Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Ni shida mkuu!
 
Ivi yule jamaa wa mazungumzo baada ya habari na maneno hayo alikuwaga nani maana alikuwa na maneno kuntu sana yule jamaa! Yuko wapi na anajishughulisha na nini?
Mzee Paulo Sozigwa
 
kipindi hiki ndio hamjataja "mashairi" msomaji Athuman Khalfan saa nane nane mchana!
Halafu ijumaa mchana waumini wa dini ya kiislamu watakumbuka sauti tulivu ya mufti wao sheikh Hemed bin Jumaa bin Hemed akitoa mawaidha kwa upole na uhakika tena bila jazba....mpaka sie tusio waislamu tulikuwa tunavutiwa kusikiliza...
 
Betrii ilikuwa shida. Wakati wa redio za Memory Q, kuna mtu kazi yake ilikuwa Ku rewind kwa kutumia peni ya Bic wakati huo kwenye redio ndio alikuwa na mamlaka ya kusema. Hata akisema uongo haikuwa busara kubishana naye!!
 
Kwenye michezo alikua halima mchuka na ezekiel malongo( RIP wote)

Salamu namkumbuka Malima Ndelema. ( nakumbuka kulikua mpaka kuna klabu za salamu mojawapo ilikua Yataka Moyo salamu klabu)
Hiyo mbona juzi tu! Mwenyewe alikuwa akiitwa Abdul Masudi Jawewa(JAW).
 
Betrii ilikuwa shida. Wakati wa redio za Memory Q, kuna mtu kazi yake ilikuwa Ku rewind kwa kutumia peni ya Bic wakati huo kwenye redio ndio alikuwa na mamlaka ya kusema. Hata akisema uongo haikuwa busara kubishana naye!!
batery za Nationa ilikuwa deal mjini,kidogo za phillips utapata...,zikizingua unazibonda bonda na kuzianika juani huku unazilinda...
 
Hivi wakuu TBC wanaweza kuwa na backup ya vitu vya zamani. ..mfano...audio clip za Jingles na signature tunes za vipindi mbalimbali. ..kipindi kama cha Bima yako, sayansi na teknolojia(hii iliimbwa na Marehemu Capt.Komba)..na nyingine kama alizotuonjesha mleta mada.

Nadhani kama wanaweza ku compile hivi vitu kwa watu wanaopenda kujikumbusha uzalendo wakajipatia kumbukumbu. Au ndio issues za copy right labda itakuwa shida.
 
Nilikuwa sikipendi... kikiisha hicho kipindi kinakuja kipindi cha ombi lako ambacho baade kilibadilishwa jina na kuwa chaguo la msikilizaji
Hapo ombi lako umenigusa!mishale ya saa tisa mchana hivi,nilikuwa navizia nyimbo za msondo hapo...
 
Nilikuwa sikipendi... kikiisha hicho kipindi kinakuja kipindi cha ombi lako ambacho baade kilibadilishwa jina na kuwa chaguo la msikilizaji
ram uko fit...,nilikuwa najaribu kukumbuka hiyo ombi lako ikawa inagoma.
 
Mkuu nashukuru kwa kujazia, sikuthibitisha iwapo tulipigwa ndio maana nilisema inasemekana.
Ila hilo la Kivuyo na Jerry Muro umenivunja mbavu.
 
Halafu ijumaa mchana waumini wa dini ya kiislamu watakumbuka sauti tulivu ya mufti wao sheikh Hemed bin Jumaa bin Hemed akitoa mawaidha kwa upole na uhakika tena bila jazba....mpaka sie tusio waislamu tulikuwa tunavutiwa kusikiliza...
Mimi ni Mristo - ila kila ijumaa saa 8:02 alasiri nilikuwa sikosi kumsikiliza Mufti Hemed Bin Jumaa bin Hemed, ki ukweli yule mzee Pengo lake halitazibika.
 
Mkuu uko vizuri, nimejikuta nacheka tu, hiki kipindi kilikuwa siku ya jumapili saa mbili asbh, watoto wa shule fulani wanajiachia kwa nyimbo, hadithi n.k bila kusahau historia ya shule. Mwavita makamba, aliwahi kushiriki hiki kipindi wakati huo mzee makamba ni mkuu wa mkoa wa kigoma
 
mwanamke wa kwanza kutangaza kipindi cha michezo saa mbili kasoro usiku alikuwa Sarah Dumba (RIP)
Hivi dada Sara kesha tangulia??? Rip sauti yake we hakuna siku hizi wa kumuiga.
 
Hivi dada Sara kesha tangulia??? Rip sauti yake we hakuna siku hizi wa kumuiga.
Kweli usemayo,ilikuwa sauti ya pekee.Yes alishatangulia sikumbuki vizuri kama ilikuwa ni mwishoni mwa mwaka jana au mwanzoni mwa mwaka huu akiwa mkuu wa wilaya katika moja ya wilaya kama sio mkoani mbeya basi ni mkoani iringa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…