Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV



Mkuu hili tangazo nalikumbuka....
CRDB ni benki ya ushirika na maendeleo vijijini,pia hutoa huduma ya mikopo
 
Kulikuwa na kipindi cha Asubuhi sana na kilianza na wimbo wa


"Kumekucha jama kumekucha,

Hata na Jua Mbinguni linatoka,

Hata majogoo vijijini yanawikaaaa,

Wazalendo amkeni tufanye kazi jamaa,


Ee eeh! Tusongembele
Ee eeh! Mama tusonge mbele
Ee eeh! Bava tusonge mbele"
 



Bujaga Izengo Kadago alikuwa anapenda kusema;

"Sherehe,Vigeregere,Nderemo na Vifijo vinatawala hapa"
 
Nimesema maimunaa!!!! Tangazo la kozi ya kiingereza hilo,mm nilikua mpenzi wa kipindi cha mama na mwana jumamos,na alfajiri kombora inafuata muzik na matangazo
 
Duh! Enzi hizo home hakuna tv ni Kaseti na redio ya mkulima.Kaseti una isikiliza weekend tena kama baba kanunua betri. Ila maisha yalikua mazuri kipindi hicho sikosi kipindi cha watoto wetu na kipindi cha mama na mwana. Siwezi kumsahau Debora mwenda (shangazi) alivyo kuwa makini kutu hadithia hizo hadithi episod baada ya episode. Mungu ambariki huko Alipo.
 
Mimi nawakumbuka na mwimbo wa five oc'lock in the morning whach gonna be around the conner.,,na ulikua unapigwa alfajiri iyo kabla ya jogoo kuwika kila siku..
 
Na Tangazo moja la maendeleo 1997.Tunapozungumzia maendeleo Tunazungumzia maendeleo yenu nyinyi wananchi..nilikua silipendi hilo tangazo maana walikua wanatuona malofa kweli yaani wanajua sisi tunajua wanasema maendelo ni ya miti..
 
Yaani unapozungumzia RTD nakaumbuka vitu vingi sana,kama vile vipindi chei chei shangazi,mama na mwana,kombora-saa 11 asubuhi. Nakumbuka vipindi vya maigizo characters wake kama Mzee Mundu,Jangala,Bi nyakomba,Mzee Jongo etc bila kusahau igizo la twende na wakati characters kama Fungafunga,Kidude etc. Reporters kama Dominic Chilambo,Ben Kiko etc . Yote tisa kulikuwa na kitu ambacho kwa sasa ni nadra sana,utasikia mtangazaji anasema "......utakuwa nami mtangazaji wako........nikiwa na fundi mitambo...."
Tumalizie na huu wimbo
"Kuleni chakula bora...chaku-ujenga mwili....."
Kama huo huukumbuki basi kumbuka huu
"Dereva..kagonga mtu....eeh..sawa hiyoooo?.......haaaata. Hiyo si-sawa dereva acha vituko"
 
hapo mimi jamani DEBORA MWENDA na mama na mwana acha kabisa nakumbuka hadithi zake za mfalme kigogwe,unyoya wa kipanga aziz,alfu lela uleka,binti chura,akaja sembamba na safarbza hatar nk jamani enz hizo niko moro ilonga msalabani miaka ya 1984-1989 yani ukiskia mama.na mwana natoka shuleni mazoezi ilonga mbioo kuwahi mama na mwana.
 

Wapi mikidad mahmood?
 


Mkuu sio Dereva kagonga mtu!! Usahihi ni kuwa

"Dereva kalewa gongo eeh sawa hiyoooo?......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…