Tukifanya Hivi, Kina Mwamposa na Manabii kuwa Walipa Kodi Wakubwa

Binafsi sioni sababu yakufungia hao wanaojiita mitume na manabii.

Acha wale pesa za wajinga.

Kenge anasikia mpaka masikio yatoe damu.

Watu wataacha kutoa pesa hovyo kwa manabii fake pale tu watakapoachana na akili za kushikiwa.

Tofauti na hapo namshauri Mwamposa aendelee kupiga pesa.
 
Unaweza kulifanyia hesabu kanisa katoliki kila senti ukajua inakwenda wapi na inatumika vipi tofauti na hao kina Mwaposya na wa aina hiyo.

Ipo nidhamu ya uendeshaji wa kanisa katoliki ambayo haipo katika makanisa hayo mengine.
Wakatoliki pesa zinajulikana zinaenda wapi na zinafanya nini!
Matokeo na tunayaona,ila hawa matapeli wakina mwaposa na wengineo pesa zao wanafanyia mambo yao binafsi tu kama kujenga majumba yao kuishi na mahoteli na kununua magari ya kifahari

Ova
 
Wakatoliki pesa zinajulikana zinaenda wapi na zinafanya nini!
Matokeo na tunayaona,ila hawa matapeli wakina mwaposa na wengineo pesa zao wanafanyia mambo yao binafsi tu kama kujenga majumba yao kuishi na mahoteli na kununua magari ya kifahari

Ova
Acha Ujinga wew hizo pesa unazosema unazijua za wakatoliki zinavyo tumika pia kwa wengine wanaona ni utapeli tuu. Jali Imani yako usidhihaki Imani za wengine. Ajidhaniae amesimama na aangalie asije akaanguka.
 

Hujui kitu wewe, hakuna mahali kwenye income tax act wamesamehe biashara zinazoendeshwa makanisani. Soma second schedule. Ni sadaka tu ndizo zimesamehewa kutozwa kodi.
Mauzo ya maji na mafuta is pure business which generates taxable income. Due to its magnitude,VAT, excise duty and income tax should be charged retrospectively.
This is happening in Tanzania because of slumberous TRA.
Katika Hali ya kawaida tunategemea sadaka inunue maji na mafuta na vigawiwe bure; if there is any consideration, then, such consideration is deemed taxable
 
Uko sahihi

Mikungu ya mavuno na vinavyonadiwa siiu za mavuno zinatakiwa kulipiwa kodi kama lengo lao ni kukomalia Mwamposya

Makanisa mengi huuza vitu kwa bei tishio siku za mavuno huvuna mamilioni hizo za Mwamposya nu ndogo

Unakuta mbuzi mmoja siku ya mavuno ananunuliwa miiioni tano

TRA waende huko pia kama ni hivyo
 
Wakatoliki pesa zinajulikana zinaenda wapi na zinafanya nini!
Tueleze huwa pesa za katoliki zinaenda wapi kufanya nini sababu shule zao hata wakatoliki.wa kawaida hawawezi kupeleka watoto huko kusoma

Hospitali zao bei mbaya

Tueleze wewe wakipata hizo pesa huwa wanapeleka wapi kusaidia nani wa kipato kipi cha juu au cha chini?
 
Ukisoma huelewi, biashara yeyote lazma ikidhi tafsiri ya biashara kwa mujibu wa ITA.
Wewe ndiye unayeiita biashara kile kinachofanywa na mwamposa , ila haijakidhi matakwa ya ITA as per business definition.

Sasa biashara za kanisa zozote zinacharjiwa Kodi, mfano mashule, frem za biashara
Ila sio sadaka, michango ya kuchangia huduma kama kwenye jumuiya na mwamposa.
 
Kwa Kanisa Katoliki,je yule ambae hajatoa kabisa atanyimwa komunio? Na kwa Mwamposa yule ambae hajatoa hiyo 5,000 atapewa maji hata kama anayahitaji?
Mkuu kwani ni lazima kila dhehebu lifuate sheria za Wakatoliki?
 

Rudia kusoma ulichokiandika, edit ili ueleweke.
Sijaelewa kitu.
 

Ukisoma na kukaririshwa ITA bila kuelewa au kupata tafsri sahihi, you will end up arguing like you do
 
MWAMPOSA ANAUZA MAJI MENGI SANA ZAIDI YA KIWANDA CHA MAJI LAKINI HALIPI KODI VIVYO HIVYO NA MAFUTA
Mi nawashangaa sn, hivi maji ni yake? Maana ni ya kampuni yyt Ile,na yanauzwa bei ileile ambayo tunanunua kwenye hayo makampuni,ss hapo kauza vipi? Maana anachofanya ni kuchukua kule kuyaombea na watu wanachukua Kwa bei ileile!
Au unaenda na maji yako yanaombewa!
Angekuwa na kiwanda hapo kwelii
 

Kama maji ni ya kampuni nyingine na yanauza bei ile ile hapo ni case nyingine
 
Kenya wametupita mbali sana kielimu. Wana maono kuliko sisi, angalia walivyopasua vichwa mpaka KANU ikaanguka.
 
Wacheni kupotosha ili kumlinda huyo jamaa yenu.

Makanisa hufanya harambee kwa kuuza vitu kwa lengo la kupata pesa zitakazotumika kwa shughuli fulani hapo kanisani, kama ujenzi, ukarabati wa jengo, hakuna harambee inayofanywa bila sababu.

Kwa mantiki hiyo, sasa hebu tuambie, Mwamposa akiuza maji na mafuta, hizo pesa huwa anazipeleka wapi?na kufanyia kitu gani?
 
Rozali,misalaba,mvinyo vinagawiwa bure?
 
Achana na habari za kusikia mkuu,Fanya utafiti upate ukweli maji pale yanauzwa shs 1000 tu,zingine ni stori zisizo na ukweli
 
Naunga mkono hoja
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…