Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

I felt sorry for him kuna mgombea ububge mmoja sijui nani alitishia kumtoa kws mandata km angeandika hbr zake ndio akajiua. Nilikuwa napenda sana aliyvyokuwa anaongea

Ni kweli mkuu, huyu alikuwa ni mmoja wa favourites wangu hasa eneo la maziwa makuu ambapo nilikuwa nikimsikiliza tangu early 90s.

Aliwakilisha BBC kwa miaka 10 mfululizo, hivyo alikuwa ni mmoja wa experts kwenye eneo hili.
 
Kuna dada mmoja Regina Malekwa sasa Regina Mziwanda alikuwa anaendesha kipindi cha phone ins pale radio Tumaini in early 90s.

Nafikiri sasa yupo BBC.

Alikuwa anafurahisha kwa uhodari wake wa kuongoza zile phones ins za masuala mbalimbali has ya siasa.
 
Ni bonge la mdada love her kwa kweli. Kuna watu na vipaji sio saaa naona watu wanaongea pumba tu wengi wamevamia au tuseme wanalazimisha fani. Wengine wapenfa sifa wanaonga vitu havina ht ladha. Maadili yanashuka viwango.
 
Kulikuwa na watangazaji mahiri kama kina Bujaga Izengo Kadago,Omar Jongo,Ahmed Jongo,Nadhir Mayoka,Rashid Idd Mchata,Edda Sanga,Salah Dumba,Bett Chalamila,Sunday Shomari,Omar Liongo,Abdalah Majura na wengine wengi tu

daah Abdala Majura!!!!
 
Kilikuaga chuma hiki... Very byutiful. Enzi za akina marehem John Ngahyoma kule ITV. Hivi yule Asma Basafar aliendaga wapi yule mmama?

John Ngahyoma ni RIP tayari km sikosei....
 
asante sana , tafadhali naomba unitumie kale ka wimbo kabla ya kipindi cha michezo kuanza
 
Umenipeleka mbali mdogo wangu. Mimi siku hizo tunatoka Seko, tukifika nyumbani siku za j. pili utapewa escort hiyo halafu mkirudi wanapelekwa chemba, hivi mliona nini? Sisemi zaidi inawezekana mdogo wangu akawa humu akaniumbua. We tulipigwa kwenda disko za mchana na hali ni saa nane mpaka 12. Mkirudi mhahesabiwa jua limetua ziwani au la lakini we acha tu.Huo urithi wanetu wameukoasa. Wacha waukose viboko vya wakati huo we! Walitusaidia maana mtu kusikia kijijini mtu kapata mimba inabidi atoroshwe apelekwe mbali. Sasa hivi maisha ndivyo yalivyo.
 
kuna ule wimbo wa issa matona kamasikosei hongera mwanangu eeh hongera,mida ya saa saba hapo njaa ishanikong'oli kinoma mama alikuwa anakipenda sana hicho kipindi
 
Hivi niliweka matangazo ya vifo? Wote kimya maana ndo simu za vijijini. Sikuwahi ona simu mpaka nilipoenda mjini ofisini nimeenda kwa shughuli zangu za kishule nikiwa darasa la 7. We kuona watu wanaongea unafikiri wanaongea na jini.
 
Mi Nakumbuka ubovu wa radio kipindi kile maana usikivu kama uko mikoani ulikuwa mbovu sana.
 
Kuna tangazo la bia ya "tusker" wanakuambia " baada ya kazi burudika na tuskerrrrrrr" nkamwambia baba niletee hiyo tusker niburudike akacheka sana ila kaniletea Pepsi cola
 
Teh na Jpili Mama na mwana
Na kale kawimbo kao
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…