Tujikumbushe Walimu wa sekondari waliokuwa wakali sana kiasi cha kuwa maarufu hadi shule zingine

Tujikumbushe Walimu wa sekondari waliokuwa wakali sana kiasi cha kuwa maarufu hadi shule zingine

Mi shule yetu mwl ukishika fimbo unafukuzwa kazi
Ilikiwa haruhusiwi katu kupiga mwanafunzi

Forest hill moro
Ila alikuwepo mwl mmoja hivi kiswahili anamikwara sana

Jina limenitoka
 
Kwa shule ya msingi kuna mpuuzi anaitwa lwebangila alikuwa mlimwa sm dodoma alikuwa nyoko sana
Mungu mwema alitumbuliwa baadaye watoto wakapona

Mwl tambala huyu mzee cristapen sita sita

Kuna mwingine mikocheni anaitwa
Mwl kondo

Mweeeee kabla hujachapwa fimbo ushakula mabanzi ya shingo mgongo shavuni kama 50 ndo ije fimbo katikati ya kiuno na tako
 
Kuna siku nilitoroka airport Dogo alinitafuta siku nzima shenzi type. Umemsahau mtu m-bad makusi hakuna kucheka.
Hahahahaa airport unapiga magot
Dakika 5 go back to your class

Raha sana
Wa mwaka gani wewe pale
 
Nimeandika huu uzi baada ya kuwakumbuka waalimu wangu hasa wale wakuu wa miaka ya 90 mwishoni na 2000 mwanzoni waliokuwa wakali sana wasiotaka masikhara kiasi cha kuweza kujulikana hadi mkoa mzima na kanda. Wafuatao walivuma sana kanda ya kaskazini;

1. Mwalimu Kibatala - Shule ya sekondari Karatu, Arusha.
2. Mwalimu Shayo - Shule ya Sekondari Arusha.
3. Mwalimu wa malezi Ilboru sec, jina limenitoka ila ana jina la kimasai. Waliosoma 1998 - 2001 wanaweza kumkumbuka.
4. Mwalimu Teti - Tanga technical Secondary school. Huyu mkuu wa shule ilikuwa sio poa...
5. Mwalimu Mpande - Moshi Technical Secondary School. Huyu mwalimu kwenye umisetta alikuwa tishio. Ukileta zako ni kibano unakula.
6. Munga - Kaloleni sec, Arusha.
7. Kipingu -
8. Mwalimu Masatu na Mgimwa - Mkwawa High School (complex)
Ongezeeni majina mengine tujikumbushe enzi za u-teenage.
Mr. Mshana Academic Master waliosoma Mbezi wanamjua huyu Mzee alikua mkali km pilipili na Mara ya mwisho naenda nilisikia alifariki kwa Kisukari, R.I.P ulale unapostahiri mwalimu
 
Du Kumbe Yule mama alishafariki!
Mkiramweli baba sijui alikuwaga na shida gani, siku moja alitaka kunichapa kiduanzi duanzi nikakataa. Akanipeleka kwa head master Mr. Isack Malisa, mkuu aliposikia kisa chenyewe akambia nirudi zangu class! Kuanzia hapo jamaa akawa kaninunia, sijui ndo kazira………wala sikujishughulisha naye!
Mkuu Isack Malisa alikuwa mkuu shule gani? Mi nilimkuta Moshi tech. 1981 - 1984. The man was very smart. Nasikia alikuja kumuoa madam Oberlin wa biology. Waalimu wetu Hawa walitu-shape vizuri, Mungu awabariki, awarehemu waliotangulia. Kina Mpande, Nzohi, Kasenge, headmaster Malale etc.
 
Duh, was looking very young.. alituchangamsha sana hasa kutuamsha asubuhi kukimbia mchakamchaka. Kupitia Dom 1 hadi Dom 40 sio mchezo. we umemaliza pale mwaka gani
Mkuu mi ilikuwa Dom X pale Karume. Vipi we ulienda kukaanga bisi kule orchard? Misele ya dom 0 vp?
 
Ningeshangaa sana kama usingemtaja Mwalimu Mpande wa Moshi Technical, daah umenikumbusha mbali sana japokuwa umri umeenda sasa ila sitakaa nimsahau huyu mtu. Alikuwa noma sana na usemi wake eenhe bwaana..😄😄, mara ya mwisho nilikutana naye pale Moshi mjini Fresh coach 2018 nikamtupia wekundu kadhaa, alinishape sana kitabia namshukuru kwa kweli may be leo nisingekuwa hivi nilivyo. Live longer Mr. Mpande
Ukipigwa biti na Mpande unajua kabisa leo nafukuzwa shule, kumbe biti tu.
 
Mkuu Isack Malisa alikuwa mkuu shule gani? Mi nilimkuta Moshi tech. 1981 - 1984. The man was very smart. Nasikia alikuja kumuoa madam Oberlin wa biology. Waalimu wetu Hawa walitu-shape vizuri, Mungu awabariki, awarehemu waliotangulia. Kina Mpande, Nzohi, Kasenge, headmaster Malale etc.
Moshi Technical miaka kuanzia 2000
 
Back
Top Bottom