Tukifuata ushauri wa Professor Janabi tutaangamia kwa njaa

Tukifuata ushauri wa Professor Janabi tutaangamia kwa njaa

Wasalaam wakuu!

Kwanza kabisa Nakubaliana na ushauri wote wakitabibu kuhusu aina sahihi ya chakula na namna nzuri ya ulaji kutoka kwa Daktari bingwa na mkuu wa kitengo cha magonjwa ya moyo professor mohamed Yakub Janabi.

Namimi baada yakumsikiliza na kuanza kufuatilia miongozo yake nikaamua kubadili aina yangu ya ulaji ili niendane na matakwa ya msomi huyu. Na sasa ni wiki ya 3 tangu nianze kufuatana na miongozo ya Janabi na nasema wazi kuwa nimenyoosha mikono juu [emoji119], hii ni Baada ya kuzidiwa na njaa kisha kupata kizungu zungu na kuanguka ghafla ofisini.

Baadhi ya miongozo ya Professor huyu msomi

1.Kunywa bia moja masaa yasiyopungua mawili na usiongee wakati unainywa hiyo bia

2.kula mara moja tu, ukizidisha iwe mara mbili na chakula kisizidi ujazo wa kiganja cha mkono wako.

3. ugali ni hatari kwa afya ya moyo na unadumaza akili

4. Professor anasema yeye hajanywa juice ya aina yoyote miaka zaidi ya 15, lakini anasema tusile sukari, chumvi, nyama nyekundu, nyama nyeupe tule kwa kiasi kidogo sana , samaki wasio na magamba wanamafuta mbaya, lakini samaki wa maji chumvi nao ni tatizo kwa moyo. Janabi anaenda mbali nakushauri mboga zote za majani ziliwe zikiwa mbichi. "Kweli kisamvu nikitafune kikiwa kibichi professor?"

Literally ni kama professor Janabi yupo katika kampen ya #kataa chakula sababu anapingana na kila mlo uliozoeleka kwa WaTanzania. Nashauri asipuuzwe ila asitiliwe maanani sana.
Huyu professor wa mchongo na taaluma yake imeleta sintofahamu kitokana na utata wa degree zake za kitabibu! Huyu ni kanjanja!
 
Janabi anapaswa kupata tiba ya afya ya akili.

He is unfit kwa namna anavyotoa maelekezo yake ya kipuuzi kwa umma.

Ushawahi kwenda kuona wanaobeba mizigo masokoni??
Hata akiwa mwembaba anakua amejengeka misuli kwa kubeba vitu vizito.

Mbeba vitu vizito umpe breakfast ya matunda/asile kama Janabi anavyodai, mchana ale kiduchu sijui jioni ale matunda , mzee kesho hata kutembea atashindwa.

Wewe ni daktari??
Mbona mwepesi wakusahau!? Bado tu unaulizia taaluma yangu licha yakujieleza kabla!?
Hebu tuachane na ishu ya msosi maana kuna wapenda kula kukuzidi wewe halikuwa uhakika wakupata hicho chakula hawana.
 
Back
Top Bottom