Nashangaa sana kuona watu wazima mmeshupaza shingo kulaumu upuuzi.
Kwamba kama kuna shirika la viwango nchini TBS, kwa nini mkuu wa nchi atoe tahadhari juu ya barakoa ambazo zinaweza kuwa na madhara kwa watumiaji?
Hivi hamjui kuwa pamoja na kuwa na shirika la viwango nchini, bidhaa nyingi feki huwa zinaingia sokoni kupitia njia za panya. Na huwa zinaghundulika baada ya muda, tena mpaka msako ufanyike?
Je, mnadhani hakuna watu wanaoionea husuda Tanzania kiasi cha kuweza kuweka madhara kwenye barakoa zinazoweza kuingizwa nchini kwa njia za panya?
Mmesahau hata USA ilipewa msaada na China na kugundua kuwa barakoa zilikuwa hazina ubora? Mmesahau?
Kuwa na shirika la viwango ndio sababu ya kutopata vifaa visivyo na ubora? Hapana, sababu njia za panya ni nyingi . Hii sio sana
sababu ya kutochukua tahadhari.
Nadhani mmepewa tahadhari ili kuwa na uhakika wa kujilinda ni bora utengeneze cloth mask yako. Maana unaweza ukawa Karagwe, Njombe,Hai na mtu wa nchi jirani akakupa mask toka nje kumbe haina kiwango na ina upupu.
Maoni; Tuache kuwa wakosoaji wa kila kitu, kisa tu tuna chuki za kisiasa. Uchaguzi umepita tuwe na umoja.