Tukio gani baya ulilowahi kukutana nalo usiku?

Tukio gani baya ulilowahi kukutana nalo usiku?

giphy.gif
umeshawahi kukutana na mguu mmoja unakimbia gizani?
Tunatishana Mkuu
 

Usiku kuna mengi
 
Tukio hili hapa

Nimelala usingizi ila ndani ya usingizi najiona nipo macho kabisa yaani nimelala ila mwili wangu upo active, najiona natembea naenda kila sehemu naongea na watu nacheka nafurahi (nafurahi kweli nacheka ila nmelala) ila kuna jambo ndani ya usingizi linatokea ghafla naona kuna mtu ananifuata kwa nia ovu nakimbia kutoka nje naingia ndani mpaka chumbani kwangu ambako niliuacha mwili wangu ukiwa umelala,

Nimeingia chumbani chumba kikawa kina giza Totoro sasa nikiwa nashangaa huyu nani alielala (kumbe ni mimi nikawa nahisi ni mtu mwingine) mara ghafla yule alikua ananikimbiza nje akawa ametokea ndani, amepitia wapi mimi sijui, nikaanza kumfukuza "toooooka" "tooooooka" akawa anakuja upande wangu ananisogelea zaidi nikawa namwambia kwa sauti zaiiiidi "tooooooka", kumbe huku nimelala ni mimi naongea nikawa nimejigeuza niinuke nimfuate, nageuka kwa nguvu niende nikamsambalatishe vuuuupu najiona ni mimi ndie ambae nilikua nimelala, kumwangalia yule mtu simuoni kuangalia saa ndio kwanza saa 5 usiku

Sikulala tena hadi Swaaaalah Swaaaaalah

Niishie hapa..
Jinamizi ilo
 
Mapatna wetu Iyunga boys. Sema sasa ss haikuwa perfect combo kwa sbb Iyunga enzo tunasoma wao walikua o level pekee. Ss form five na six enzi hzo. Vipi wameshaanzisha A level I hope so.
Yah Mkuu A level ipo na mimi nimepiga hapo Advance mkuu...Hakika Mlikua ma partner wetu..hata sisi tulikua hatusikii kitu kuhusu Loreza aisee...Tunawapenda Toka moyoni hahahaha
 
Habarini wakuu,
Jana night katika safari zangu za hapa na pale kwenye daladala nipo zangu na deep feeling za kusikiliza music kwa earphones siti ya dirishani macho yakiwa nje kutazama tunavyoikata miti na mito mbalimbali, it was perfect kwangu maana me hupenda kusafiri sana, Huwa safari za usiku zinanisisimua sana hasa ile unakuta mnalikata pori alafu mfano unamuona mtu yupo peke yake maybe ukizingatia giza ni nene na pia mazingira yanatisha ila unakuta huyo mtu maybe haoneshi hofu au pengine ana hofu ila ndo hivyo yupo kwenye mapito yake ya kimaisha pia, Hilo jambo likanifanya niutafakari usiku na matukio yake mabaya niliyowahi kukutana nayo....

Tukio la kwanza, Mimi nililelewa na baba pekee baba alikuwa akinionya sana kuhusu usiku, Alikuwa akinisihi sana niepukane na mizunguko ya usiku kwani ni hatari sana, Mwanzoni nilikuwa simuelewi hadi pale nilipofikia umri wa kubalehe kwenye yale mahusiano ya girlfriend na girlfriend katika zile appointments za hapa na pale siku moja tukapanga tukutane night fulani hivi na mtoto mzuri, Though nilijua nikirudi home itakuwa msala kwa mzee ila sikujali hilo sana maana niliona cha muhimu niende na nirudi salama nikajitusu...
Ile siku niliponea kuuwawa na vibaka kama sio kujeruhiwa na girlfriend wangu alibakwa, so sad ila tulisolve mambo yakakaa sawa kuanzia pale nikagundua usiku ni hatari sana.

Tukio la pili, Hili sio la muda sana
Nilikuwa natoka kazini kuelekea nyumbani, hapakuwa na umbali sana so nikawa natembea kwa mguu barabara ya mandela road kupitia service road nilikuwa nikiongozana na mdada mmoja ambae sikumfahamu ila tulikuwa uelekeo sawa yeye yupo mbele mimi nyuma ghafla wakatokea Majamaa wawili wamepakizana kwenye bike (bodaboda) wakanipita mimi na kumuingilia yule dada kwa mbele wakamblock katika kutahamaki lile tukio maana walifunga breki ya ghafla nilisikia tu wakimuambia yule dada "Tunaomba hilo begi" (dada alikuwa ana begi, Yule dada akaanza kama kuwabwatukia hivi jamaa mmoja kashuka akamsogelea kisha akachomoa pistol akamfyatua mbili za kichwa na kuchukua begi akadandia bike wakasepa, Wakati huo mimi nimebaki kama nimeduwaa tu nisijue nini cha kufanya na hofu ikiwa imenijaa, baada ya sec kadhaa tu watu wakawa wamezingira mwili wa dada yule pale chini, Police wakaja tukaojiwa na kutoa maelezo ya tukio, vipimo vikafanyika mwili wa dada wa watu ukachukuliwa kwenda kuhifadhiwa, Kwa tetesi nilizosikia pale ni kwamba mdada yule alikuwa wakala so, pale alikuwa katoka kafunga hesabu na kwenye begi mule ndo kulikuwa na pesa za hesabu so walimtime, Me binafsi iliniuma sana kuona watu wanamtoa mtu uhai kwaajili ya jasho lake na hiyo ikanifanya nizidi kuamini usiku sio muda mzuri.

