Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Nilikua mdogo na nilikuwa nacheza ule mlio unaotolewa kabla na baada ya matangazo ya vifo
 
M nakumbuka ka saut kale taarifa ya habari kabla ya kuanza ka saa mbili kamili
 
Hehee kama bado hujaoa basi oa broo.
 
Mkuu nimekukubali ila ungeongeza na misakato kila jumamosi asubuhi tunapata nyimbo mpya zinazorekodiwa halafu jioni kwa Uncle J.Nyaisanga anaposema "kwa mara nyingine tena,radio Tanzania Dar es alam yawaletea CLUB RAHA LEOOO....shoooooooo.." bila kusahau jumapili mchana sauti nzito ya David Wakati kipindi nipe habari,halafu asubuhi kuanzia saa mbili unusu asubuhi NJOO TUIMBE SOTE hapa luteni john komba ndo alipotokea na kwaya zake,ila nakumbuka kwaya moja sikumbuki aliimba nani "mtaje mtaje kiijanaa aliyekupa mimba saakina dada.....
 
Kale ka mziki kipindi cha majira saa tatu umekasahau duh we jamaa una kumbukumbu sana
 
Jumapili saa nane mchana ilikuwaga ni kipindi cha MAMA NA MWANA.
 
Aisee Mtoa mada umenikumbusha jinsi nilivyokuwa naigiza sauti ya Bakari Msulwa akisoma habari. Zaidi sitakaa nisahau kipindi cha Kombora cha saa 11 asubuhi hasa ule mziki na jamaa akianza kwa kusema "Komboraaa" hapa siku moja nikiwa mdogo sikulala nikisubiri siku inayofuata kuanza safari ya kwenda mjini Arusha kutoka kijijini kwa mara ya kwanza. Basi nlivyosikia Komboraaa nikaruka kwa furaha.
 
Nakumbuka enzi hizo ulikuwa unanunua daftari alafu unanunua big G kisha zile big g ndani zilikuwa zina stika za wachezaji wa mpira wa kizamani kisha unatafuna big g ikishaisha utamu unabandika picha katika daftari alafu unashinda na mwenzako picha za wachezaji au vikosi vya timu kama wanazo
enzi hizo wakina;
1.Zenden
2. Kaptain Dunga
3. paul ince
4.davo sukar
5. edga david
6. oliver khan
7. zidane
8. emanuel petit
9. a. nesta
10 dino baggio
11. Lizarazu
12 ben mc carthy
13 okocha
14 hierro
15 kruivet
16 seedorf
17 Marc Overmars
18 Alan shearer
19 diego simeone
20. g. batistuta.
 
kuna kile kipindi cha kuwatembelea wagonjwa hospitali then wanatuma salam.....mtangazaji kanitoka.... nakikumbuka sanaaaaaa
 
Nikizikumbuka hizo nyakati huwa nalia mwenyewe kwa uchungu......
Huwezi ku rewind wakati,Ingekuwa inawezekana na hizi shida za dunia mie ningerudi umri wa Chekechea!!tena ningekimbilia[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] daa maisha nayatunisha misuli[emoji123] [emoji123] [emoji123] [emoji123] [emoji123]
 
Hiyo ilikuwa ya kuanzia kipindi ya kumalizia ubeti.ulikuwa hivi:

kwaherini watoto wote
tukutane juma lijalooo
msikose kipindi cha watoto
asanteni kwaherini woteeee.

Ilikuwa lazima ujongee redioni wakti ukitaradad
Daah umenikumbusha mbali na mpk nikamkumbuka marehemu mdogo wangu,tulikua tunashindana kujibu maswali yaliyokua yanaulizwa redioni km methali,nahau,mafumbo etc.da Mungu muacheni aitweni Mungu
 

Hahaha mule mule kwy reli! Noma sana. Ile jingle ya majira usiku saa tatu naikumbuka sana.Baada ya majira wote kwenda kulala daah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…