Tujikumbushe: Waziri Magufuli alipotoa waraka wa mafanikio ya Rais Kikwete kwenye mambo ya ujenzi kuanzia mwaka 2005 hadi 2015

Hizo 3500KM unazosema kajenga JPM yeye kaja kumalizia kazi tu manake wakati yupo field kutafuta kura ile 2015, ujenzi wa hizo barabara ulikuwa unaendelea!
Ni muhimu ukazingatia kuwa barabara zina viwango tofauti vya ujenzi. Hizo KM 17762 ni barabara zote kwa ujumla lakini barabara za lami zilizokamilika kwa miaka 10 ni ,KM 5568 na km 3873 zilikuwa zinaendelea.

Ni kweli baadhi ya hizo zimekamilishwa kipindi cha awamu ya Tano. Hili ni jambo la kawaida katika ujenzi wa barabara, lazima kuwe na overlapping kwa kila awamu. Kwa trend hii ya Rais Magufuli zaidi ya KM 10,000 zitakuwa zimejengwa kwa kiwango cha LAMI ndani ya miaka yake 10.
 

Hizo kilometa 3500 unazosema JPM kazijenga, ni miongoni mwa zile kilometa 3873 ambazo Kikwete aliacha zinajengwa.

Taarifa ya hizo barabara unazozisema ni kwenye screeshot ifuatayo, tazama nilipowekea rangi nyekundu.

 
Namba zake nyingine kaweka za uongo. Kwa mfano 2.1.7 umbali toka Sekenke mpaka Shelui ni kama KM 12 tu na sio 33km alivyoweka
 
Namba zake nyingine kaweka za uongo. Kwa mfano 2.1.7 umbali toka Sekenke mpaka Shelui ni kama KM 12 tu na sio 33km alivyoweka

Hiyo ni ripoti ya Magufuli mwenyewe wakati akiwa waziri

Data za hiyo taarifa zinasapotiwa na mtandao wa TANROADS, angalia hapa Chini

 
Huu uzi nausave kwa ajili ya reference huko mbeleni
 
Bora kumchagua Rungwe kuliko Jiwe

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 

Fungua hiyo pdf niliyoweka kwenye attachment hapo mwanzoni mwa hii thread ukurasa wa 20, kisha uone Upembuzi yakinifu wa TAZARA -FLYOVER na Ubungo Interchange ilianza lini?. Kiufupi mpaka mwaka 2015 hiyo miradi upembuzi wake yakinifu ulishafanyika, kilichokuwa kinasubiriwa ni ujenzi tu

Ngoja nikuwekee screenshot

 
Siyo kweli Flyover ya Ubungo mkopo wake ulisainiwa tarehe 20 March 2017 . Ni Rais Magufuli aliyesimamia majadiliano yake na hatimaye mkopo kutolewa. Angalia hapa chini..
Duh!!

Kwahiyo unataka kutuambia Rais wetu kipenzi, mpenda wanyonge Bwana John Pombe Magufuli alilidanganya Bunge mwaka 2015 aliposema kwamba World Bank wamekubali kugharamia ujenzi wa Ubungo Interchange, au?!!

Yaani seriously unasema rais wetu mwongo?! Kweli?! I'm so sad kututukania rais wetu kwa matusi ya rejareja!!!

Mi nasema hivi, miradi yote ya flyovers Magu kakuta imeshafanyiwa kazi na financiers walishapatikana! Tafuta Final Report ya TANROADS ya January 2015 kuhusu Ubungo Interchange!!

Na usisahau, miradi aina hii negotiation upembuzi yakinifu na negotiation zinachukua muda mrefu kisha jiulize kama Final Report ilitoka 2015 zoezi zima lilianza lini!!

Sehemu ya ripoti hiyo inasema:-
Baada ya kuona hilo jambo ni inconvenience, ndipo TANROADS wakaja na idea kwamba:-
Na baada ya WB kuwa requested wakakubali kwa sababu mradi wa BRT ulikuwa chini yao, na construction ya interchange ilikuwa ni kwa ajili ya kuboresha BRT!

Ni kutokana na hilo, ndio maana JPM kwenye hotuba yake kama Waziri wa Ujenzi akaongea bungeni kwamba WB wamekubali kugharamia huo ujenzi!!

Hicho unachoona wewe kama JPM ndie kafanikisha ilikuwa ni mwendelezo tu wa BRT New Phase ambayo ni ujengaji wa interchange!! Tena hata hiyo habari uliyoweka wewe, hiyo ni sehemu tu ya full report!!!

Full Updated Report ni hii hapa chini, zingatia hapo nilipofanya bolding na RED:-

UTAONA hapo juu WB wanazungumzia mradi ule ule wa BRT lakini second phase!!!
 
Mkuu ingekuwa na vizuri ukaweka takwimu zako kwa kutaja maeneo/barabara zenyewe na urefu wake.
 
