Tujikumbushe vya zamani kidogo, vimepotelea wapi hivi?

Tujikumbushe vya zamani kidogo, vimepotelea wapi hivi?

kuna hili songi nimekumbuka

Mungu mkubwa, bwa bwabwa na samaki, ki king majuto, to tone la maji, ji jitu la kale, le lenye midevu, vu vumbua dhahabu........Nimesahau linaendeleaje

Bu bubu hasemi ?mi mimi mdogo go gogo la mti..ti tina na mjuba..ba baba mkali..li lindi wa tausi......tausi ndege wangu ndege wa fahari...... hhhaaaaaaa
 
Hahaha mama wa kambo, mbo mbona wanitesa, sa sasa naondoka, ka kaa peke yako, ko koma kunipiga, ga gari la jeshi, shi shingo ya mtu, tu tundu la nyoka, ka karibu na wewe, we wembe wa kucha, cha chakula kitamu, mu Mungu mkubwa.....

Mungu mkubwa bwa, bwawa la samaki ki, king majuto to , tone la maji ji, jitu la kale le, lenye madevu vu, vumbua dhahabu bu, bubu hasemi MI, mimi mdogo go, gogo la mti ti, Tina na mjuba ba, baba wa kambo mbo, mbona wanitesa sa, sasa naondoka ka, kaa peke yako ko, koma kunitesa,
 
Enzi zetu kulikuwa na:

Nago
Mdako
Kipande
Ndiki (mpira wa miguu au netiboli)
Ukuti
Kidali
Gololi
Pia

Na mingineyo, kuikumbuka yote yataka wasaa.
 
Mungu mkubwa bwa, bwawa la samaki ki, king majuto to , tone la maji ji, jitu la kale le, lenye madevu vu, vumbua dhahabu bu, bubu hasemi MI, mimi mdogo go, gogo la mti ti, Tina na mjuba ba, baba wa kambo mbo, mbona wanitesa sa, sasa naondoka ka, kaa peke yako ko, koma kunitesa,
Teh enzi zetu mwee
 
Kipindi hicho utoto ilikuwa raha sana aisee..Nakumbuka kitaa tulikuwa na lugha zetu ambazo tulikuwa tunaelewana wenyewe tu..Mtu wa kuja unaweza kutetwa na usielewe

Hii ya lugha umenikumbusha mbali ,tulikua tunaweka herufi "chi"kutenganisha herufi mfano neno wewe lilitamkwa "wechiwechi"

",kachimachi wechiwechi nichi mchijachinjachi uchimechinichiechilechiwachi
 
Bu bubu hasemi ?mi mimi mdogo go gogo la mti..ti tina na mjuba..ba baba mkali..li lindi wa tausi......tausi ndege wangu ndege wa fahari...... hhhaaaaaaa
Ndege umekwima mali,sasa wataka vumbi...
Wapita watu wawili,wameleta uramani sasa tuko mbali mbali
 
Hii ya lugha umenikumbusha mbali ,tulikua tunaweka herufi "chi"kutenganisha herufi mfano neno wewe lilitamkwa "wechiwechi"

",kachimachi wechiwechi nichi mchijachinjachi uchimechinichiechilechiwachi
Umeona ehhee..Hapo unaweza kuniteta wala nisishike hata moja..Sisi tulikuwa na ya kuongea Kinyume, pamoja na ya kuondoa herufi za mwisho na kuweka "psi"....Mapsi vipsi kapsi(mambo vipi kaka)
 
Teh teh. kat.ph Mkuu naona umepiga remix kabisa...Hadi Sangulooooo
 
Last edited by a moderator:
kuna hili songi nimekumbuka

Mungu mkubwa, bwa bwabwa na samaki, ki king majuto, to tone la maji, ji jitu la kale, le lenye midevu, vu vumbua dhahabu........Nimesahau linaendeleaje

Bu bubu hasemi, mi mimi mdogo, go gogo la mti, ti tina na mjuba...
Lol Sisi tuliendelezeaga hvyo na ilikuaga raha kwakwel
 
Back
Top Bottom