Tujuzane aina ya manukato (perfume) unayotumia

Nliwai inunua kali mno😂, nikijpulizia tu mwanangu anapiga chafya hata kama amelala,,

Sijrudia tena,, inasambaa kwa haraka sana,, kali mno
 
Ipi sasa..Bitter peach ama the only one?

Pole
 
Hizi zinaendaje mkuu?

Siuzi mkuu, hii ni collection yangu nayotumia...

Ila ukitaka jua bei zake ni hivi, niliagiza toka SA na Dubai...

120 USD - YSL + Deo Stick (EDP)
1600 ZAR - Dolce & Gabbana The One (EDP)
1700 ZAR - Givenchy Gentleman Boisse ( EDP)
599 ZAR - Zara Tobacco Sublime + ZaraMan Gold + Zara Vibrant Weather & Oud ( Zote EDP)
 
Nikiwa tayari unaweza kunisaidia kunichukulia ya ZAR 600 hadi 800 hivi?
 
Huu mzigo unaitwa Epiq adventure Night upo fresh sana upande wangu, kuna mwengine alishawahi kuutumia? Nani anauza hapa?

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu mimi sio mfanyabiashara...

Hizo niliagiza wadau waliokuwa wamesafiri...
Sawa Mkuu, nilikuelewa wewe siyo mfanyabiashara ila post yangu ilidhamiria kusema kwamba ikitokea unaagiza kwa hao wadau na mimi niunge hapo. Hili limeisha mkuu.
 
Sawa Mkuu, nilikuelewa wewe siyo mfanyabiashara ila post yangu ilidhamiria kusema kwamba ikitokea unaagiza kwa hao wadau na mimi niunge hapo. Hili limeisha mkuu.

Pamoja mkuu, roger that!
 
Sawa Mkuu, nilikuelewa wewe siyo mfanyabiashara ila post yangu ilidhamiria kusema kwamba ikitokea unaagiza kwa hao wadau na mimi niunge hapo. Hili limeisha mkuu.

Preference zako ni zipi?
 
Nikipata Paco Rabane, Invictus au D&G Light Blue itakuwa poa.

Invictus EDP ana matoleo mengi kuna Platinum, Victory na Legend...na Invictus EDT pia ana matoleo mengi Intense, Aqua na nyingine inaitwa tu Invictus, sasa ni ipi labda...vyema ungeambatanisha na picha
 
Emat perfume zake kali, sio uongo.
Yan uwa napulizia nguo, naingia kuoga. Mpaka nitoke imekaa moderate.

Syria perfume baba lao, nimetumia pink sugar yao aisee ni kunukia utamu tu
Pink Sugar naweza kupuliza mimi mwanaume?
 
Invictus EDP ana matoleo mengi kuna Platinum, Victory na Legend...na Invictus EDT pia ana matoleo mengi Intense, Aqua na nyingine inaitwa tu Invictus, sasa ni ipi labda...vyema ungeambatanisha na picha
Nataka nikanunue perfume aina mbili za kupima. Kati ya hizi unashauri nikabebe gani:

  • Bleu de Chanel
  • Creed Aventus
  • Sauvage Dior
  • Lacoste White
  • One Million
  • Hugo sijui nini.
  • Pink Sugar.

(Mimi ni mwanaume)
 
Hizo 3 za juu...

Binafsi ninapenda Bleu de Chanel...

Creed na Sauvage watu wanazitumia sana kiasi kwamba kila mtu atajua umevaa manukato yapi...
 
Nikipata Paco Rabane, Invictus au D&G Light Blue itakuwa poa.

Light Blue 200mil inauzwa ZAR 3710 approx 540,000 TZS , kuna mshikaji anakuja na ndege ya usiku ile, kama unahitaji...

Invictus kakosa...

Ila kwa ushauri, bei za perfume SA ni ghali kidogo kuliko hata TZ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…