Mkuu ingekuwa na vizuri ukaweka takwimu zako kwa kutaja maeneo/barabara zenyewe na urefu wake.
 
Sijazungumzia suala km 17K bali nimejibu hoja yako uliyosema ndani ya miaka 5, JK kajenga 5.5K na JPM kakamilisha 3.9K, ndipo nikakukumbusha kwamba hizo 3 point something JPM kazikuta zinajengwa! Ina maana kila kitu kilifanyika kabla hajawa rais!!

Sasa kama zilikuwa ktk hatua mbalimbali, how come zote unazihamishia kwa Magu wakati yeye kaja kumalizia tu?! Hivi itakuwa ni sahihi kusema aiport Terminal III au Hospitali ya Mlonganzilwa imejengwa na JPM?
 
Mkuu tenganisha upembuzi yakinifu na financing ya mradi. Mradi unaweza kufanyiwa upembuzi yakinifu na ikachukua miaka kadhaa kupata financier. Ni vitu viwili tofauti. Ni kweli upembuzi yakinifu ya Ubungu interchange ilianza kabla ya Urais wa Mheshimiwa Magufuli na kampuni iliyokuwa ikifanya hiyo kazi ni Hamza Company ya Misri.
 
Duh!!

Kwahiyo unataka kutuambia Rais wetu kipenzi, mpenda wanyonge Bwana John Pombe Magufuli alilidanganya Bunge mwaka 2015 aliposema kwamba World Bank wamekubali kugharamia ujenzi wa Ubungo Interchange, au?!...

Mkuu tenganisha upembuzi yakinifu na financing ya mradi. Mradi unaweza kufanyiwa upembuzi yakinifu na ikachukua miaka kadhaa kupata financier. Ni vitu viwili tofauti. Ni kweli upembuzi yakinifu ya Ubungu interchange ilianza kabla ya Urais wa Mheshimiwa Magufuli na kampuni iliyokuwa ikifanya hiyo kazi ni Hamza Company ya Misri.

Kuna overlapping ya utekelezaji wa miradi. Kuna anayefanya upembuzi yakinifu na anayetafuta pesa. All in all ni kwamba Ubungo interchange imejengwa na Chama cha Mapinduzi chini ya usimamizi wa Mh Rais Magufuli akiwa Waziri wa Ujenzi na akiwa Rais. Ndugu yangu tumpe kura zetu aendelee kufanya maajabu mengine ya ujenzi wa barabara na interchange zingine, usishangee hata mtaani kwako lami itapita. Magufuli huyoooooo hadi 2025.
 

Flyover ya Tazara mkataba wa Ujenzi uliwekwa saini tarehe 15 October 2015 kati ya serikali ya Tanzania na wafadhili (Wajapani), wakati huo rais akiwa bado JK na kabla hata ya uchaguzi mkuu uliomuingiza Magufuli madarakani.

Kwa hiyo Financing ya mradi wa Flyover ya TAZARA ilitafutwa na kupatikana wakati wa JK
 
Man, jaribu kuelewa mtu anachosema, na ninarudia kwa ufupi labda maelezo marefu yanakuchanganya:-

1. Kauli ya JPM Bungeni akiwa waziri anasema:-
Benki ya Dunia imekubali kugharamia utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara za juu (Interchange) katika makutano ya Ubungo. Upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Interchange ya Ubungo umekamilika.
Ina maana maelezo hayo kwako yanazungumzia upembuzi yakinifu wakati umeambiwa wazi kwamba "..upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Interchange ya Ubungo umekamilika" na kwamba "Benki ya Dunia imekubali kugharamia utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara za juu."

Hiyo hotuba ilisomwa May 2015!!!

Na World Bank wenyewe wamesema wazi kwamba: "...foundation stone for the second phase of the BRT. It will entail the construction of the Ubungo Interchange."

Sasa mtu anayezungumzia suala la second phase ina maana itakuwa hufahamu kwamba huo ni mwendelezo wa first phase?!

Au hufahamu kwamba BRT inajengwa kwa phases tofauti tofauti lakini financier ni yule yule World Bank ambae HAKUTAFUTWA na Awamu ya V, na hata sasa sio kwamba atakuwa anatafutwa financier mwingine!!
 
Naomba kujua alisema lini na wapi
Na kama una video clip

Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
 
Kikwete alijenga Flyover ngapi ? Alinunua ndege ngapi ? Hii nchi ilichezewa sana ...
Hivi kutotumia akili mtaacha lini?
Hivi Hao waliotangulia wasingejenga barabara hizo fly over mgejenga wapi
 
Niwafahamishe kwamba kila kiongozi anakuja na namna yake ya kutawala kwayo hamna haha ya kulalamika kwani hata sasa ajira zipo na pia tumejengewa kujiamini na kuweza kujitegemea tuamke sasa magufuli kanuinua ni ukweli usiopingika
 
Tanzania hii hii au tanga na nyika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…