Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

HAPA UMENIPELEKA MOJA KWA MOJA IDHAA YA BIADHARA YA REDIO TANZANIA. [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122]
 
matangazo ya vifo tuu, kutwa mara saba.
 
Reactions: ram
Kipindi cha club raha leo show na kile cha "noon spin" external service kila siku saa 6 mchana , walikuwa wanasikiliza mabrazamen na msisita duh. Kazi kweli
Umesahau idhaa ya biadhara special kwa vijana wa enzi hizo. Na idhaa ya taifa na kipindi cha mkulima wa kisasa special kwa wazee
yaaani we acha tu mtoa thread kanikymbusha Zama!!
 
Jamani mwenye CLIPS za sauti za vipindi mbalimbali atuwekee. Nikumbuke kijijini kwetu KILOMENI Wilaya ya Mwanga Kilimanjaro na redio yetu maarufu kama dudu proof (277) na alama ya MENDE aliyepigwa mkato. Ya kale ni dhahabu!!
 
Nimekumbuka huu wimbo maarufu enzi zile;
Chama chetu kimetuongoza
Kulenga lengo la ujamaa
Mwenyekiti Mwaliomu Nyerere ni mjenzi mwenye wingi wa sifa Tanzania

Ewe TANU nguzo yetu madhubuti kwa hakika, ...mwenyekiti Mwalimu Nyerere ni mujenzi mweney wingi wa sifa Tanzania...

Asiyejua kufa....mwambie aone kaburi.... mwenyekiti Mwalimu Nyerere ni mujenzi mwenye wingi wa sifa Tanzania

Vv
 
radio csssete maarufu enzi hizo ilikuwa ni memory Q!!
 
Umesahau idhaa ya biadhara special kwa vijana wa enzi hizo. Na idhaa ya taifa na kipindi cha mkulima wa kisasa special kwa wazee
yaaani we acha tu mtoa thread kanikymbusha Zama!!
Upo sahihi,idhaa ya biashara ilikuwa ni special kwa mashirika ya umma - kabla mtangazaji hajaanza mambo yake alikuwa anatuomba tuburudike kwa Muziki.
Unakumbuka kipindi cha Muziki na BP cha uncle J Nyaisanga, kila jumatano saa 1:15 jioni, hapo ndio tulikuwa tunapata vitu vipya kabisa toka majuu?
 
Kipindi cha club raha leo show na kile cha "noon spin" external service kila siku saa 6 mchana , walikuwa wanasikiliza mabrazamen na msisita duh. Kazi kweli

Pia kulikuwa na kipindi cha MISAKATO kila Jumamnosi saa 3 asubuhi, kulikuwa na nyimbo mpya za wiki. Watayarishaji na waongozaji wa kipindi walikuwa wanapokezana Uncle J Nyaisanga, Michael Katembo, na Henry Michael Libuda. Walikuwa pia ni watayarishaji na waongzaji wa kile kipindi cha Club Raha Leo. wote hao ni marehemu, miaka inakwenda loh.

Vv
 
UNCLE J (R.P.I)
 
mimi nakumbuka kawimbo flani amazing ka afya yetu,KULENI KUKU MAYAI CHAKULA BORA JAMANI,CHA KUUJENGA MWILI,MBOGA SAMAKI MAZIWAA!
 
UNAKUMBUKA KIPINDI CHA AFRICA JOURNAL? Habari za wiki nzima za Africa hasa O.A.U.
 
WAZEE JF SIJUI TUPO WANGAPI! NILI REKI FACE BOOK SIKUONA HATA MZEE MMOJA (vijana wa enzi hizo) especial waliomaliza form four mwaka 1988 sijui wazee ni stress na majukumu au vip. inasikitishaaaaaa!!!
 
Walikuwa wananikera na ile miziki yao ya makabila SIPATI PICHA!
 
Nadhani betty Chalamila ndo baadae aliolewa na kujiita betty Mkwasa.kwao ni mafinga Iringa maeneo ya KINYANAMBO!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…