha mbali sana kaboom

Hili songi naona lina version nyingi..Kuna watu walikuwa wakiimba hawamalizi
 
Dah nakmbk mnaanza gemu saa mbili asubuhi mnatoks saa saba kwa ajili ya msosi then mnalianzisha mpaka kumi na mbili.....mtu unatoka umechoka chepechepe afu ukilala usiku ukiamka asubuhi kitanda kama bwawa vile....

Wengine ilikuwa ukienda kula wanaliendeleza kila mtu anaenda kwa mda wake
 
[emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji86] [emoji86] [emoji86] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Najua na we uliwahi..Kama ulinusurika kwenye kibaba baba ,basi kwenye kombolela..tena huko ndo mlikuwa mnabadilisha hadi nguo
 
Najua na we uliwahi..Kama ulinusurika kwenye kibaba baba ,basi kwenye kombolela..tena huko ndo mlikuwa mnabadilisha hadi nguo
Haha Hahaaaaaaaa nikithema utanichapa. Nope kombolela tulikuwa tunabadilishana nguo watu wa jinsia moja
 
kuna hili songi nimekumbuka

Mungu mkubwa, bwa bwabwa na samaki, ki king majuto, to tone la maji, ji jitu la kale, le lenye midevu, vu vumbua dhahabu........Nimesahau linaendeleaje

Vumbua dhahabu bu, bubu hasemi MI, mimi mdogo go, gogo la mti ti, Tina na mjuba ba, baba wa kambo mbo, mbona wanitesa sa, sasa naondoka ka, kaa peke yako ko, koma kunitesa! Sa sanguloooo ooooh 🎶 sangulo ooooh 🎶😂
 
Kitu cha tobo dunda hahaha na mchezo mwingne ni bong'oa daa mchezo ilitupa akili sana zaman
 
Back
Top Bottom