Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

CRDB ni benki ya wakulima kama..... Vijijini unalikumbuka hili tangazo? Tegemea bp ni nini...trekta meli ndege na vyombo vinginevyo...bp Tanzania limited ni zaidiiii! Je unakumbuka? Vikoromboso vinavyoendelea sasa iv kwenye radio ni aibu tupu. Damn I miss my childhood!!!


Mkuu hili tangazo nalikumbuka....
CRDB ni benki ya ushirika na maendeleo vijijini,pia hutoa huduma ya mikopo
 
Kulikuwa na kipindi cha Asubuhi sana na kilianza na wimbo wa


"Kumekucha jama kumekucha,

Hata na Jua Mbinguni linatoka,

Hata majogoo vijijini yanawikaaaa,

Wazalendo amkeni tufanye kazi jamaa,


Ee eeh! Tusongembele
Ee eeh! Mama tusonge mbele
Ee eeh! Bava tusonge mbele"
 
Du! mkuu, umenikumbusha mbali sana.

Mimi nilipenda sana usomaji wa taarifa za habari za watangazaji wafuatao.

Mzee mwenyewe nguli David Wakati RIP ( ambae hata kanisani Mtakatifu Albano) nasikia alikuwa akipenda kusoma somo la kwanza kwenye biblia)

Charles Hillary

Julius Nyaisanga

Salim Mbonde

Ahmed Jongo

Abisai Stephen

Peter Makorongo

Mikidadi Mahmud

Sekione Kitojo

Suleyman Kumchaya

Florian Kaiza

Jacob Tesha

Bujaga Izengo Kadago

Tumbo Tamim Risasi (alikuwa anapooza kidogo kwenye usomaji wake na ndio maana alikuwa hasomi taarifa kwenye "peek time" kama saa mbili usiku)

Sarah Dumba

Halima Kihemba

Betty Mkwasa

Chini ya marehemu David Wakati, RTD ilikuwa na heshima yake kwa wakati ule na kila msikilizaji aliweza kufahamu ni mtangazaji gani angesoma taarifa ya habari ya saa saba mchana, saa mbili jioni na saa nne ya usiku.Watangazaji walikuwa wakipangwa kusoma taarifa kulingana na uzito wa taarifa hizo na uwezo wao.

Kwa kweli RTD ilikuja kupoteza watangazaji hodari na wenye uwezo mkubwa wa utangazaji katika tasnia hiyo na ni masuala ya malipo ndio yaliyoanza kuwatawanya kwenye kutafuta maslahi sehemu zingine.



Bujaga Izengo Kadago alikuwa anapenda kusema;

"Sherehe,Vigeregere,Nderemo na Vifijo vinatawala hapa"
 
Nimesema maimunaa!!!! Tangazo la kozi ya kiingereza hilo,mm nilikua mpenzi wa kipindi cha mama na mwana jumamos,na alfajiri kombora inafuata muzik na matangazo
 
Duh! Enzi hizo home hakuna tv ni Kaseti na redio ya mkulima.Kaseti una isikiliza weekend tena kama baba kanunua betri. Ila maisha yalikua mazuri kipindi hicho sikosi kipindi cha watoto wetu na kipindi cha mama na mwana. Siwezi kumsahau Debora mwenda (shangazi) alivyo kuwa makini kutu hadithia hizo hadithi episod baada ya episode. Mungu ambariki huko Alipo.
 
Mimi nawakumbuka na mwimbo wa five oc'lock in the morning whach gonna be around the conner.,,na ulikua unapigwa alfajiri iyo kabla ya jogoo kuwika kila siku..
 
Na Tangazo moja la maendeleo 1997.Tunapozungumzia maendeleo Tunazungumzia maendeleo yenu nyinyi wananchi..nilikua silipendi hilo tangazo maana walikua wanatuona malofa kweli yaani wanajua sisi tunajua wanasema maendelo ni ya miti..
 
Yaani unapozungumzia RTD nakaumbuka vitu vingi sana,kama vile vipindi chei chei shangazi,mama na mwana,kombora-saa 11 asubuhi. Nakumbuka vipindi vya maigizo characters wake kama Mzee Mundu,Jangala,Bi nyakomba,Mzee Jongo etc bila kusahau igizo la twende na wakati characters kama Fungafunga,Kidude etc. Reporters kama Dominic Chilambo,Ben Kiko etc . Yote tisa kulikuwa na kitu ambacho kwa sasa ni nadra sana,utasikia mtangazaji anasema "......utakuwa nami mtangazaji wako........nikiwa na fundi mitambo...."
Tumalizie na huu wimbo
"Kuleni chakula bora...chaku-ujenga mwili....."
Kama huo huukumbuki basi kumbuka huu
"Dereva..kagonga mtu....eeh..sawa hiyoooo?.......haaaata. Hiyo si-sawa dereva acha vituko"
 
hapo mimi jamani DEBORA MWENDA na mama na mwana acha kabisa nakumbuka hadithi zake za mfalme kigogwe,unyoya wa kipanga aziz,alfu lela uleka,binti chura,akaja sembamba na safarbza hatar nk jamani enz hizo niko moro ilonga msalabani miaka ya 1984-1989 yani ukiskia mama.na mwana natoka shuleni mazoezi ilonga mbioo kuwahi mama na mwana.
 
Kwa vijana wa zamani. Unakumbuka nini unapopitia majina haya? Je, yuko wapi kwa sasa? Unamkumbuka katika kipindi kipi kilichokufurahisha?

1. Bujaga Izengo Kadago
2. Debora Mwenda
3. Sarah Dumba
4. Julius Nyaisanga
5. Charles Hillary
6. Eshe Mhidini
7. Frolian Kaiza
8. Tumbo Risasi
9. David Wakati
10. Halima Kihemba
11. Betty Mkwasa
12. January Costantine
13. Lando Mabula
14. Ben kiko
15. Abubakary Lyongo
16. Sued Mwinyi
17. Abisai Stevin
18. Nswima Ernest
19. Malima Ndelema
20. Richard Leo
21. Ahmed Jongo
22. Christina Chokunogela
23. Shaban Kissu
24. Jacob Tesha
25. Sallim Mbonde
26. Sekion Kitojo
27. Omary Jongo
28. Abdalla Majura

Wapi mikidad mahmood?
 
Yaani unapozungumzia RTD nakaumbuka vitu vingi sana,kama vile vipindi chei chei shangazi,mama na mwana,kombora-saa 11 asubuhi. Nakumbuka vipindi vya maigizo characters wake kama Mzee Mundu,Jangala,Bi nyakomba,Mzee Jongo etc bila kusahau igizo la twende na wakati characters kama Fungafunga,Kidude etc. Reporters kama Dominic Chilambo,Ben Kiko etc . Yote tisa kulikuwa na kitu ambacho kwa sasa ni nadra sana,utasikia mtangazaji anasema "......utakuwa nami mtangazaji wako........nikiwa na fundi mitambo...."
Tumalizie na huu wimbo
"Kuleni chakula bora...chaku-ujenga mwili....."
Kama huo huukumbuki basi kumbuka huu
"Dereva..kagonga mtu....eeh..sawa hiyoooo?.......haaaata. Hiyo si-sawa dereva acha vituko"


Mkuu sio Dereva kagonga mtu!! Usahihi ni kuwa

"Dereva kalewa gongo eeh sawa hiyoooo?......
 
Back
Top Bottom