Tujionee kwanza haya maajabu ya Kikokotoo kwa Watumishi wa Umma

Tujionee kwanza haya maajabu ya Kikokotoo kwa Watumishi wa Umma

Unaambiwa Mtumishi wa uuma wa ngazi ya chini aliyefanya kazi serikalini kwa zaidi ya miaka 30. Anapostaafu analipwa 33% tu ya mafao yake.

Yaani kama mtumishi hiyo wa umma alistahili kupata milioni 100 kama mafao (kumbuka hii ni pesa yake halali aliyokatwa kupitia mshahara wake kwa miaka yote hiyo 30+), basi atapatiwa kiasi cha shilingi milioni 33 tu. Na kiasi kinachobakia analipwa kila mwisho wa mwezi kwa muda wa miaka 12! Ikitokea mstaafu akafariki wakati wowote ule baada tu ya kustaafu, na hicho kiasi nacho kinakomea hapo hapo (Wizi wa mchana huu [emoji2960])
Halafu kichekesho zaidi ni kwamba hiki kikokotoo ni kwa baadhi tu ya Watumishi wa umma! Mfano walimu, Manesi, Maafisa ugani, nk.

Ukija kwa Vigogo wa ngazi za juu, mfano Wabunge; eti wenyewe hawahusiki na hiki kikokotoo! (Ona ubaguzi na upendeleo wa wazi huu [emoji2960]) Ingawa na wenyewe eti ni watumishi wa umma!! Yaani wenyewe kila baada ya miaka 5 ya Ubunge wao, wanapatiwa mafao yao yote yanayokadiriwa kuwa kiasi cha shilingi milioni 250 za Kitanzania!

Ukija kwa vigogo wengine wa juu zaidi; mfano Rais, Makamu, Waziri Mkuu, Spika, na sasa wake wa hao vigogo; ikitokea wamestaafu! Wanapewa mafao yao yote! Na kila mwezi wanalipwa mshahara wa 80% kama ule wa Kigogo aliyeko madarakani kwa wakati huo kwa maisha yake yote! (Ubaguzi mwingine huu [emoji2960])

Swali la kujiuliza!! Kwa nini serikali mnawafanyia wafanyakazi wenu uonevu na wizi wa mchana kiasi hiki?

Mkiulizwa, mnatoa sababu za kipuuzi tu; eti wafanyakazi wakipewa hela zao zote kwa mkupuo wanaishia kuzitapanya na kutapeliwa, na mwisho wa siku wanakuwa masikini!! Sasa hao wafanyakazi wastaafu wakizitapanya hizo hela zao, nyinyi mnapata athari gani? Je, waliwaomba muwatunzie kupitia hicho kikokotoo chenu cha wizi?

Na kama mnaona ni muhimu kufanya hivyo, kwa nini msifanye mpaka kwa Wabunge? Je, ni kwa mini msitoe uhuru kwa Wastaafu kuchagua kama wanataka kupewa 33% pekee, au mafao yao yote?

Binafsi nimeandika haya malalamiko baada ya kushuhudia wastaafu fulani hivi niliopanda nao daladala sehemu fulani, wakilalamika kwa uchungu baada ya kulipwa mafao kiduchu kwa mfumo wenu huu kandamizi wa 33%.

Ushauri wangu kwa serikali; rejesheni mara moja kikokotoo cha zamani. Acheni kuwadhulumu wastaafu pesa zao.
Kumbe unaweza kuandika bila kulaza muandiko. Hongea Tate mkuu shegwashi
 
Acha uongo, mfano ma prof vyuoni walipata mpaka mil 30 tu. Kwa ufupi kila mfuko ulikuwa na fomula yake, ila kwa sasa inatoa fursa sawa. Nimemtukana kwa sababu ni mjinga anapotosha watu. Kikokotoo cha sasa kinamuwezesha mstaafu kuishi bila wasiwasi kwa sababu monthly pension ni kubwa na mstaafu akiiwekeza vizuri lumpsum kwenye miradi mbali mbali inamlipa vizuri hata kama ikitokea lumpsum imeisha anaweza kuishi vizuri. Mleta maada aacha uzuzu
HIyo sijuwi lumpsum,lapusamu hatuiiataji tunataka mzigo wetu wote tutajuwa wenyewe huko cha kufanya.We kama unakipenda kitumie.
 
Huu utaratibu ni mzuri sana. Nimeupenda na hongera kwa aliyeuweka. Kusema ukweli kumpa mfanyakazi eg sh milioni 100 zote kwa mkupuo ni hatari sana. Sh milioni 100 ni fedha nyingi sana kwa mlalahoi na anaweza kuzimia mara anapokabidhiwa kwa sababu alizoea kushika elfu laki mbili. Pia ni kuhatarisha afya ya watanzania na kuwafanya kunenepa kwa kula sana. Viongozi wakubwa ndiyo wanatakiwa kupewa fedha nyingi.
I wish ungekuwa ni mstaafu, halafu ukasema hivi; ningekuelewa sana. Ila naheshimu maoni yako.
 
