Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

KUNA MZEE HAPO KATUTUSI WA DOT COM, Mzee Mzima Busara Hakuna. Mimi Wa 94, Lakini Naweza Kuielezea RTD Nilo Ipenda Na Si TBS Ya Sasa, Namkubali Mze Masood Masood Na Zilipendwa, Napenda Zaidi Hata Sasa Kipindi Cha Kutoka Maktaba Ambacho Waga Kina Rudia Vipindi Vya Zamani. Siku Moja Walirudia Cha CLUB LAHA LEO Cha Mwaka 91, Nikasema Zamani Ilikuwa Raha. Zamani Nilimsikiaga Beni Kiko, Sijui Yu Wapi? Tumboi Lisasi, Halima Mchuka Kifo Chako Kilinipa Shida Saana! Nakumbuka Twende Na Wakati, Namkumbuka Kibuyu. Namkumbuka Bakari Msulwa Nilimfuatilia Mpaka Katika Redio Japan NHK, Anisamehe Maana Niliwaacha Ghafla Kutokana Na Majukumu Ya Hapa Na Pale. Ashedi Chelewa Na Ndelema Bado Wana Tangaza Kipindi Cha Ngoma. Masoooood Mungu Akupe Maisha Marefu, Hazina Yetu Wewe! Nina Mengi Ya Kusema Lakini RIH, RIH,RIH RTD
 
...ewaaa.....right on!!...Ms Eda Sanga...hivi huyu yuko wapi hivi sasa?.......

Kuna wakati alikuwa Tume ya Uchaguzi ya Kiravu, sasa hasikiki tena , labda amekua freelance ? Pengine Pasco aje kutusaidia
 
Kuna wakati alikuwa Tume ya Uchaguzi wakati wa Kuravu, baadaye akawa hasikiki, labda ni freelance sasa, labda Pasco aje kusaidia

Mwaka Jana Nakumbuka Alikuwa Pale Mlimani Akiwa Msimamizi Wa Mlimani Tv Na Redio. Na Mlimani Radio....... Hafikiri Atakuwa Pale
 

Shangazi Debora Mwenda.
 
Mkuu TBC haikuwepo kipindi hicho.
Acha kupotosha...

Mkuu Bramo hajapotosha.
Marehemu Ally Saleh ni cousin wangu.
Alifariki wakitoka kazini na gari ya TBC kwa kugongwa na treni kwenye crossing ya Ilala Shaurimoyo.
Walikuwa watatu:-
Ally Saleh, Kwege Munthali na mwingine jina limenitoka.
 
KBC unanikumbusha kipindi cha Je huu ni uungwana? na Leonard Mambo Mbotela

Kuna mtangazaji mmoja wa KBC Bi Hadijah Ally, nadhani ni kutoka mkoa wa Mombasa. Huyu mama atakuwa mzee kwa sasa, ila ana kiswahili fasaha sana zaidi ya hata ya Watanzania.
 
pascal, hawa nao huwakumbuki? Dastan Tido Mhando, Chama omari Matata, Godfrey Mngodo, Teckla Gumbo, (Salim?- Mume wa Zamzam Maalim),Ahmed Kipozi, Julius Nyaisanga, Sango Kipozi, Abdul Omar Masudi, Mshindo Mkeyenge etc
Nawakumbuka, asante kunikumbusha Mshindo Mkenyenge ndie nilimshau, Masoud na Juliasi niliisha waweka, not sure status ya Thecla maana aliishakuwa mtu mzima sana. Tido, Chama, Mngodo, Kipozi na Sango wapo!.
Pascal
 
...ewaaa.....right on!!...Ms Eda Sanga...hivi huyu yuko wapi hivi sasa?.......
Aliajiriwa mwaka 1968 with the maiden name ya Edda Williams Ngulukulu, alikuja kuolewa na Sanga na kugeuka Edda Sanga, enzi hizi watangazaji wa habari walikuwa ni wanaume tuu, yeye ndio alikuwa mwanamke wa kwanza kutangaza habari RTD miaka ya 80's.

Alistaafu RTD na sasa ni mkurugenzi wa Mlimani Media.
Pasco.
 
Nawakumbuka, asante kunikumbusha Mshindo Mkenyenge ndie nilimshau, Masoud na Juliasi niliisha waweka, not sure status ya Thecla maana aliishakuwa mtu mzima sana. Tido, Chama, Mngodo, Kipozi na Sango wapo!.
Pascal

List imemsahau Radio DJ wa kwanza wa enzi hizo:-
Said Omar Kassongo.

Nakumbuka mitumbuizo yake na story nyiiiingi. Ama kweli wametangulia watu wa ukweli!
 

Ya, mama huyu(kwa sasa ni mama) ni mtangazaji mahiri sauti imetulia, akisoma habari anatulia vituo kwa vituo. Jambo ambalo silipendi ni huu mfumo wa usomaji wa TBC ambapo wameondoa ule wa mwanzo wa kutaja eneo halafu habari yake inafuata na kuadapt ile ya habari kusomwa tu ndani yake ndo unajua tukio hili lilitokea Shinyanga. Zamani ilikuwa hivi
 

Vipi na BALANDINA HIZZA??
Mara ya mwisho nilisikia yuko Tanga, mtu mzima sana.... bado yupo?
 

Zamani ilikuwa hivi: Shinyanga, Watu wanne wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kuchovhea ugomvi.....na maelezo mengine mengi ndani yake yakifafanua habari hiyo. Siku hizi: Watu wanne wanashiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kuchochea ugomvi.........na mengine baadae utaambiwa, tukio hilo limetokea jana Shinyanga..... Sasa hii format siyo nzuri. Lakini jambo ambalo.pia siyo zuri ni kuondoa ngoma zile za mzee Morris wakati wa Taarifa ya habari TBC Taifa, badala yake wameweka Tone ambayo hata siipendi
 

Binafsi nilitambulishwa kwako na Anko wangu (John Kayuza) ambaye alikuwa Mwalimu wako pale TSJ, Ilala Shariff Shamba. Kipindi hicho nakumbuka hata Nadhir Mayoka naye alikuwa hapo Chuo. Pasco, maandiko yako "nayakubali"na mchango wako ndani ya JF, ni mkubwa sana na bado unahitajika......

 
....................Asheri Stanley Chilewa.................
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…