Tukio gani baya ulilowahi kukutana nalo usiku?

Tukio gani baya ulilowahi kukutana nalo usiku?

𝕊𝕒𝕒 4 𝕙𝕚𝕧𝕚 𝕦𝕤𝕚𝕜𝕦 𝕟𝕒 𝕜𝕚𝕓𝕖𝕘 𝕔𝕙𝕒𝕟𝕘𝕦 𝕜𝕚𝕟𝕒 𝕃𝕒𝕡𝕥𝕠𝕡 𝕞𝕡𝕪𝕒 𝕡𝕒𝕝𝕖 𝕜𝕒𝕣𝕚𝕓𝕦 𝕟𝕒 𝔹𝕚𝕘 𝔹𝕠𝕟, 𝕟𝕒𝕥𝕒𝕗𝕦𝕥𝕒 𝕘𝕒𝕣𝕚 𝕝𝕒 𝕌𝕓𝕦𝕟𝕘𝕠, 𝕜𝕒𝕥𝕠𝕜𝕖𝕒 𝕛𝕒𝕞𝕒𝕒 𝕞𝕞𝕠𝕛𝕒 𝕒𝕜𝕒𝕤𝕖𝕞𝕒 𝕟𝕚𝕞𝕖𝕞𝕜𝕒𝕟𝕪𝕒𝕘𝕒, 𝕟𝕚𝕜𝕒𝕞𝕨𝕒𝕞𝕓𝕚𝕒 𝕤𝕒𝕞𝕒𝕙𝕒𝕟𝕚 𝕒𝕜𝕒𝕖𝕟𝕕𝕖𝕝𝕖𝕒 𝕜𝕦𝕟𝕚𝕠𝕟𝕖𝕤𝕙𝕒 𝕕𝕠𝕟𝕕𝕒 𝕝𝕚𝕟𝕒𝕥𝕠𝕒 𝕕𝕒𝕞𝕦 𝕞𝕘𝕦𝕦𝕟𝕚. Nikahisi vby moyoni...Mara naona kundi linaongezeka wakinisihi niwajibike...Kichwani taa ikawaka nikajua hapa naibiwa maana wengine wapo nyuma yangu. Aisee nikakumbuka hapo zamani nilikimbiaga Dojo la Masta Rama, ila viskills bado vimo vimo, nikachagua mmoja wa sampuli (hapo akili inafanya kazi haraka balaa) Nilimfyatua teke moja kali la kichwa yule aliyedai nimemkanyaga, wakati anaweweseka nilitandiga buti lingine mguuni aka mtama, likampata pale pale penye kidonda. Jamaa akaanguka chini huku anapiga kelele. Wale wenzake nikashangaa wanachochola mbaya....Nami nikatembea fasta nikadandia Daladala bila hata kusoma linaelekea wapi....Baada ya kukaa kwenye siti ndo Moyo ukaanza kudunda balaa na woga mkali ukaniingia!!
 
Habarini wakuu,
Jana night katika safari zangu za hapa na pale kwenye daladala nipo zangu na deep feeling za kusikiliza music kwa earphones siti ya dirishani macho yakiwa nje kutazama tunavyoikata miti na mito mbalimbali, it was perfect kwangu maana me hupenda kusafiri sana, Huwa safari za usiku zinanisisimua sana hasa ile unakuta mnalikata pori alafu mfano unamuona mtu yupo peke yake maybe ukizingatia giza ni nene na pia mazingira yanatisha ila unakuta huyo mtu maybe haoneshi hofu au pengine ana hofu ila ndo hivyo yupo kwenye mapito yake ya kimaisha pia, Hilo jambo likanifanya niutafakari usiku na matukio yake mabaya niliyowahi kukutana nayo....

Tukio la kwanza, Mimi nililelewa na baba pekee baba alikuwa akinionya sana kuhusu usiku, Alikuwa akinisihi sana niepukane na mizunguko ya usiku kwani ni hatari sana, Mwanzoni nilikuwa simuelewi hadi pale nilipofikia umri wa kubalehe kwenye yale mahusiano ya girlfriend na girlfriend katika zile appointments za hapa na pale siku moja tukapanga tukutane night fulani hivi na mtoto mzuri, Though nilijua nikirudi home itakuwa msala kwa mzee ila sikujali hilo sana maana niliona cha muhimu niende na nirudi salama nikajitusu...
Ile siku niliponea kuuwawa na vibaka kama sio kujeruhiwa na girlfriend wangu alibakwa, so sad ila tulisolve mambo yakakaa sawa kuanzia pale nikagundua usiku ni hatari sana.

