Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Siku hizi redio zimekuwa fujo tupu vipindi vyafanana na hujui usikilize redio ipi ilimradi tu tafran,na redio nyingi wanahusudu miziki
Halafu ni special kwa wenye ving'amuzi.Minara ya mawasiliano ime-haribu.Vijijini wenye uwezo mdogo mf wasio na umeme hawapati lolote.Mambo yamebadilika sana. Maisha ni mchaka mchaka[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Pia watangazaji wake mahiri ambao walikuwa wanatangaza kitaaluma hasa kwa kufuata maadili kama akina
Deborah mwenda
Eda sanga na wengineo nimewasahau akina kipozi kama hivyo. Siku hizi ukijua kuongea sana tu umepata kazi hata ethics huzijui mwisho wa siku watu wanakejeliana watangazaji wanaona ni lugha laini tu khaaa!

wewe unawakumbuka watangazaji gani wengine mwenzangu
Mie naona RTD ilibamba AFRICA MASHARIKI kwa umakini na ratiba nzuri za utangazaji.
 
RATIBA ZA UTANGAZAJI NA VIPINDI VYA WAKATI ULE VILI REFLECT MAISHA HALISI YA ZAMA HIZO. KUMBUKENI WIMBO WA MWANAMEKA MPIGAJI AMENITOKA KIDOGO ULIINGIA KWENYE SYLABUS YA KISWAHILI O-LEVEL.
 
Kusema za ukweli siku hizi hakuna watangazaji bali kuna waropokaji na wapiga domo huko studio.......baada ya kuelimika kupitia vyombo vya habari jamii ndio kwanza inahiribiwa........hakuna kipindi chenye manufaa kwenye jamii zaidi ya kuitangaza zinaa na matendo ya ngono.......
Matukio ya wasanii kufanya ngono ndio yanayopewa kipaumbele kuliko matukio mengi ya msingi yanayozinguka jamii zetu.....

Mtangazaji ukimuona mtaani mpaka unashindwa kumtofautisha na watumiaji wa mihadarati kwa jinsi alivyo na muonekano mbaya.....
 
Mkuu nimekukubali ila ungeongeza na misakato kila jumamosi asubuhi tunapata nyimbo mpya zinazorekodiwa halafu jioni kwa Uncle J.Nyaisanga anaposema "kwa mara nyingine tena,radio Tanzania Dar es alam yawaletea CLUB RAHA LEOOO....shoooooooo.." bila kusahau jumapili mchana sauti nzito ya David Wakati kipindi nipe habari,halafu asubuhi kuanzia saa mbili unusu asubuhi NJOO TUIMBE SOTE hapa luteni john komba ndo alipotokea na kwaya zake,ila nakumbuka kwaya moja sikumbuki aliimba nani "mtaje mtaje kiijanaa aliyekupa mimba saakina dada.....

Duh....wee mkali..... umeukumbuka hadi wimbo wa sakina?
Nimesoma maneno tu sauti ikaja....Big up...you made my morning
 
Jumapili saa nane mchana ilikuwaga ni kipindi cha MAMA NA MWANA.

Ilikuwa ni siku ya jumamosi na mama Debora Mwenda akiwa hayupo basi Aleicia Maneno anasimamia kipindi. tulikuwa na club za mama na mwana mashuleni, mkiandika barua yenu siku hiyo ikasomwa kwenye kipindi manajiona niendio nie...lol tumetoka mbali
 
Ilikuwa ni siku ya jumamosi na mama Debora Mwenda akiwa hayupo basi Aleicia Maneno anasimamia kipindi. tulikuwa na club za mama na mwana mashuleni, mkiandika barua yenu siku hiyo ikasomwa kwenye kipindi manajiona niendio nie...lol tumetoka mbali
Nakumbuka mwaka 1983 nikiwa std 7 nikiandika barua yangu kwenye kipindi cha mama na mwana kisha ikasomwa daa kijijini kwetu nilizua ujikooo! niliwachorea zawadi ya bata teh teh teh!![emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122]
 
radio csssete maarufu enzi hizo ilikuwa ni memory Q!!

Your correct. Nakumbuka nilivyunja mlango wa redio upande wa kuwekea kanda......niliweka kanda, kumbe haijakaa vizuri mie nikang'ang'aniza kufunga mlango, kutahamaki mlango umevunjika, kipigo nilichokipata kutoka kwa mother sitakaa nisahau
 
kipindi hiki ndio hamjataja "mashairi" msomaji Athuman Khalfan saa nane nane mchana!
 
Nakumbuka nilikua sifaham maana ya kipindi cha "club raha leo shoooow" kikinikera kweli kikianza! Na hakuna station nyingine kubadilisha labda tuweke cassete ya UB40! Time hizo baba awe hajarudi home lkn, akirudi hatuna tena access na radio! Those were days

kulikua na idhaa ya biashara, idhaa ya Taifa na external service. hakuna cha zaidi. Jumapili watoto wa geti kali lazima tusikilize "At your request"
watuma salamu kwenye kipindi hiki ni kutoka Oysterbay, Upanga na Chang'ombe kidogo. Uswahili wanatoka Magomeni mikumi.
Namkumbuka sana Jacob Tesha, na sauti yake. Sauti yako ndio qualification yako ya kutangaza radio, vinginevyo unakua fundi mitambo. Kama hujui kutofautisha L na R au H na A, kutangaza radio sahau. Mwenye lafudhi ya kabila lake pia sahau, fanya kwenye mitambo kule, usiharibu shughuli. Ilikua raha sana. Siku hizi hata hamu ya kusikiliza ina bore hasa ukikutana na mtangazaji asiyejua kutofautisha R na L au A na H
 
RATIBA ZA UTANGAZAJI NA VIPINDI VYA WAKATI ULE VILI REFLECT MAISHA HALISI YA ZAMA HIZO. KUMBUKENI WIMBO WA MWANAMEKA MPIGAJI AMENITOKA KIDOGO ULIINGIA KWENYE SYLABUS YA KISWAHILI O-LEVEL.

wimbo wa Marijani Rajab huo
 
Kwa kweli nilikuwa mtoto lakini kuna kipindi cha maigizo cha akina mzee jangala ambapo kuna sauti ilikuwa ikisikika "ung'waaa anhaaa haa dukudukuuu msondo ngoma"
 
1.Michezo na Abdul Omar Masoud na Juma Ngondae
2.Club Raha Leo show na Brother Enock Ngombare
3.Usiku wa Raha na Debora Mwenda/Halima Mchuka
4.Malimwengu
5.Mazungumzo baada ya habari na Salum Seif Mkamba
6.Majira na Mshindo Mkeyenge
7. From me to You (External service)
 
Mazungumzo baada ya habari pamoja na maneno hayoooooo


Hali kadhalika ujumbe wa leo, "......waswahili wa Darisalama wananambia Mwl hatuna pesa, najiuliza pesa nizitoe wapi kama hatutaki kufanya kazi......"
 
Back
Top Bottom