Formula

[1/580]×N×APE×12.5×33%

Where:
1/580 = accrual factor
APE = The best three years avarage salary
12.5 =Avarage life expectancy after retirement
33% = pension lumpsum at retirement
N = Number of months contributed
Maliza kabisa.. weka figures.
 
Wewe idiot huna elimu ya kikokotoo, ni mbumbu na lijinga. Kikokotoo ni kizuri sana. Imagine anayelipwa mil 1,300,000 kwa mwezi anakuja kupokea 46 mil kama lumpsum, na bado kila mwezi atapata kama 500k, hivi huyu mtu akiamua kuiwekeza hiyo 46m kwenye duka au mifugo si atatengeneza kama laki tano zingine ukijumlisha anapata kama mil moja, compare na wakati wa ajira ana pungukiwa hela kidogo tu. Na hapo anakuwa na uhakika na cashflow yake.
Wewe sio chawa wa mama tu, we ni kunguni na kiroboto wa mama pia.
 
I wish ungekuwa ni mstaafu, halafu ukasema hivi; ningekuelewa sana. Ila naheshimu maoni yako.
Nimepiga kijembe ndugu yangu. Unadhani yametoka moyoni? Anyways, mimi msimamo wangu ni kuwa CCM inachezea na kudarau watazania kiasi ambacho inaweza kufanya vitu vya kufikirika. Hebu fikiria wana mpango wa kununua tena eti ndege ya viongozi? Kwa upande mwingine ni vizuri wanavyofanya ili wananchi waamke na kujitetea. Tumekuwa kama makondoo.
 
Wanatengeneza hizo formula ni watumishi wenyewe ama wakiwa ofisini ama kwa nyakati tofauti.

Acha kieapige hadi watakapo pata akili.
 
Yaani kama mtumishi hiyo wa umma alistahili kupata milioni 100 kama mafao (kumbuka hii ni pesa yake halali aliyokatwa kupitia mshahara wake kwa miaka yote hiyo 30+), basi atapatiwa kiasi cha shilingi milioni 33 tu. Na kiasi kinachobakia analipwa kila mwisho wa mwezi kwa muda wa miaka 12! Ikitokea mstaafu akafariki wakati wowote ule baada tu ya kustaafu, na hicho kiasi nacho kinakomea hapo hapo (Wizi wa mchana huu 🤭)
Halafu kichekesho zaidi ni kwamba hiki kikokotoo ni kwa baadhi tu ya Watumishi wa umma! Mfano walimu, Manesi, Maafisa ugani, nk.
Wabunge wote wasirudishwe bungeni 2025
 
Mnacholalamikia ni kitu gani?

Waopanga kikokotoo ni Wanasiasa Wabunge. Anayesaini iwe sheria ni Mwanasiasa Rais.
Wanaopata 80% hadi kufa wao na watoto wao ni viongozi wa Siasa.

Ni ninyi wale wale mkiambiwa kushirikia siasa , hamtaki kwa kauli ' mambo ya siasa hayanihusu''
Mkiambiwa muandamane ili tutengeneze mifumo yenye haki mnasema ninyi si Wapinzani.

Mkiambiwa mtumie 'voting block' kama Walimu, Wauguzi n.k. ili kuwafanya Wanasiasa wawasikilize, hamtaki kufanya hivyo badala yake mnatumia 'voting block zenu kama Chama cha Walimu' kumchukulia Form mwanasiasa.

Mtazungumzia kikokotoo na kitawazingua hadi siku mtakapo baini ni ninyi WAAJIRI wa hao Wanasiasa na kwamba siasa inaamua maisha yako ya kilas siku utake usitake.

Kukaa pembeni na siasa ni kusikilizia maumivu taratibu. Kusubiri Wapinzani wafanye ni kuahirisha maumivu.

Wenye hatma ya kikokotoo ni ninyi wenyewe mkiamua na mkitaka!

Tulieni sindano iingie.

JokaKuu Tindo Pascal Mayalla
 
Unaambiwa Mtumishi wa uuma wa ngazi ya chini aliyefanya kazi serikalini kwa zaidi ya miaka 30. Anapostaafu analipwa 33% tu ya mafao yake.

Yaani kama mtumishi hiyo wa umma alistahili kupata milioni 100 kama mafao (kumbuka hii ni pesa yake halali aliyokatwa kupitia mshahara wake kwa miaka yote hiyo 30+), basi atapatiwa kiasi cha shilingi milioni 33 tu. Na kiasi kinachobakia analipwa kila mwisho wa mwezi kwa muda wa miaka 12! Ikitokea mstaafu akafariki wakati wowote ule baada tu ya kustaafu, na hicho kiasi nacho kinakomea hapo hapo (Wizi wa mchana huu 🤭)
Halafu kichekesho zaidi ni kwamba hiki kikokotoo ni kwa baadhi tu ya Watumishi wa umma! Mfano walimu, Manesi, Maafisa ugani, nk.