Je, wewe ni tukio gani baya ulilowahi kukutana nalo usiku?
So sad
 
Miaka ya nyuma (90's), tekinonojia ikiwa bado chini, mabasi yalikuwa yanasafiri hata siku mbili kwenda mikoani. Mabasi hayo yalikuwa yanasafiri usiku na mchana. Sasa safari moja nikiwa naenda mkoa fulani, safari ikiendelea usiku wa manane, tukiwa katika pori kubwa, giza totoro, mtu mmoja akamwomba konda kuwa anataka kushuka. Konda akamwuliza unataka kujisaidia, akajibu, nashukia hapa, nimefika. Watu wa mle ndani ya basi tulishangaa sana! Maana ni msitu mnene hauna dalili ya kukaa mtu. Basi konda akamsihi dereva asimame, na mtu huyo alishuka. Sasa watu mle kwenye basi wakaanza kuulizana, hapa mbona hawakai watu, huyu anaenda wapi. Watu wengine wakasema, usiku huu, tuyaache kama yalivyo. Hapo mahali aliposhukia hata ukipita leo hii mchana kweupe, hakuna dalili ya watu, maana ni msitu mzito sana. Sasa yule jamaa usiku ule alienda wapi na alikuwa peke yake! Kila nikipita maeneo yale huwa najiuliza maswali mengi sana!
 
Aisee usiku sio poa

Siku moja si nipo mitaa za zenj hivy kama saa 5 namsindikiza demu home kwao baada ya kumsindikiza mi narudi fresh sina hili wala lile

Ebwanaa we si kumbe ubaya ubaya walinilia teming nashtuka tayar nimwzungukwa mbele na nyuma nikajua hapa leo kazi

Sehem ilikua kuna ka kigiza hivi nikachomoa pochi nikadondosha chini nataka kuchomoa na smu nakuta jamaa kalita kisu mkononi kikanijeruhi kidgo

Basi wakachkja smu wakatoka nduki

Siku ya pili tukaanza msako si tuje kumshika mmoja aisee nilipasua pumbu zote sasa sjui kua aliishi au alikufa.
 
Miaka ya nyuma (90's), tekinonojia ikiwa bado chini, mabasi yalikuwa yanasafiri hata siku mbili kwenda mikoani. Mabasi hayo yalikuwa yanasafiri usiku na mchana. Sasa safari moja nikiwa naenda mkoa fulani, safari ikiendelea usiku wa manane, tukiwa katika pori kubwa, giza totoro, mtu mmoja akamwomba konda kuwa anataka kushuka. Konda akamwuliza unataka kujisaidia, akajibu, nashukia hapa, nimefika. Watu wa mle ndani ya basi tulishangaa sana! Maana ni msitu mnene hauna dalili ya kukaa mtu. Basi konda akamsihi dereva asimame, na mtu huyo alishuka. Sasa watu mle kwenye basi wakaanza kuulizana, hapa mbona hawakai watu, huyu anaenda wapi. Watu wengine wakasema, usiku huu, tuyaache kama yalivyo. Hapo mahali aliposhukia hata ukipita leo hii mchana kweupe, hakuna dalili ya watu, maana ni msitu mzito sana. Sasa yule jamaa usiku ule alienda wapi na alikuwa peke yake! Kila nikipita maeneo yale huwa najiuliza maswali mengi sana!
Atakua anaenda kwa mganga wake, ishu kama hiyo ilitokea siku nimepanda lori, uzuri tulikua na abiria mwingine akasema hapa anapatikana mganga matata wa masuala ya uchumi.
 
Nilishuhudia mbwa wangu akifa tena niliua mwenyewe pasipo kujua.....Home tulikuwa tunafuga chairfire muda ukifika wa ada tunauza tunalipa....nimesoma kwa njia hiyo....sasa sikuhiyo chairfire alitoka bandani so nikawa nafukuzia ile night ili aingie bandani mdomoni nimebana simu ya mama nipate mwanga....mkono mmoja nimeshika nyundo na msumari wa kureplace pale alipotokea chairfire.....nikaona ananizungusha tu haingii bandani,si nikainua nyundo nimwotee makalio ....daaa si mbwa wangu akawa kajitokeza alikula nyundo ya kichwa...akazimia akajazinduka bembeleza samaki ale wapii....nikaamua nikalale kuamka asubuhi kamanda kafa.... [emoji24] [emoji24][emoji24]nalia mpaka Leo jamani ....I killed it mweee.....yaan daaa.
Bahati mbaya kama hizo hutokea.!

Kuna siku mzee anarudisha gari nyuma kumbe paka wetu mzur alilala chini ya tair.!

Nililia kushuhudia anavyo jaribu kuinusur roho yake.
 
Bahati mbaya kama hizo hutokea.!

Kuna siku mzee anarudisha gari nyuma kumbe paka wetu mzur alilala chini ya tair.!

Nililia kushuhudia anavyo jaribu kuinusur roho yake.
Inaumiza sana kuona mnyama asiye na jeuri yoyote anaangamia
 
Back
Top Bottom