Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Swedi mwinyi aisee...jamaa ana kipaji cha ajabu cha utangazaji hasa anapotangaza mipira utapenda hawa wa sasa wanajitahidi kwa mbali ingawa maadili yao yako chini mnoo
Mzee wa Karate, nakumbuka miaka ya mwanzoni mwa 2000 aliwahi kupanga nyumba maeneo ya Ubungo Maziwa karibu kabisa na Matank ya Tanesco.

Alihama bila kuaga majirani mara baada ya tank moja kulipuka mwaka 2003, moto uliozimwa na kikosi cha kuzima moto cha South Africa...
 
Gooooooo...anakosa, Zamoyoni Mogela anapiga mpira ule unapita sentimita chache ya mwamba wa goli yapata urefu wa unyayo wa binti yangu mariam.......kionjo murua toka kwa sweeed bin mwinyi. Dah jamaa nlikua namkubali sana pamoja na jamaa mmoja alikua anatangazia Radio One, Aboubakar Liongo..

Aboubakar Liongo ...yupo wapi mtu huyu!!!..Nahisi kitenge amekopi na kupesti aina ya utangazaji wake..!
 
Hannah Maige, Halima Mchuka (al marhum), Malima Ndelema, Henrik Libuda.....................
 
Aboubakar Liongo ...yupo wapi mtu huyu!!!..Nahisi kitenge amekopi na kupesti aina ya utangazaji wake..!
Jamaa alikua BBC London...Kitenge kipindi yuko TSJ alikua anafanya Training Radio one chini ya Abubakar Liongo. Alianza kumuiga toka kipindi hicho....Dah, jamaa alikua anajua sana
 
Sara Dumba, Jacob Tesha, Seleman Hega, Danstan Tido Mhando, Seleman Kumchaya, Peter Makorongo, Charles Hillary,

Omary Jongo, Ahmed Jongo, Sango Kipozi, Masoud Masoud, Aloisia Isabula,Aloisia Maneno, Debora Mwenda, Mikidadi Mahamoud, Juma Nkamia, Swedi Mwinyi, Ahmed Kipozi, Dominic Chilambo, Bati Kombwa, Nadhir Mayoka, Abdallah Majura,

Michael Katembo,Abisae Steven, Abdallah Mlawa,Nassoro Nsekeli,Bujaga Izengo Kadago,David Wakati,Khalid Ponera,Christina Chokunogela,Ahmed Kipozi,Siwatu Luwanda,Salim Seif Nkamba,Salama Mfamao,Bartholomew `Bati' Kombwa

Ahmed Jongo,Dominic Chilambo,ngalieni Mpendu,Sekioni Kitojo,Chisunga Steven, Tumbo Risasi,
Edda Sanga,Mikidadi Mahmoud,Mshindo Mkeyenge.

Hii ilikuwa Lineup ya kutisha sio ujinga wa kipindi hiki hakuna ethics wala nini...................Wengine ongezeni.

Nawasilisha.

Umemsahau Ben Kiko.

Dandi Wakati huyu mnzanzibar alikuwa mkurugenzi wa RTD
 
Swedi mwinyi aisee...jamaa ana kipaji cha ajabu cha utangazaji hasa anapotangaza mipira utapenda hawa wa sasa wanajitahidi kwa mbali ingawa maadili yao yako chini mnoo

Ni kweli Mkuu, umenikumbusha alivyokuwa anasema, namna gani pale, anaruka maigeli.
 
Hapo kwa Juma Nkamia toa na weka Nswima Ereeenest au Tutajie Sekioni Kitojo. Tafadhali mkuu.
 
Sara Dumba, Jacob Tesha, Seleman Hega, Danstan Tido Mhando, Seleman Kumchaya, Peter Makorongo, Charles Hillary,

Omary Jongo, Ahmed Jongo, Sango Kipozi, Masoud Masoud, Aloisia Isabula,Aloisia Maneno, Debora Mwenda, Mikidadi Mahamoud, Juma Nkamia, Swedi Mwinyi, Ahmed Kipozi, Dominic Chilambo, Bati Kombwa, Nadhir Mayoka, Abdallah Majura,

Michael Katembo,Abisae Steven, Abdallah Mlawa,Nassoro Nsekeli,Bujaga Izengo Kadago,David Wakati,Khalid Ponera,Christina Chokunogela,Ahmed Kipozi,Siwatu Luwanda,Salim Seif Nkamba,Salama Mfamao,Bartholomew `Bati’ Kombwa

Ahmed Jongo,Dominic Chilambo,ngalieni Mpendu,Sekioni Kitojo,Chisunga Steven, Tumbo Risasi,
Edda Sanga,Mikidadi Mahmoud,Mshindo Mkeyenge.

Hii ilikuwa Lineup ya kutisha sio ujinga wa kipindi hiki hakuna ethics wala nini...................Wengine ongezeni.

Nawasilisha.

Yaani umerudia baadhi ya majina ila umemwacha Malima Ndelema.???nakata rufaa
 
Nkamia is a misfit in this list. mtafutieni wenzake kiukweli sio hawa waungwana.
 
Kama hutamtoa Juma Nkamia kwenye hiyo list, nashika shilingi.
Nkamia si mchumia tumbo wa juzi juzi tu na akaajiriwa bbc kama msoma habari tu na si kundika chochote, kurekebisha chochote au kuongeza neno lolote.
Hata Tido alisema haya ninayosema.
 
Ben Kiko, sijui yuko wapi huyu jamani
Alesia maneno na Alesia Isabula nadhani bado wapo TBC taifa
Watangazaji wa zamani walikuwa watangazaji kweli
Chezea Michael Katembo na Kipindi cha mkoa kwa mkoa
Nilikuwa nampenda Siwatu Luanda(RIP)nakumbuka alifariki nikiwa drs la tano miaka hiyo

Ben Kiko amefariki usiku wa kuamkia leo 31-10-2014 huko Tabora. RIP Ben Kiko!
 
Kumbe Khaled Ponera hatupo naye tena,namkumbuka sana siku ya jumamosi na jumapili saa 3 na nusu usiku kwenye vipindi vya maigizo cha waakina marehemu mzee Janja,mzee Jongo na jumapili kipindi cha waakina Mzee Jangala na mzee Mundu.Yeye ndio alikuwa anafungua hivyo vipindi vya maigizo na kuvifunga na vipindi hivyo huwaga baada ya majira usiku.
Nitakukumbuka daima Khaled Ponera.
 
Kipindi hiko kulikuwa na vipindi vinavyogusa jamii jamani,watoto walivutwa na mama na mwana,kuna kipindi cha wakati wa kazi,kipindi cha salamu za wagonjwa yaani hadi raha ,mungu awaweke mahali pema watangazaji waliotangulia mbela za haki,wakati nikiwa nafanya kazi Abood media mkoani Morogoro nikiwa na miezi mitatu pale radio na Abood Tv ndipo karim besta akafariki dunia,mungu awaweke mahali pema peponi ,

Kile kipindi cha salamu kwa wagonjwa ndio kile cha ugua pole ambacho kilikuwa jumapili kati ya mida ya saa 3 na saa 4 asubuhi.
 
Kharid Ponela nae ametutoka lini jamani, RIP watangazaji wote wa RTD, sitokuja kumsahau Siwatu Luanda, yule dada alivyokufaga nilitoaga machozi

Back
Top Bottom