Tukio la pili, Hili sio la muda sana
Nilikuwa natoka kazini kuelekea nyumbani, hapakuwa na umbali sana so nikawa natembea kwa mguu barabara ya mandela road kupitia service road nilikuwa nikiongozana na mdada mmoja ambae sikumfahamu ila tulikuwa uelekeo sawa yeye yupo mbele mimi nyuma ghafla wakatokea Majamaa wawili wamepakizana kwenye bike (bodaboda) wakanipita mimi na kumuingilia yule dada kwa mbele wakamblock katika kutahamaki lile tukio maana walifunga breki ya ghafla nilisikia tu wakimuambia yule dada "Tunaomba hilo begi" (dada alikuwa ana begi, Yule dada akaanza kama kuwabwatukia hivi jamaa mmoja kashuka akamsogelea kisha akachomoa pistol akamfyatua mbili za kichwa na kuchukua begi akadandia bike wakasepa, Wakati huo mimi nimebaki kama nimeduwaa tu nisijue nini cha kufanya na hofu ikiwa imenijaa, baada ya sec kadhaa tu watu wakawa wamezingira mwili wa dada yule pale chini, Police wakaja tukaojiwa na kutoa maelezo ya tukio, vipimo vikafanyika mwili wa dada wa watu ukachukuliwa kwenda kuhifadhiwa, Kwa tetesi nilizosikia pale ni kwamba mdada yule alikuwa wakala so, pale alikuwa katoka kafunga hesabu na kwenye begi mule ndo kulikuwa na pesa za hesabu so walimtime, Me binafsi iliniuma sana kuona watu wanamtoa mtu uhai kwaajili ya jasho lake na hiyo ikanifanya nizidi kuamini usiku sio muda mzuri.

Je, wewe ni tukio gani baya ulilowahi kukutana nalo usiku?
giphy.gif
umeshawahi kukutana na mguu mmoja unakimbia gizani?
 
Jamaangu mmja boda boda alikuwa kila siku anachelewa kurudi home gheto alikopanga zake ni saa nane usiku

So akawa anaruka ukuta anafungua geti anaingiza boda

wapangaji wenzake wakamchoka
wakatega mavi ukutani , mwamba ile kuruka tu tshirt nzima ilitapakaa mavi

Aliama kesho yake
 
Mim kutembea usiku siwez hata niwe na baunsa siwez.

Juzi tu hapa nmelala nasikia watu kama mia wanakatiza usawa wa dirisha la chumbani kwangu.

Nkaamka chap nikazima taa zote za ndani nkabakisha za nje alf nkajifanya naongea na simu eeh wamekuja sogeeni getini muwapakie wote kweny karandinga nilisikia watu wana kimbia hapo nje muda huo mtoto angu nishamuamishia uvunguni.

Asubui nakutana na wasenge wananitolea mimacho mchana nkawaita washkaji zangu wawili mapongo nkawaambiwa waje na wenzao wafike hata watano wakaja na defender na mitutu.

Kutoka getini tena wale waloanzisha kijiwe sion mtu hata mmja jion kutoka nje nasikia sister habari nkasema fresh ety mbona tumeona defender hapo getini kuna nn nkawaambiwa hao wafanyakazi wenzangu wamekuja kunipa pole nilipata msiba eeh watu wote kimya. Wangejua mim ni dada machinga sijui tu
 
Yap tulikua tumetoka kwenye bash(UNIVRSTY BASH) vibaka walivamia shoo halafu waandaaji DREAM FM Wakaingia mitini...aisee hebu vuta picha MAMA JOHN,CCM,ILOMBA,SAE,NANENANE,JESHINI,KILIMO ndio ufike UYOLE...Njia nzima ni kukimbizwa MWENDO MCHIBUYU halafu nilikua na demu wangu TINA....2014
 
𝕊𝕒𝕒 4 𝕙𝕚𝕧𝕚 𝕦𝕤𝕚𝕜𝕦 𝕟𝕒 𝕜𝕚𝕓𝕖𝕘 𝕔𝕙𝕒𝕟𝕘𝕦 𝕜𝕚𝕟𝕒 𝕃𝕒𝕡𝕥𝕠𝕡 𝕞𝕡𝕪𝕒 𝕡𝕒𝕝𝕖 𝕜𝕒𝕣𝕚𝕓𝕦 𝕟𝕒 𝔹𝕚𝕘 𝔹𝕠𝕟, 𝕟𝕒𝕥𝕒𝕗𝕦𝕥𝕒 𝕘𝕒𝕣𝕚 𝕝𝕒 𝕌𝕓𝕦𝕟𝕘𝕠, 𝕜𝕒𝕥𝕠𝕜𝕖𝕒 𝕛𝕒𝕞𝕒𝕒 𝕞𝕞𝕠𝕛𝕒 𝕒𝕜𝕒𝕤𝕖𝕞𝕒 𝕟𝕚𝕞𝕖𝕞𝕜𝕒𝕟𝕪𝕒𝕘𝕒, 𝕟𝕚𝕜𝕒𝕞𝕨𝕒𝕞𝕓𝕚𝕒 𝕤𝕒𝕞𝕒𝕙𝕒𝕟𝕚 𝕒𝕜𝕒𝕖𝕟𝕕𝕖𝕝𝕖𝕒 𝕜𝕦𝕟𝕚𝕠𝕟𝕖𝕤𝕙𝕒 𝕕𝕠𝕟𝕕𝕒 𝕝𝕚𝕟𝕒𝕥𝕠𝕒 𝕕𝕒𝕞𝕦 𝕞𝕘𝕦𝕦𝕟𝕚. Nikahisi vby moyoni...Mara naona kundi linaongezeka wakinisihi niwajibike...Kichwani taa ikawaka nikajua hapa naibiwa maana wengine wapo nyuma yangu. Aisee nikakumbuka hapo zamani nilikimbiaga Dojo la Masta Rama, ila viskills bado vimo vimo, nikachagua mmoja wa sampuli (hapo akili inafanya kazi haraka balaa) Nilimfyatua teke moja kali la kichwa yule aliyedai nimemkanyaga, wakati anaweweseka nilitandiga buti lingine mguuni aka mtama, likampata pale pale penye kidonda. Jamaa akaanguka chini huku anapiga kelele. Wale wenzake nikashangaa wanachochola mbaya....Nami nikatembea fasta nikadandia Daladala bila hata kusoma linaelekea wapi....Baada ya kukaa kwenye siti ndo Moyo ukaanza kudunda balaa na woga mkali ukaniingia!!
Ulikuwa mandonga siku hiyo.
 
