Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 1,604
- 3,715
Vyakula wanavyopikiwa wanafunzi na vikundi fulani vyenye mafungamano na walimu wa shule sio salama kabisa! Tunaambiwa watoto kila siku watoe 1000 ya chakula, kwa mfano shule moja Chanika inawanafunzi 1800, wanafunzi 1500 wanakula shule na wengine wanaingia mchana.
Kwa mantiki hiyo kila siku inakusanywa mil 1.5, naambiwa walimu wanakata laki 5, mpishi anapewa mil 1, anaambiwa ajitahidi kila mwanafunzi apate chakula!
Kwa mantiki hiyo, huyu mpishi anapika chakula kisicho na ubora ili na yeye apate faida! Nimeitembelea shule hii mpaka nimeogopa, maharage hayajaiva na hayana viungo.
Yaani wali wanapimiwa kwenye kikombe haitamaniki, umeungulia, hawajali hata afya ya watoto. Natamani kila mtoto ajibebee chakula kutoka kwao.