Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Siyo kweli. Amin alipigwa moja kwa moja toka vita ilivyoanza, japo kulikuwa na majibizano hapo Lukaya na mahali panaitwa Luweero na Kapeeka. Wakati wote huo, Ben Kuko alikuwa ni burudani tosha kwa ripoti zilizokuwa zibawakejeli askari wa Amin, unaweza kumlinganusha na Jerry Muro lakini kwa sauti ya Hemedi Kivuyo anapokuwa anainanga timu yenu iliyofungwa!!
Na sasa umenikumbusha nyimbo zilizokuwa zinapigwa wakati huo kama ule usemao; "Amewaua ndugu zetu bila kosa lolote masikini....ooh mungu warehemu ndugu zeetu,ameaua na watoto wasiojua lolote masikini...ooh jama,malaika wa muungu...",na ule wa " kufyeka fyeka pori tumkamate nduli huuyoo,tutamkata na kumnyoa manyoya yake...."
 
Kweli usemayo,ilikuwa sauti ya pekee.Yes alishatangulia sikumbuki vizuri kama ilikuwa ni mwishoni mwa mwaka jana au mwanzoni mwa mwaka huu akiwa mkuu wa wilaya katika moja ya wilaya kama sio mkoani mbeya basi ni mkoani iringa.
Ni marehemu Sara Dumba. Alifariki March 22 mwaka huu akiwa mkuu wa wilaya ya Njombe.
 
Halafu ijumaa mchana waumini wa dini ya kiislamu watakumbuka sauti tulivu ya mufti wao sheikh Hemed bin Jumaa bin Hemed akitoa mawaidha kwa upole na uhakika tena bila jazba....mpaka sie tusio waislamu tulikuwa tunavutiwa kusikiliza...
Mola amrehemu mufti Hemed Bin Juma
 
batery za Nationa ilikuwa deal mjini,kidogo za phillips utapata...,zikizingua unazibonda bonda na kuzianika juani huku unazilinda...
Ha ha ha haaa.. Hii comment imenichekesha alfajiri yote hii...
 
dominic chilambo mtangazaji wa mfano kwangu mbwembwe na madoido ya kutosha!!
Sisahau kipindi cha chaguo la msikilizaji na mama na mwana hadithi taamu ya adili na nduguzeee wachaaa hakika zilikuwa enzi tamu!!
 
Mkuu

Jamaa wa Mazungumzo baada ya Habari alikuwa ni Salimu Seif Mkamba almaarufu S.S.Mkamba, au walikuwa wanapokezana na Paulo Sozigwa ?
Paulo Sozigwa ndiye alikuwa mwandishi maana alikuwa "party ideologue". Wakati mwingine Moses Nnauye naye alikuwa anachangia
Mkuu nashukuru kwa kujazia, sikuthibitisha iwapo tulipigwa ndio maana nilisema inasemekana.
Ila hilo la Kivuyo na Jerry Muro umenivunja mbavu.
 
Umesahau idhaa ya biadhara special kwa vijana wa enzi hizo. Na idhaa ya taifa na kipindi cha mkulima wa kisasa special kwa wazee
yaaani we acha tu mtoa thread kanikymbusha Zama!!
Hili neno limenipa shida kidogo kulielewa. Ila baada ya kujua kuwa unatokea Kilomeni nimelielewa.
 
Namkumbuka ezekiel malongo katika utangazaji wa mpira sauti yake ilikuwa inanogesha unataman usikilize redio kuliko kuangalia tv
 
baba alikua akitoka asbh anatoa betry anaficha,akitoka kazini ndo anawasha radio,saa 8 ucku,nakumbuka enzi hzo mech zilikua znachezwa ucku,hv kwanin cku hz hakuna?
 
Naomba mnikumbushe mtangazaji wa kipindi cha ngoma zetu. Alifariki kitambo ila alikuwa na sauti nzuri na vituko akiweka ngoma za wajaluo kwa sana.
 
1.Michezo na Abdul Omar Masoud na Juma Ngondae
2.Club Raha Leo show na Brother Enock Ngombare
3.Usiku wa Raha na Debora Mwenda/Halima Mchuka
4.Malimwengu
5.Mazungumzo baada ya habari na Salum Seif Mkamba
6.Majira na Mshindo Mkeyenge
7. From me to You (External service)

Hivi hiyo "External Service" bado ipo ...daaaa na kile kiingereza chao cha kusoma, yani hakuna kumungunya maneno kama siku hizi.... ila nilikuwa siielewagi
 
mahokaa!!!!! kuna mzee mmoja alikua anacheka sana mwanzo wa kipindi "we mama mbavu zangu ha! ha! haaaa!"
 
Back
Top Bottom