Tujiulize, vita ya uchumi tunapigana na nani?

Zero Hours

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2011
Posts
12,942
Reaction score
18,669
Asilimia 80% ya hotuba za Rais John Pombe Magufuli huzungumzia jinsi tulivyo katika vita ya kiuchumi. Lakini mpaka anamaliza awamu yake ya kwanza, hajawai kutueleza hii vita tunapigana na Taifa gani.

Katika maongezi yake, ni kama vile kuna nchi kubwa haitaki Tanzania tuendelee kiuchumi. Hii nchi au Taifa au Mataifa yanafanya mbinu ovu ili tukwame kiuchumi.

Swali ambalo watanzania wengi wanajiuliza na hatupati jibu ni.. Tanzania tunapigana vita ya kiuchumi na nchi gani?

Logically Nchi zinazopigani vita kiuchumi ni lazima ziwe zinalingana/ shabiana kiuchumi. Mfano USA and CHINA. Hawa ukiwaangalia ni kweli wako vitani sababu mmoja anataka awe juu za mwenzie na wanawekeana vikwazo. Hata siku mmoja Tanzania haiwezi ingia vitani na mataifa matajiri. Zimbabwe analijua hili vizuri sana.

Kwa maana iyo, Tanzania haiwezi kuwa vitani na Mataifa makubwa kiuchumi hasa ya bara la Ulaya, America na Asia. Ni upotoshaji kusema au kuassume tupo vitani na nchi inayosuppprt asilimia ya budget yetu. Ni upumbavu kuamini tupo vitani na nchi ambayo haitutegemei wakati sisi tunawategemea. Pia ni ujinga kuamini tupo vitani na nchi ambayo Mapato yake kwa wiki ndyo mapato yetu kwa mwaka.

Labda tuassume Tupo vitani na Majirani zetu ambao tupo nao pamoja kwenye East African community. Hatuwezi pigana na Rwanda wakati ndye rafiki wa nchi yetu mkubwa, hatuwezi pigana na Uganda wakati tulishampiga na hawezi kutuchokoza kabisa. Hatuwezi pigana na Wakenya wakati nao ni marafiki zetu mpaka tugawagawia Tausi. Tena hawa wakenya Tulikamata vifaranga kutoka kwao tukavichoma, wao wakakamata ngombe toka kwetu wakawarudisha.

Sasa swali bado linabaki. Tunapigana vita na Nani? Hii vita ya kiuchumi ni nani anatukwamisha tusiendelee kiuchumi wakati tumeweza tengeneza ajira 6million, tumejenga viwanda zaid ya 4000 ndani ya miaka 4. Hata Kenya haitufikii sasa kwa viwanda.
 
Bila shaka tunapigana vita dhidi ya MABEBERU ya mbuzi wa kule machinjioni Vingunguti. Zaidi ya hapo, basi ujue hizo ni porojo tu kama zile za kwenye vijiwe vya kahawa.
 
Hizi ni nadharia za kijamaa na wengi ni waliosoma syllabus za zamani miaka ya 80 s kushuka chin,baada ya Uhuru walibadili mitaala ya elimu Bora ya kikoloni elimu vitendo,wanatuletea elimu siasa,ambayo ilikuwa ikiwapandikizia wanafunzi chuki za kuwachukia wazungu na mabeberu hasa baada ya watawala kushindwa kuwaletea wananchi maendeleo baada ya kuwaaminisha tukimfukuza mkoloni tutaendelea wote zaidi ya mkoloni.Kumbe mpira walikuwa wakiucheza kwa nje walipoingia ndani wakakuta sivyo walivotegemea.

Nyerere akaleta ujamaa ( itikadi za uvivu sababu ya kila kitu bure).Mfumo sahihi wa uchumi ilitakiwa ni ule wa kikoloni,yaani kuwalazimisha watu kufanya kazi yaani kuwabana na kuwatengenezea mazingira wezeshi ya kufanya kazi.Ukimsoma jemedari wa vita vya pili vya dunia wa uingereza Bernard Montgomery wakati wa vuguvugu la mwanzo la Uhuru Africa ambalo wazo lililetwa na Askari wa kiafrica ambao waliochukuliwa kwenda kupigana nje ya Africa,mwaka 1952 Montgomery amewahi waambia wenzake "hawa waafrika wanataka uhuru wapeni lakini hawatoweza fika mbali watarudi kukutegemeeni tena"zaidi ya miaka 60 maneno yake yanaishi Hadi leo.

