Hata sijakuelewa. Msingi wa hii mada haijawahi kuihusu FIFA wala Saudi Arabia, imehusu vitendo vya kuonyesha mlengo wa kisiasa kwenye mechi ya mpira ambavyo vimetendwa na mashabiki kadhaa na HASA HASA wachezaji wa Al Ahly ambavyo vina uashiria kuwa vimebarikiwa na CAF maana mpaka sasa hawajavikemea. Nimekuwa clear sana na nia ya mada hii ila tatizo mnataka kuilazimisha iwe mada tofauti na iliyoletwa hadi unataka kuleta story za Saddam.
Mnatolea mifano ya Russia ila mnaacha mifano ya Kenya, Kuwait, Indonesia na Zimbabwe ambao kwa nyakati tofauti walipigwa ban kwa sababu ya serikali zao kuingilia masuala ya michezo. Hata Tanzania tuliwahi kuingia katika matatizo kutokana na wanasiasa kuingilia ishu za michezo. Haya yote lakini hayahusiani na mada UNLESS mnalalamika kwa nini Israel haijawa banned kama Russia na HILO NI NJE YA MADA HII, sijui kipi hakieleweki.
Sababu kubwa ya kuzuia haya mambo viwanjani ni kwa sababu mitazamo ya watu kuhusu siasa haifanani na haiwezi kufanana kamwe. Ushahidi upo katika uzi huu, hata sijasema naisapoti Israel ila tayari kuna watu wako tayari kuninyofoa korodani zangu kisa nimesema mambo ya siasa na dini yasiingizwe kwenye mpira. Ukiachia kila mtu aje viwanjani kuanzia wachezaji hadi mashabiki waseme wanalotaka kuhusu misimamo yao ya kisiasa na kiimani hakutakuwa tena na mpira. Hii ni common sense.