Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

1.SIku ya matangazo ya mpira (sauti ya Charles Hillary) , utasikia "...na mafundi mitambo kwenye OB van ;David Namaloye ,Ali Said Tunku, Fundi Ali Kengele.."
2.Mabingwa wa salamu Wajadi Fundi wa Mahuta Shimoni , Dula One wa makorora Tanga
3.Taarifa ya Habari asubuhi na Jacob Tesha
4.Kipindi cha Malenga wetu /mashairi kichizi kila siku saa nane mchana


Dah ilikuwa raha sana
 
Daah Enzi za kununua kadi na kutuma salamu redioni!! Unawapaisha wadau wako wote. Nyakati zimekwenda wapi??
 
Hiyo jingle ninayo mkuu kama unaihitaji nitafute kwenye whatsapp +255 752 22 06 49 nikutumie
 
1. Hisia na muziki: yaani hapo inatengenezwa story nzuri kupitia nyimbo za wakati huo kilikua kinarushwa saa tatu na nusu usiku, siku nimeisahu
2.ATC Hewani: ratiba za usafiri wa anga kupitia shirika letu la ndege la ATC
 

Matuga alikuwa na sauti safi iliyoyulia, walikuwepo kina havijawa, mzee jongo, maua, kuna yule dada alikuwa anacheza nafasi mbili ktk mchezo mmoja, sauti ya kihindi na sauti ya kawaida jina limenitoka, alikuwa mkorofi kwenye mchezo wa mkataa pema pabaya panamwita.

Television zilivyoingia, mnakumbuka tamthilia ya Tausi miaka ya tisini katikatika hapo, unakuta mtaani kuna nyumba moja tu ndio wanativii manajazana kwenye nyumba ya watu kuangalia tamthilia ya Tausi
 
Mpendu na Shaban Kisu

Angalieni Mpendu.....
Shabani Kisu sio wa siku nyingi kivileee, ni D
Nakumbuka kipindi cha cheichei shangazi na uugua pole ule wimbo wakufungulia kipindi nilikuwa na upenda sana ingawa nilikuwa mdogo.

Chei chei shangazi, cheichei shangazi, shangazi chei shangazi, cheichei shangazi
Uje tena shangazi, uje tena shangazi......chei shangazi, uje tena shangazi........
 
salute mkuu [emoji2]
MAMA NA MWANA ..DEBORA MWENDA
 
Nicheki nikutumie hiyo Nidhamu ya kazi ni msingi .......0758 393 393
 
Namkumbuka msomaji wa taarifa ya habari ya R.T.D Barnabas Mluge.Nakumbuka vipindi vya misakato, ,mambo mpwito mpwito,club raha leo show,mazungumzo baada ya habari,Usiku wa dansi,Watangazaji Christine Chakunogela,Jacob Tesha,Mickdad Mahamdu Mruma, naikumbuka pia idhaa ya biashara ya redio Tannzania na n.k n.k!!!!!!!
 
Nakumbuka kipindi cha maneeeeno hayoooo asubuhi na mapema nikiwahi kwenda shule ya msingi janjajanja.
 
Kwenye michezo alikua halima mchuka na ezekiel malongo( RIP wote)

Salamu namkumbuka Malima Ndelema. ( nakumbuka kulikua mpaka kuna klabu za salamu mojawapo ilikua Yataka Moyo salamu klabu)
 
Ukifika umefika utoke uende wapii RTD ( hilo lilikua tangazo lao ah ah ah kitambo)
 
Wazungu wanasema "Old is Gold" tulikua pembeni ya babu zetu tukifatisha wasoma habari.

Na kuna kale kamwimbo ukikasikia tu unajua mida wa kuamka kwenda shule...daah kalikia kanakata stim zooote.
Kumekucha jama kumekuchaaaaa na jogoo vijijini wanawika hata na jua mbinguni kinatoka Wazalendo amkeni tufanye kazi saaasaaa[emoji323] [emoji323] [emoji323] [emoji122] [emoji122] [emoji122] kweli nyakati zinasonga mbele.[emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120]
 
HIVI TAUSI ILIONYESHWA KITUO CHA K.B.C TV?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…