Baada ya watawala wa kiafrica kushindwa kuwaletea waafrika tumaini la matunda ya Uhuru ndo wakaja na falsafa za kusingizia hujuma za mabeberu,Mara sijui Vita vya kiuchumi,Mara sijui ukoloni mamboleo,hii inaitwa kutupia lawama wengine juu ya kushindwa kwako.

Sasa kizazi cha sasa ni tofauti mbali na mabadiliko ya syllabus za mashuleni,pia Wana global vision sababu ya mitandao,na uuona ukweli halisi.Kwamba hizi ni propaganda za kushindwa kwa watawala sababu ya sera mbovu.
 
Vita vya kiuchumi,wimbo wa mabeberu, ukoloni mamboleo,sijui IMF,nk hizi ni nadharia za watu walioshindwa kuleta matokeo positive kwenye Jamii.Ina maana Asia, Vietnam,Brazil,Dubai huko Hakuna mabeberu, ukoloni mamboleo,IMF,nk.

Kwann wanashindwa kuleta matokeo positive ni sababu Jamii hatushirikishwi kwenye vipaumbele vyetu,maana vipaumbele vya watawala si vipaumbele vya wananchi.Watawala vipaumbele vyao ni vya kutafuta sifa baada ya kuvimbiwa Kodi zetu,sisi hata Kama tunakufa umasikini sio hoja kwetu.
 
Asilimia 80% ya hotuba za Rais John Pombe Magufuli huzungumzia jinsi tulivyo katika vita ya kiuchumi. Lakini mpaka anamaliza awamu yake ya kwanza, hajawai kutueleza hii vita tunapigana na Taifa gani.

Katika maongezi yake, ni kama vile kuna nchi kubwa haitaki Tanzania tuendelee kiuchumi. Hii nchi au Taifa au Mataifa yanafanya mbinu ovu ili tukwame kiuchumi.

Swali ambalo watanzania wengi wanajiuliza na hatupati jibu ni.. Tanzania tunapigana vita ya kiuchumi na nchi gani?

Logically Nchi zinazopigani vita kiuchumi ni lazima ziwe zinalingana/ shabiana kiuchumi. Mfano USA and CHINA. Hawa ukiwaangalia ni kweli wako vitani sababu mmoja anataka awe juu za mwenzie na wanawekeana vikwazo. Hata siku mmoja Tanzania haiwezi ingia vitani na mataifa matajiri. Zimbabwe analijua hili vizuri sana.

Kwa maana iyo, Tanzania haiwezi kuwa vitani na Mataifa makubwa kiuchumi hasa ya bara la Ulaya, America na Asia. Ni upotoshaji kusema au kuassume tupo vitani na nchi inayosuppprt asilimia ya budget yetu. Ni upumbavu kuamini tupo vitani na nchi ambayo haitutegemei wakati sisi tunawategemea. Pia ni ujinga kuamini tupo vitani na nchi ambayo Mapato yake kwa wiki ndyo mapato yetu kwa mwaka.

Labda tuassume Tupo vitani na Majirani zetu ambao tupo nao pamoja kwenye East African community. Hatuwezi pigana na Rwanda wakati ndye rafiki wa nchi yetu mkubwa, hatuwezi pigana na Uganda wakati tulishampiga na hawezi kutuchokoza kabisa. Hatuwezi pigana na Wakenya wakati nao ni marafiki zetu mpaka tugawagawia Tausi. Tena hawa wakenya Tulikamata vifaranga kutoka kwao tukavichoma, wao wakakamata ngombe toka kwetu wakawarudisha.

Sasa swali bado linabaki. Tunapigana vita na Nani? Hii vita ya kiuchumi ni nani anatukwamisha tusiendelee kiuchumi wakati tumeweza tengeneza ajira 6million, tumejenga viwanda zaid ya 4000 ndani ya miaka 4. Hata Kenya haitufikii sasa kwa viwanda.
Tunapigana na ccm.
 
Asilimia 80% ya hotuba za Rais John Pombe Magufuli huzungumzia jinsi tulivyo katika vita ya kiuchumi. Sasa swali bado linabaki. Tunapigana vita na Nani? Hii vita ya kiuchumi ni nani anatukwamisha tusiendelee kiuchumi wakati tumeweza tengeneza ajira 6million, tumejenga viwanda zaid ya 4000 ndani ya miaka 4. Hata Kenya haitufikii sasa kwa viwanda.
Mkuu hizo ni kauli za Nyerere ambazo kina Magu wamezikariri tu bila kujua.

