Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hayo matukio hata jioni jioni tuHabarini wakuu,
Jana night katika safari zangu za hapa na pale kwenye daladala nipo zangu na deep feeling za kusikiliza music kwa earphones siti ya dirishani macho yakiwa nje kutazama tunavyoikata miti na mito mbalimbali, it was perfect kwangu maana me hupenda kusafiri sana, Huwa safari za usiku zinanisisimua sana hasa ile unakuta mnalikata pori alafu mfano unamuona mtu yupo peke yake maybe ukizingatia giza ni nene na pia mazingira yanatisha ila unakuta huyo mtu maybe haoneshi hofu au pengine ana hofu ila ndo hivyo yupo kwenye mapito yake ya kimaisha pia, Hilo jambo likanifanya niutafakari usiku na matukio yake mabaya niliyowahi kukutana nayo....
Tukio la kwanza, Mimi nililelewa na baba pekee baba alikuwa akinionya sana kuhusu usiku, Alikuwa akinisihi sana niepukane na mizunguko ya usiku kwani ni hatari sana, Mwanzoni nilikuwa simuelewi hadi pale nilipofikia umri wa kubalehe kwenye yale mahusiano ya girlfriend na girlfriend katika zile appointments za hapa na pale siku moja tukapanga tukutane night fulani hivi na mtoto mzuri, Though nilijua nikirudi home itakuwa msala kwa mzee ila sikujali hilo sana maana niliona cha muhimu niende na nirudi salama nikajitusu...
Ile siku niliponea kuuwawa na vibaka kama sio kujeruhiwa na girlfriend wangu alibakwa, so sad ila tulisolve mambo yakakaa sawa kuanzia pale nikagundua usiku ni hatari sana.
Tukio la pili, Hili sio la muda sana
Nilikuwa natoka kazini kuelekea nyumbani, hapakuwa na umbali sana so nikawa natembea kwa mguu barabara ya mandela road kupitia service road nilikuwa nikiongozana na mdada mmoja ambae sikumfahamu ila tulikuwa uelekeo sawa yeye yupo mbele mimi nyuma ghafla wakatokea Majamaa wawili wamepakizana kwenye bike (bodaboda) wakanipita mimi na kumuingilia yule dada kwa mbele wakamblock katika kutahamaki lile tukio maana walifunga breki ya ghafla nilisikia tu wakimuambia yule dada "Tunaomba hilo begi" (dada alikuwa ana begi, Yule dada akaanza kama kuwabwatukia hivi jamaa mmoja kashuka akamsogelea kisha akachomoa pistol akamfyatua mbili za kichwa na kuchukua begi akadandia bike wakasepa, Wakati huo mimi nimebaki kama nimeduwaa tu nisijue nini cha kufanya na hofu ikiwa imenijaa, baada ya sec kadhaa tu watu wakawa wamezingira mwili wa dada yule pale chini, Police wakaja tukaojiwa na kutoa maelezo ya tukio, vipimo vikafanyika mwili wa dada wa watu ukachukuliwa kwenda kuhifadhiwa, Kwa tetesi nilizosikia pale ni kwamba mdada yule alikuwa wakala so, pale alikuwa katoka kafunga hesabu na kwenye begi mule ndo kulikuwa na pesa za hesabu so walimtime, Me binafsi iliniuma sana kuona watu wanamtoa mtu uhai kwaajili ya jasho lake na hiyo ikanifanya nizidi kuamini usiku sio muda mzuri.
Je, wewe ni tukio gani baya ulilowahi kukutana nalo usiku?
bahati yako una akili😁Mim kutembea usiku siwez hata niwe na baunsa siwez.
Juzi tu hapa nmelala nasikia watu kama mia wanakatiza usawa wa dirisha la chumbani kwangu.
Nkaamka chap nikazima taa zote za ndani nkabakisha za nje alf nkajifanya naongea na simu eeh wamekuja sogeeni getini muwapakie wote kweny karandinga nilisikia watu wana kimbia hapo nje muda huo mtoto angu nishamuamishia uvunguni.
