Tukio gani limewahi kukutokea mpaka ukajisemea kweli Mungu yupo?

Tukio gani limewahi kukutokea mpaka ukajisemea kweli Mungu yupo?

Katika dunia tunapitia mambo mengi ya huzuni na furaha, ya amani na magomvi vipi katika maisha yako jambo gani limewahi kutokea na ukajisemea kweli Mungu yupo.

Binafsi ni jinsi nilivyo faulu kidato cha sita yaani daah!

Nikikumbuka naishia kusema kweli Mungu yupo na anatenda maana nilijua nikijitahidi sana ntakuwa na division 3 ila asilimia kubwa nilijua hii ni division 4 lakini matokeo yalivyokuja daah! Sikuamini niliishia kusema kweli Mungu yupo kwani nilifaulu vizuri.

Vipi wewe kwa upande wako please share experience.

ANGALIZO: Wale wazee wa Mungu hayupo tafadhali hii sio thread ya ubishani juu ya uwepo wa Mungu so pita kimya kimya tu.
Nililala njaa nikaaamini Mungu yupo
 
Lkn pia katika mahusiano yangu nimeshuhudia Mungu kwa ukubwa wa ajabu,na bado nazidi kumtegemea yy,na hapa ndipo Imani yangu imekuwa kubwa kwa Mungu wangu,kitendo Cha kuachana na mtu uliyempenda na kumuamini kwa asilimia kubwa,na ukaamua kujitoa kwa ajili yake tu,halafu ujue amekusaliti kwa kuoa na kuzaa watoto wawili bila ya ww kujua,hakika ni maumivu yasiyokuwa na kipimo.

Lakini Mungu alisimama na mimi na akanikumbusha kuwa kuna siku nilimwambia anionyeshe kuwa huyu niliye naye ndiye au siye,basi alinijibu kwa kunifunulia kuwa niliyenaye na ninayemtegemea kama mume na baba wa familia sio wangu,ndipo akanidhihirishia kuwa kumbe alishaanzisha mahusiano mengine na mtu mwingine na kupata watoto wengine,licha ya hata kukumbuka faddila zangu kwake.Lkn Mungu alinitetea mpaka Leo naishi,ni kwa nguvu zake tu.

Na Imani yangu ni kubwa sana kwake,najua ipo siku ataniletea wa kufanana naye,hivyo nazidi kumtegemea yy tu.
 
Ni watu wasio na ufahamu wa uwepo wa Mungu ndio watabisha.
Mungu yupo, alikuwepo na ataendelea kuwepo milele na milele.
Maajabu yake yapo ni kila siku na kila wakati.
Mimi niliajiriwa shirika la serikali, mshahara mzuri, nyumba, gari na marupurupu kibao.
Kumbe kuna wakubwa wana kitaka kiti changu.
Nimekaa hapo shirikani miaka mitatu tu, nikaundiwa zengwe na nisijue linatoka wapi.
Zengwe halina kichwa au miguu, lakini serious.
Kwa cheo changu bodi ilibidi ihusishwe.
Kumbe aliyekuwa nyuma ya yote ni Mkurugenzi Mkuu aliyekuwa anaona siye vijana tuko overqualified na twaweza kuchukua kazi yake.
Nilijitetea kwa nguvu zangu zote pamoja na viambatanisho, lakini wapi.
Nilishakuwa sikio la kufa.