Vita ya uchumi tunapigana dhidi ya maadui umasikini, ujinga na maradhi. Tatizo kubwa ni kwamba wengi ya wanaoongoza vita hii leo hii ni wajinga! Utakuta hata mikopo toka nje wanaita fedha zetu za ndani, hawajui hata maana ya assets and liabilities na ndio maana wanakopa tu kila siku kwa kuwa mikopo inakuwa fedha zetu kwa muujiza fulani!
 
Hizo ni lugha za enzi za vuguvugu za tawala za kikoloni. Inaonekana tuna rais mwenye hangover ya Zama za ukoloni, ndio maana anatumia misamiati hiyo ya karne iliyopita. Na ukijaribu kumtazma rais wetu ni kama ameamua kuiga falsafa zote za Nyerere, akiamini bado kizazi hiki kinaamini falsafa hizo za Nyerere, kumbe asilimia zaidi ya 60 haijui wala kuamini falsafa za Nyerere. Kwa maneno marahisi tuna rais anayeongoza kwenye karne hii, kwa vionjo vya karne iliyopita.
 
Ni kama vile nchi inarudi nyuma ki IQ
 
Asilimia 80% ya hotuba za Rais John Pombe Magufuli huzungumzia jinsi tulivyo katika vita ya kiuchumi. Lakini mpaka anamaliza awamu yake ya kwanza, hajawai kutueleza hii vita tunapigana na Taifa gani.

Katika maongezi yake, ni kama vile kuna nchi kubwa haitaki Tanzania tuendelee kiuchumi. Hii nchi au Taifa au Mataifa yanafanya mbinu ovu ili tukwame kiuchumi.

Swali ambalo watanzania wengi wanajiuliza na hatupati jibu ni.. Tanzania tunapigana vita ya kiuchumi na nchi gani?

Logically Nchi zinazopigani vita kiuchumi ni lazima ziwe zinalingana/ shabiana kiuchumi. Mfano USA and CHINA. Hawa ukiwaangalia ni kweli wako vitani sababu mmoja anataka awe juu za mwenzie na wanawekeana vikwazo. Hata siku mmoja Tanzania haiwezi ingia vitani na mataifa matajiri. Zimbabwe analijua hili vizuri sana.

Kwa maana iyo, Tanzania haiwezi kuwa vitani na Mataifa makubwa kiuchumi hasa ya bara la Ulaya, America na Asia. Ni upotoshaji kusema au kuassume tupo vitani na nchi inayosuppprt asilimia ya budget yetu. Ni upumbavu kuamini tupo vitani na nchi ambayo haitutegemei wakati sisi tunawategemea. Pia ni ujinga kuamini tupo vitani na nchi ambayo Mapato yake kwa wiki ndyo mapato yetu kwa mwaka.

Labda tuassume Tupo vitani na Majirani zetu ambao tupo nao pamoja kwenye East African community. Hatuwezi pigana na Rwanda wakati ndye rafiki wa nchi yetu mkubwa, hatuwezi pigana na Uganda wakati tulishampiga na hawezi kutuchokoza kabisa. Hatuwezi pigana na Wakenya wakati nao ni marafiki zetu mpaka tugawagawia Tausi. Tena hawa wakenya Tulikamata vifaranga kutoka kwao tukavichoma, wao wakakamata ngombe toka kwetu wakawarudisha.

Sasa swali bado linabaki. Tunapigana vita na Nani? Hii vita ya kiuchumi ni nani anatukwamisha tusiendelee kiuchumi wakati tumeweza tengeneza ajira 6million, tumejenga viwanda zaid ya 4000 ndani ya miaka 4. Hata Kenya haitufikii sasa kwa viwanda.

Vita ya kiuchumi tunapigana na wazungu ambao wanaongozwa na mataifa 10 tajiri duniani ambayo ndio yanapanga bei ya kila kitu kwa kutumia exchange mechanism regime kuwakandamiza waafrika.
 
Uza ubongo huo maana unakaa nao kwa hasara dogo.
 
Vita ya kiuchumi tunapigana na wazungu ambao wanaongozwa na mataifa 10 tajiri duniani ambayo ndio yanapanga bei ya kila kitu kwa kutumia exchange mechanism regime kuwakandamiza waafrika.
Ni sawa unapigana na baba yako ambaye anakulipia school fee, unaishi kwake, na unakula na kunya kwake.
 
Back
Top Bottom