Asubui nakutana na wasenge wananitolea mimacho mchana nkawaita washkaji zangu wawili mapongo nkawaambiwa waje na wenzao wafike hata watano wakaja na defender na mitutu.
Kutoka getini tena wale waloanzisha kijiwe sion mtu hata mmja jion kutoka nje nasikia sister habari nkasema fresh ety mbona tumeona defender hapo getini kuna nn nkawaambiwa hao wafanyakazi wenzangu wamekuja kunipa pole nilipata msiba eeh watu wote kimya. Wangejua mim ni dada machinga sijui tu
Tina alifanikiwa kukimbia umbali huo kweli?Yap tulikua tumetoka kwenye bash(UNIVRSTY BASH) vibaka walivamia shoo halafu waandaaji DREAM FM Wakaingia mitini...aisee hebu vuta picha MAMA JOHN,CCM,ILOMBA,SAE,NANENANE,JESHINI,KILIMO ndio ufike UYOLE...Njia nzima ni kukimbizwa MWENDO MCHIBUYU halafu nilikua na demu wangu TINA....2014
Hakuna wa piliwe mzee bana[emoji16][emoji16] mguu mmoja unakimbia vipi sasa
Yani pona pona yangu.Mim muoga mnobahati yako una akili😁
Goodthing ni kwamba TINA alikua kwenye athlete board ya uni(mwanariadha),hatumii kilevi halafu anaumbo dogo,mpare wa milimani halafu ni chembambaTina alifanikiwa kukimbia umbali huo kweli?
pole, kabla ya kulala usaliTukio hili hapa
Nimelala usingizi ila ndani ya usingizi najiona nipo macho kabisa yaani nimelala ila mwili wangu upo active, najiona natembea naenda kila sehemu naongea na watu nacheka nafurahi (nafurahi kweli nacheka ila nmelala) ila kuna jambo ndani ya usingizi linatokea ghafla naona kuna mtu ananifuata kwa nia ovu nakimbia kutoka nje naingia ndani mpaka chumbani kwangu ambako niliuacha mwili wangu ukiwa umelala,
Nimeingia chumbani chumba kikawa kina giza Totoro sasa nikiwa nashangaa huyu nani alielala (kumbe ni mimi nikawa nahisi ni mtu mwingine) mara ghafla yule alikua ananikimbiza nje akawa ametokea ndani, amepitia wapi mimi sijui, nikaanza kumfukuza "toooooka" "tooooooka" akawa anakuja upande wangu ananisogelea zaidi nikawa namwambia kwa sauti zaiiiidi "tooooooka", kumbe huku nimelala ni mimi naongea nikawa nimejigeuza niinuke nimfuate, nageuka kwa nguvu niende nikamsambalatishe vuuuupu najiona ni mimi ndie ambae nilikua nimelala, kumwangalia yule mtu simuoni kuangalia saa ndio kwanza saa 5 usiku
Sikulala tena hadi Swaaaalah Swaaaaalah
Niishie hapa..
Ila Arusha ina mbwa jamani 🤣🤣🤣Sema mimi sijui kwanini gari lipo ila sitaki kuendesha,boda boda masela wengi nawajua ila sitaki lifiti,mda mwingine napenda kutembea kwa miguu,tena usiku wa kiza kinene kwa mtu anayejua arusha usiku panakuaje bonge la giza ni makelele ya umbwa kama wote
Haya ntakua nakuita usijali.usiwe unalala peke yako niite ata mimi nipo tu kwa hapa pembeni nimekaa
Always kabla ya kuangusha mwili wangu iwe usiku iwe mchana hua napiga goti chini napiga dua zangu za kutosha, natoa shukurani km zote kwa Creator & our Maker, sijawahi lala bila kusali aisee hata siku mojapole, kabla ya kulala usali
sasa mbona ukawa unasema toka badala ya kukemea kwa kutumia jina la Mungu wako?Always kabla ya kuangusha mwili wangu iwe usiku iwe mchana hua napiga goti chini napiga dua zangu za kutosha, natoa shukurani km zote kwa Creator & our Maker, sijawahi lala bila kusali aisee hata siku moja