Tukio gani kwenye soka huwezi kulisahau?

Yeah dogo yupo pale Liverpool u21
 
Mambo Gani hayo ya kukumbushana machungu
Kama kumbukumbu zangu hazijapotea...

Alianza balloteli x2,
Beki wenu jonny evans alikula umeme,
Akaja aguero x2,akafuata DZEKO,akamaliza silva..

halafu refa alikua mark clattenburg,mlikua old trafford..
babu fergie na msaidizi wake mike phelan,walimaliza mabox ya BIG G
 
Kuna match ujerumani na Italy World Cup 2006......kocha wa ujerumani alikuwa anaandika wapiga penalties dk ya 118 asee nilichokiona kilikuwa ni ukatili wa kibinadamu asee match ilikuwa 0-0
Nimeenda toilet narudi dah nakuta Italy 2-0Germany


Kocha akatafuta kikaratasi🤣🤣
 
Sitaisahau fainali ya Uefa second leg round of 16...Kati ya Barcelona na Psg pale Le parc Des Princes......ufaransa,

1st leg Barca akifa 4-0 Camp Nou!...2016-2017

Aisee ile Comeback ya Barca chini ya mwamvuli wa MSN pale France 6-1... Na kupita Kwa aggregate ya 6-5.....

Ni Moja ya game yangu bora kabisa ya Uefa kupata kuishuhudia.... Unbelievable!

Hadi ikapewa jina la kispaniola/french....." la remontada" means " (The Comeback)".... Aisee....

Ulipigwa mpira mwingi mnoooo!.... Pira biriani....pira ugali... Pira ukoko.....nomaaa!
 
Mlitukota siku ile, Super Mario alitoka kuunguza sehemu ya nyumba yake akaja akatuweka goli na ushangiliaji wa aina yake
Na usiku huo anaalikwa dinner na roberto mancini anaporudi kwake akapitia club akakutana na kimwana funny neguesha...
Balaa,mikosi,nuksi vilianza kumwandama super mario tangu alivyokutana na jini lile
 
Hatari sana
 
Man city 3-2 QPR: 2012, aguerooooooooo

Man city 3-2 Aston villa ;2022
6 minutes of rescue from super Gundo & Rodri.
 
Fainal kati ya Simba na Stella 1993, nilikuwa safarini kwenye Bus walikuwa wakitangaza huo mpira Sasa nipo na yangu nikasikia gooooal shangwe zikarindima uwanjani, Bus zima wako kimya Mimi na kikofia changu Cha Simba nikaruka juu nikshangilia mara nasikia "Uzalendo umetushinda" niliumia saana nilipogundua ni wanayanga wanawashangilia Stella, naapa, ninaapa kwa hicho kitendo sitowasamehe yanga na niliichukia ile timu hata nikiwa nje ya nchi wanacheza siendi kuangalia nilikwenda siku moja tu kwa kulazimishwa sikuishangilia japo walishinda
 
Nilitoka ukumbini dk 89 ili nikirudi nikute Mechi imeisha. Naingia ukumbini Aguero anafunga goli la pili baada ya pasi ya kichaa.
 
1999
Dakika 88 Bayern Munich 1-0 Man United. Full time 1-2 magoli ya Teddy Sherringham na Olle. Nililala SAA 12 asubuhi.
 
Goli la mapema baada ya Yanga kufunga hata hawajamaliza kushangilia ulipigwa mpira na chenga za maudhi likaingia goli.

Hii nayo ikae kwenye rekodi
 
Hiyo Namba 2 ndo haitafutika akilini mwangu
 
1. Goli la Kibu D dhidi ya Yanga 2023
2. Simba 5 Yanga 0
3. Yanga 3 Simba 0 kipindi cha kwanza, FT Yanga 3 Simba 3
Hii ya 3 kwa 3 ndo haitasahaulikaa kamweee.
 
Waarabu kuwaziba mdomo gongowazi kabla hawajamaliza kushangilia goli la Mayele jana hapo mjini Lupaso.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…