Ushauri wowote wa jinsi ya kula chakula, jinsi ya kufanya mazoezi, jinsi ya kula dawa, na mambo mengine muhimu yoyote ya kiafya ya jamii, hautakiwi kutolewa kiujumla.
Ndiyo maana wenzetu baada ya kutoa ushauri, husisitiza sana suala la kwamba kila mtu yuko tofauti, usiufanyie kazi ushauri kabla ya kuongea na daktari wako.
Kila mtu ana tofauti, na hivyo, anaweza kuhitaji mbinu tofauti.
Mfano, mtu mwenye uzito uliozidi, anayefanya kazi ofisini, anayekaa sana kwenye kiti, mwenye gari, ambaye hana mizunguko mingi kwa siku, anaweza kuangaliwa na daktari wake akaambiwa aongeze mazoezi na kupunguza caloric intake na ushauri huu ukamsaidia.
Lakini, mtu ambaye yuko underweight, analima kwa kutumia nguvu kubwa sana siku nzima, ana mizunguko mingi, kazi yake tu ni sawa na mazoezi, inahitaji nishati kubwa sana, na yeye utamwambia apunguze kula na aongeze mazoezi? Hai make sense.
Dr. Janabi anapotoa ushauri, huwa anasisitiza watu waongee na madaktari wao kwanza kabla ya kupanga jinsi ya kula au kufanya mazoezi?