Ukija kwa Vigogo wa ngazi za juu, mfano Wabunge; eti wenyewe hawahusiki na hiki kikokotoo! (Ona ubaguzi na upendeleo wa wazi huu 🤭) Ingawa na wenyewe eti ni watumishi wa umma!! Yaani wenyewe kila baada ya miaka 5 ya Ubunge wao, wanapatiwa mafao yao yote yanayokadiriwa kuwa kiasi cha shilingi milioni 250 za Kitanzania!

Ukija kwa vigogo wengine wa juu zaidi; mfano Rais, Makamu, Waziri Mkuu, Spika, na sasa wake wa hao vigogo; ikitokea wamestaafu! Wanapewa mafao yao yote! Na kila mwezi wanalipwa mshahara wa 80% kama ule wa Kigogo aliyeko madarakani kwa wakati huo kwa maisha yake yote! (Ubaguzi mwingine huu 🤭)

Swali la kujiuliza!! Kwa nini serikali mnawafanyia wafanyakazi wenu uonevu na wizi wa mchana kiasi hiki?

Mkiulizwa, mnatoa sababu za kipuuzi tu; eti wafanyakazi wakipewa hela zao zote kwa mkupuo wanaishia kuzitapanya na kutapeliwa, na mwisho wa siku wanakuwa masikini!! Sasa hao wafanyakazi wastaafu wakizitapanya hizo hela zao, nyinyi mnapata athari gani? Je, waliwaomba muwatunzie kupitia hicho kikokotoo chenu cha wizi?

Na kama mnaona ni muhimu kufanya hivyo, kwa nini msifanye mpaka kwa Wabunge? Je, ni kwa mini msitoe uhuru kwa Wastaafu kuchagua kama wanataka kupewa 33% pekee, au mafao yao yote?

Binafsi nimeandika haya malalamiko baada ya kushuhudia wastaafu fulani hivi niliopanda nao daladala sehemu fulani, wakilalamika kwa uchungu baada ya kulipwa mafao kiduchu kwa mfumo wenu huu kandamizi wa 33%.

Ushauri wangu kwa serikali; rejesheni mara moja kikokotoo cha zamani. Acheni kuwadhulumu wastaafu pesa zao.
MKUU MAMA ANAUPIGA MWINGI.....,NILISHASEMA NA LEO NARUDIA CCM WOTE NI MAJIZI HAWAJAWAHI KUWA NA UCHUNGU NA UMASKINI WA WATANGANYIKA, HAWA NI KUNDI LA PANYA WANAJALI MATUMBO YAO TU.NA FAMILIA ZAO, CCM NI WATAWALA NA SIO VIONGOZI
 
Naomba kujua, hii wanayopewa kila mwisho wa mwezi kama sehemu ya 67% yao iliyobaki,
Inahusiana na ile 50%( Nusu ya mshahara aliokua anapata kipindi yupo kazini) anayoipata kila mwezi?
Kama ulitakiwa kupata 150m wanakupa 45m ya Mkupuo. Hiyo 105m ndio wanakulipa kidogo kidogo Kwa miaka 12.5. Yaani hakuna Pensheni kama wale WA before 2022 July. Wale walipewa Mkupuo wao eg 150m na Pensheni ya kila Mwezi Hadi wafe. Za hawa Kikokotoo wameambiwa Walipewa zote Mifuko itafilisika. Hivi kwani Kwa Mwaka Wastaafu ni Wangapi? Inabidi Watengewe Bajeti Yao bcoz hawafiki hata elfu 10.
 
Hayati ndio alileta huu upuuzi.
Nakazia huu ni upuuzi wa Hayati.
Upuuzi huu aliuleta Hayati ni upuuzi wake.
Upuuzi huu ni upuuzi kama ulivyo upuuzi wake mwingine aliuleta hayati.
 
Wewe idiot huna elimu ya kikokotoo, ni mbumbu na lijinga. Kikokotoo ni kizuri sana. Imagine anayelipwa mil 1,300,000 kwa mwezi anakuja kupokea 46 mil kama lumpsum, na bado kila mwezi atapata kama 500k, hivi huyu mtu akiamua kuiwekeza hiyo 46m kwenye duka au mifugo si atatengeneza kama laki tano zingine ukijumlisha anapata kama mil moja, compare na wakati wa ajira ana pungukiwa hela kidogo tu. Na hapo anakuwa na uhakika na cashflow yake.
Mxiuuuuuu! Acha niishie hapa. Ukitia neno naanza upyaaa!
 
Back
Top Bottom