Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Nilidhani wa zamani kweli ili tutaje akina Hamza Kassongo, Sango Tua...
 
Salama Mfamao RIP
Aloysia Isabula
Aloysia Maneno
Peter Makorongo
Suleiman Kumchaya
Juma Ngondae RIP
Mshindo Mkeyenge
Abdallah Mlawa
Siwatu Luanda RIP
Salim Mbonde
Omary Masoud RIP
Pascal Mayalla
Adam Mwaibabile
etc....

ongezea;
John Luanda
 
Yaani we ndo umenikumbusha enzi hizooooo............Kwa kweli siku zikipita na mambo yanapita. Kumbuka hilo shati la shule umeweka wanga au blue ling'ae.......!!!! halafu linadondokewa jivu...!!

Hahaha dah tena blue yenyewe ndio ulinunuliwa kidonge ndio umekimalizia then jivu linaangukia mhh! Hapo nishang'arisha mokasini zangu na kiwi! Na begi langu la mgongoni nasubiri monie enzi hizo begi la mgongoni anasa!
 
Umemshau,Salama Mpamao,si mbaya nikiwataja na hawa,Mzee Jangala,Kiatu,Tomato,Mshamu,Igunanilo,Mzee Mundu na wengineo ongezea.
TBC mi nadhan siyo mbaya kwani kuna KBC, UBC, SABC n.k n.k
Ila kwa wakati ule RTD ilibamba sana. Vipindi kama majira, jambo, mchana mwema,chaguo la msikilizaji, kutaja vichache vilinikuna sana.
 
kipindi cha pokea salamu kitu saa sita na ugali kwa mbaali unanukia....jioni saa moja moja kipindi cha kahawa yetu...
 
Wengi washajimalizia career zao kwenye politiki

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
afu kipindi kama hiki cha kuendea sikukuu kulikuwa na kipindi kinaitwa mshindi ni nani?
 
TBC mi nadhan siyo mbaya kwani kuna KBC, UBC, SABC n.k n.k
Ila kwa wakati ule RTD ilibamba sana. Vipindi kama majira, jambo, mchana mwema,chaguo la msikilizaji, kutaja vichache vilinikuna sana.

Hakuna haja sana ya kuwafuata hao, watu kama Uganda hawana lugha inayowaunganisha. Kwanini tusiwe tofauti?
 
omar jongo zamoyoni mogela anaachia shuti linapiga mtamba panya. refa ndo mwamuzi wa mwisho akisema haya ni mapanya ni mapanya tu.ananakwenda alafu mic inaachiwa mashabiki alafu unasikia ni kona boli au goli kiki au ni penalti maguu kumi na mbili ya mtu mzima. wakati ule tulikuwa tunatuma telegram kuzitakia timu ushindi, baada ya mechi wanarudi studio unapigwa wimbo wa mabruki wa maquiz,
 
Kuna mtangazaji nimemsahau alitangaza mechi ya Yanga na Milambo Kilimanjaro premium league kesho yake tukatangaziwa kafariki ilikuwa kama 1993/4. Nani anamkumbuka huyu mtangazaji?
 
Hivi TBC hawawezi angalau kila siku japo kwa robo saa wakatukumbusha vipindi vya zaman kwa kutuwekea saut za Watangazaji wa zamani wa RTD?Club Rahaleo show, misakato da we acha tu. Kiashiria cha kipindi cha michezo kuanza we acha tu.
 
Wakati ule ilikuwa hivi: Hii ni ya Idhaa ya Biashara ya Radio Tanzania Dar es Salaam, sasa tunaungana na Idhaa ya Taifa kusikiliza Taarifa ya Habari. Baada ya kufutwa Idhaa ya Biashara ikaundwa External Service ya RTD.Baadae sana ndo ikaundwa PRT iliyounda TBC FM.Hata hivyo kwa sasa kuna pia TBC International kama replica ya External Services ya akina Abbisai Steven
 
External service ilikuwako wakati wa idhaa ya biashara mkuu

Tumewasahau
Suleiman Hega
Muhamed Dahman

Kipindi kile nikisikia ule mlio wa vipindi vya matangazo ya kifo ule mngurumo tu unajuwa kuna mtu ameondoka

Kile kipindi tulipofunguwa mipaka na Kenya na kuwaalika kwenye ule mkutano wa mwanzo kule Kizota, wale watangazaji wa Kenya walikuwa wakijuwa Kingunge ni moja ya cheo katika ujamaa wao walikuwa wakitangaza tunawaona hapa 'vingunge' wakiingia ukumbini kwenda kuhojiwa,
Siwezi kuisahau hii kwani nilikuwa Dodoma kipindi hicho
Wakati ule ilikuwa hivi: Hii ni ya Idhaa ya Biashara ya Radio Tanzania Dar es Salaam, sasa tunaungana na Idhaa ya Taifa kusikiliza Taarifa ya Habari. Baada ya kufutwa Idhaa ya Biashara ikaundwa External Service ya RTD.Baadae sana ndo ikaundwa PRT iliyounda TBC FM.Hata hivyo kwa sasa kuna pia TBC International kama replica ya External Services ya akina Abbisai Steven
 
Nawakumbuka wote kwa upendo mkubwa, waliunganisha taifa letu na mchango wao hasa wakati wa vita dhidi ya nduli Idd Amini, ni wa kujivunia, popote walipo, wawe proud, walitimiza wajibu wao
 
kipindi cha pokea salamu kitu saa sita na ugali kwa mbaali unanukia....jioni saa moja moja kipindi cha kahawa yetu...

kuna kile kipindi cha chuo cha ushirika moshi, kuna dada alikuwa na sauti sio mchezo

enzi hizo ikifika mida ya taarifa ya habari na mazungumzo baada ya habari nyumba nzima inakuwa kimya mzee ndio anaimiliki redio, full nidhamu, full uzalendo
 
Mi nakumbuka tangazo la National bank of commerce ndio bank yetu sote na ni bank ya kisasa lilikua linaletwa wkt wa mchezo wa redio. Nlikua nakipenda sana kipindi cha wkt wa kazi, jambo na kile cha wagonjwa nshakisahau jina, apo huletwa nyimbo motomoto
 
Club Raha Leo kilikuwa kinaongozwa na Julius Nyaisanga,Henry Michael Libuda na Enock Ngombare Mwiru
 
Back
Top Bottom