WELL SAID MKUU
Umetueleza jambo moja very sensitive, maisha ya sasa tumezungukwa na chuki, roho mbaya, unafki, ubinafsi na majungu. Roho zote hizi mbaya mzizi wake ni WIVU na kutakiana mabaya.
Kijana hakikisha hauna marafiki ambao hauna connection nao ya kueleweka. Hasa hawa uliokutana nao kazini au vijiwe vya pombe- Ulabuni na mtaani unapo kaa. Usipende kukaribisha marafiki hao nyumbani kwako, waishie kupaona kwa mbali, ikibidi kama nyumba ni ya kwako waambie umepanga, na wala usipende kushea nao mipango, mikakati na mafanikio yako. Hakika hao ndio watakao kukaanga mapema zaidi.
Mtu anakuja kwako kukutembelea kama mshkaji halafu huyo huyo anakuchora mambo yako anapeleka maneno kazini kuwa huyu jamaa anabonge la nyumba kajenga kwa mshahara upi? kanunua gari amemfungulia mkewe biashara anaishi vizuri kwa mshahara upi huyu lazima anakula rushwa au anapiga hela sehemu sio bure.....
Mambo ya kazini jitahidi yaishie kazini, mambo ya nyumbani na mtaani yaishie huko yasiende kazini. Kata huo mnyororo wa mahusiano kabisa. Kataa kabisa marafiki wakazini kuja nao mtaani. Hawa watu uliokutana nao kazini SIYO MARAFIKI ZAKO mmekutana pale kwaajili ya kazi ukitaka kuamini hao siyo marafiki zako mmoja wenu abadili kazi, aachishwe kazi, au ahamishwe eneo, Uone kama ukaribu na mawasiliano yataendelea kuwepo.
Kama unafanya ujenzi au biashara usipeleke marafiki wakazini wakapajue. Tena kwenye biashara wakijua ni biashara yako hawatanunua vitu kwako wataenda kununua kwingine, kwako utaona wanauliza bei wana sepa.
Na usikubali kujenga nyumba mtaa mmoja na wafanyakazi wenzako hiyo ni mbaya kinoma, kama huamini fuatilia uone majungu wanayopigana walio jenga hivyo.
Rafiki yako wa kweli ni yule ulietoka nae utotoni mpaka leo uko nae karibu (japo kuwa nao baadhi wanakuaga wasaliti na wapuuzi) Kama huna huyo achana kabisa kushobokea watu ulio kutana nao wakati umeota ndevu, au maziwa...hao watu watakukaanga vibaya.. huto amini. Jenga urafiki na mtu ambae unaona ana akili nzuri kama ya kwako au kuzidi ya kwako ila asiwe wa kazini kwako.
Chunga sana...Mmbaya wako siku zote hatoki mbali, Mchawi huwa harogi mbali.. Hakikisha unatokomeza masnitch wote usio waelewa katika hatua za mwanzo sana, usiruhusu mtu akujue jue ovyo ovyo, wala asikuzoee ovyo. Utaishi kwa raha sana na mambo yako hawata kuchawia.