naumbu
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 4,717
- 8,083
hivyo karim besta hayupo abood tv huyu? amefariki lini?
Dah wote nilikua na taarifa nao kasoro huyo Besta nakumbuka enzi zao RTD na baadae DTV
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hivyo karim besta hayupo abood tv huyu? amefariki lini?
Ni TSJ na sio DSJ!. Ndicho tulichosoma sisi, kilikuwa Ilala Shariff Shamba ndani ya campus ya BASATA, kilipohamishiwa UDSM, eneo liule ndipo kikaanzishwa DSJ.
Pascal.
Pascal unaweza kujua kama Angalieni Mpendu tunae? Na kuna kile kipindi cha 'Hisia na Muziki' kilikuwa poa sana
nafikiri ninayemtafuta ni yule wa itv enzi hizo na kipindi cha kitimoto yuko wapi yule bwana?
Nimemkumbuka Hassan Mgumba kama sijakosea jina na kipindi chake cha matukio ya wiki
enzi hizo kwa sisi wa mpakani tunaipata RTD usiku pekee tena kwenye shortwave
Tulitegemea zaidi raidio za Kenya.
Kuna mwingine anaitwa Mrekoni alikuwa na kipindi chake kizuri cha karibu mgeni au mgeni wetu alifariki majuzi
He was talented.
Nimemkumbuka Malima Ndelema, huyu alikuwa bingwa wa kipindi cha ngoma za asili za makabila mbalimbali, sijui yu hai bado au sijui yu wapi sasa huyu mtu.
Ni watu waliokuwa wanakupa sababu na kukulazimisha kusikiliza radio tofauti kabisa na sasa!
Asante kwa kunikumbusha, Saidi Omari Kassongo mmoja wa watangazaji maarufu miaka ile ya mwishoni mwa miaka ya 60. Kwenye bandiko langu namba 209 nilimataja kimakosa kama Salim(?) Asante sanaList imemsahau Radio DJ wa kwanza wa enzi hizo:-
Said Omar Kassongo.
Nakumbuka mitumbuizo yake na story nyiiiingi. Ama kweli wametangulia watu wa ukweli!
huyu mtu nimemuona zaidi ya mara tano mahali kwenye ofisi ya umma, ana makovu kama mtu alienguka na pikipiki, amechakaaa, ananuka pombe, na inasadikiwa ni mwandishi kanjanja.Takribani miaka kumi hv iliyopita,kabla rtd haijabadilishiwa jina na kuitwa tbc 2,alikuwepo mtangazaji mahiri wa habari za michezo na msoma taarifa za hbr nguli aliyeitwa ezekiel malongo.Huyu mwanahabari alinikosha sana enzi zake lkn siku hz simsikii kabisa na siju alikimbilia wapi.Mwenye taharifa zaidi kumhusu anijuze.
Baada ya kutimuliwa RTD (now TBC Taifa, maana pale Eda Sanga alikiuwa anamvumilia sana na mambo yake ya kulewa chakali ndo anakuja kazini), alikuwa anasimamia magari ya wanafunzi wa shule za Filbert Bayi (ambaye ni mjomba wake), akafukuzwa baada ya kuanza kuwakaza wanafunzi, then akawa dalali wa tiketi za mabasi pale Ubungo bus Terminal, napo akaacha, baadae akawa anashinda pale bar ya Rambo Manzese.
Kwa sasa yupo tu mtaani, ila kachoka sana, ukimuona utamuonea huruma kama vile mgonjwa.