Napamanya pote hyo mitaa,ndo maana nimeshangaa mi ni zao la Loleza girls ya Enzi zilee. So mitaa hyo naijua. Halafu hapo ni mbali mnoo duuu poleni
 
Nikiwa na misele ya night lazima nitembee na kisu Cha kukunja.

Usitembee mkavu lazima uwe na ka silaha kadogo au tafuta pepper spray.

Usiku haufai

Na usitembee tu randomly bila kuwa na uelewekeo.

Mimi ukiniona natembea usiku basi Jua nafuata Kat somewhere otherswise huwa nachili home.
amini✊
 
Mwaka juzi nilikua natoka masasi narud dar ilikua kama saa 9 usiku ivi niliona wanaume wawili wanakimbia mdogo mdogo na maeneo hayo kuna poli hakuna kijiji karibu adi Leo sielew ilikuaje
dah, binadamu tuna safari sana
 
jamaa mmoja kashuka akamsogelea kisha akachomoa pistol akamfyatua mbili za kichwa na kuchukua begi akadandia bike wakasepa. Binadamu tumekuwa wakatili kuliko hata Wanyama Mungu tusaidie.
acha tu mzee
 
𝕊𝕒𝕒 4 𝕙𝕚𝕧𝕚 𝕦𝕤𝕚𝕜𝕦 𝕟𝕒 𝕜𝕚𝕓𝕖𝕘 𝕔𝕙𝕒𝕟𝕘𝕦 𝕜𝕚𝕟𝕒 𝕃𝕒𝕡𝕥𝕠𝕡 𝕞𝕡𝕪𝕒 𝕡𝕒𝕝𝕖 𝕜𝕒𝕣𝕚𝕓𝕦 𝕟𝕒 𝔹𝕚𝕘 𝔹𝕠𝕟, 𝕟𝕒𝕥𝕒𝕗𝕦𝕥𝕒 𝕘𝕒𝕣𝕚 𝕝𝕒 𝕌𝕓𝕦𝕟𝕘𝕠, 𝕜𝕒𝕥𝕠𝕜𝕖𝕒 𝕛𝕒𝕞𝕒𝕒 𝕞𝕞𝕠𝕛𝕒 𝕒𝕜𝕒𝕤𝕖𝕞𝕒 𝕟𝕚𝕞𝕖𝕞𝕜𝕒𝕟𝕪𝕒𝕘𝕒, 𝕟𝕚𝕜𝕒𝕞𝕨𝕒𝕞𝕓𝕚𝕒 𝕤𝕒𝕞𝕒𝕙𝕒𝕟𝕚 𝕒𝕜𝕒𝕖𝕟𝕕𝕖𝕝𝕖𝕒 𝕜𝕦𝕟𝕚𝕠𝕟𝕖𝕤𝕙𝕒 𝕕𝕠𝕟𝕕𝕒 𝕝𝕚𝕟𝕒𝕥𝕠𝕒 𝕕𝕒𝕞𝕦 𝕞𝕘𝕦𝕦𝕟𝕚. Nikahisi vby moyoni...Mara naona kundi linaongezeka wakinisihi niwajibike...Kichwani taa ikawaka nikajua hapa naibiwa maana wengine wapo nyuma yangu. Aisee nikakumbuka hapo zamani nilikimbiaga Dojo la Masta Rama, ila viskills bado vimo vimo, nikachagua mmoja wa sampuli (hapo akili inafanya kazi haraka balaa) Nilimfyatua teke moja kali la kichwa yule aliyedai nimemkanyaga, wakati anaweweseka nilitandiga buti lingine mguuni aka mtama, likampata pale pale penye kidonda. Jamaa akaanguka chini huku anapiga kelele. Wale wenzake nikashangaa wanachochola mbaya....Nami nikatembea fasta nikadandia Daladala bila hata kusoma linaelekea wapi....Baada ya kukaa kwenye siti ndo Moyo ukaanza kudunda balaa na woga mkali ukaniingia!!
appreciate masta, hiyo ndo ilikuwa bahati yako
 
Back
Top Bottom