Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Swedi mwinyi aisee...jamaa ana kipaji cha ajabu cha utangazaji hasa anapotangaza mipira utapenda hawa wa sasa wanajitahidi kwa mbali ingawa maadili yao yako chini mnoo
Mzee wa Karate, nakumbuka miaka ya mwanzoni mwa 2000 aliwahi kupanga nyumba maeneo ya Ubungo Maziwa karibu kabisa na Matank ya Tanesco.

Alihama bila kuaga majirani mara baada ya tank moja kulipuka mwaka 2003, moto uliozimwa na kikosi cha kuzima moto cha South Africa...
 

Aboubakar Liongo ...yupo wapi mtu huyu!!!..Nahisi kitenge amekopi na kupesti aina ya utangazaji wake..!
 
Hannah Maige, Halima Mchuka (al marhum), Malima Ndelema, Henrik Libuda.....................
 
Aboubakar Liongo ...yupo wapi mtu huyu!!!..Nahisi kitenge amekopi na kupesti aina ya utangazaji wake..!
Jamaa alikua BBC London...Kitenge kipindi yuko TSJ alikua anafanya Training Radio one chini ya Abubakar Liongo. Alianza kumuiga toka kipindi hicho....Dah, jamaa alikua anajua sana
 

Umemsahau Ben Kiko.

Dandi Wakati huyu mnzanzibar alikuwa mkurugenzi wa RTD
 
Swedi mwinyi aisee...jamaa ana kipaji cha ajabu cha utangazaji hasa anapotangaza mipira utapenda hawa wa sasa wanajitahidi kwa mbali ingawa maadili yao yako chini mnoo

Ni kweli Mkuu, umenikumbusha alivyokuwa anasema, namna gani pale, anaruka maigeli.
 
Hapo kwa Juma Nkamia toa na weka Nswima Ereeenest au Tutajie Sekioni Kitojo. Tafadhali mkuu.
 

Yaani umerudia baadhi ya majina ila umemwacha Malima Ndelema.???nakata rufaa
 
Nkamia is a misfit in this list. mtafutieni wenzake kiukweli sio hawa waungwana.
 
Kama hutamtoa Juma Nkamia kwenye hiyo list, nashika shilingi.
Nkamia si mchumia tumbo wa juzi juzi tu na akaajiriwa bbc kama msoma habari tu na si kundika chochote, kurekebisha chochote au kuongeza neno lolote.
Hata Tido alisema haya ninayosema.
 

Ben Kiko amefariki usiku wa kuamkia leo 31-10-2014 huko Tabora. RIP Ben Kiko!
 
Kumbe Khaled Ponera hatupo naye tena,namkumbuka sana siku ya jumamosi na jumapili saa 3 na nusu usiku kwenye vipindi vya maigizo cha waakina marehemu mzee Janja,mzee Jongo na jumapili kipindi cha waakina Mzee Jangala na mzee Mundu.Yeye ndio alikuwa anafungua hivyo vipindi vya maigizo na kuvifunga na vipindi hivyo huwaga baada ya majira usiku.
Nitakukumbuka daima Khaled Ponera.
 

Kile kipindi cha salamu kwa wagonjwa ndio kile cha ugua pole ambacho kilikuwa jumapili kati ya mida ya saa 3 na saa 4 asubuhi.
 
Kharid Ponela nae ametutoka lini jamani, RIP watangazaji wote wa RTD, sitokuja kumsahau Siwatu Luanda, yule dada alivyokufaga nilitoaga machozi

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…