Kweli nilitimuliwa kwa mashtaka ya uongo na kutunga.
Nilifungua kesi mahakamani.
Muajiri akamuwahi advocate wangu na kumjaza minoti, naye akayeyuka.
Nilisononeka sana kiasi cha kutaka kulipa kisasi, lakini namkumbuka sana marehemu baba yangu , Mungu amrehemu, alinituliza sana na kusema niachilie suala na lipite na Mungu atalipa.
Kweli Mungu ni wa ajabu, kuna ndugu wa cheo cha juu ambaye hatukumfikiria mwanzoni tulimpa habari.
Yeye aliposoma matatizo yote aliona ni michezo inayofanyiwa watu serikalini.
Akamwita huyo Mkurugenzi Mkuu na kumuonya vikali.
Kumbe huyo Mkurugenzi Mkuu alisha andaa hadi mashtaka ya kunibambika.
Huyo Mkurugenzi Mkuu kumbe ana godfather sehemu moja nyeti sana, na ndio aikuwa akimungoza nana ya kueliminate potential threats kwa kazi yake.
Mimi kwa ushauri wa baba yangu nikaanza na mishe zangu za kimaisha kutafuta noti, na Mungu ni mwema zilikubali.
Haikupita muda huyo godfather wa MD akauwawa katika mazingira tatanishi.
MD akadumu muda kiasi kimang'amung'amu halafu akastaafishwa.
Tukawa tupo sote mitaani.
Aliyenifukuza na niliyefukuzwa sote tupo kitaa.
Ex MD baadaye akapata mazonge ya kutisha kifamilia na mwishowe akapata kansa.
Baada Ex MD kuugua sana, kuna mchungaji wa kanisa aliyelifahamu sakata langu alienda kumuombea, nami aliniomba nimsamehe.
Haikuwa taabu kwangu maana tayari mimi nilikuwa katika mishe mishe zangu.

Haikupita muda tena yule ex MD akafariki.
Kwa alivyonifanyia watu walishangaa nilipohudhuria mazishi yake.

Nilimshangaa sana Mungu, yule aliyenitendea mabaya kachukuliwa, niliyetendewa mabaya nimesalimika.

Kwa viwango vyovyote wacha Mungu aitwe Mungu.
Hapo unathibitisha vipi uwepo wa Mungu!?

Unajuaje kama hayo matukio yote yalikuwa yanaongozwa na kitu kingine na sio kwamba yalikuwa yanajiongoza yenyewe tu isipokuwa yamekufurahisha tu!?
 
Unataka ni kuthibitishiwa hell ipo kwa logic sio ..ok Jibu hili swali kubaka ni jambo nzuri au baya?
Nijibu alafu twende kwa logic Sasa kama unavyotaka.
Wapi nmesema nataka uthibitishe hell kwa logic?
 
Yaan Mungu muweza wa yote anashindwa kuumba jiwe zito litakalomshinda kulibeba!!

Ajabu hii
Hilo ni jibu lako wewe yaani umeamua kuuliza swali huku unajibu lako na unaamini jibu lako ni sahihi, Kumbe sio jibu tu sio sahihi yaani hata swali lako pia sio sahihi
In short umeuliza Swali silo na umejipa jibu silo.
 
Hapo unathibitisha vipi uwepo wa Mungu!?

Unajuaje kama hayo matukio yote yalikuwa yanaongozwa na kitu kingine na sio kwamba yalikuwa yanajiongoza yenyewe tu isipokuwa yamekufurahisha tu!?
Mkuu bottom line ni imani.
Usipokuwa na imani huoni, hatakama unatazama.
 
Wasioamini katika Mungu wanaona wanaotoa shuhuda za makuu ya Mungu kama mchezo. Ni mpaka upitie uzoefu wa kuona nguvu za Mungu zikitenda maishani mwako ndipo utaelewa kwa nini watu husema yupo Mungu.
 
Wasioamini katika Mungu wanaona wanaotoa shuhuda za makuu ya Mungu kama mchezo. Ni mpaka upitie uzoefu wa kuona nguvu za Mungu zikitenda maishani mwako ndipo utaelewa kwa nini watu husema yupo Mungu.
Yani kutoa ushuhuda tu napo ukiufuatilia kwa umakini unaona kabisa Mungu huyo hayupo.

Mungu muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo wote angekuwepo kweli, kusingekuwa na haja ya shuhuda

Unaelewa hilo.

Hao wanaotoa shuhuda wanazitoa baada ya kupitia mabaya,then mambo yake yakinyooka ndo anakuja na hisia hiyo ya kwamba kuna Mungu kamfanyizia.

Sasa Mungu huyo mwenye sifa zile inakuwaje tena awe na ulimwengu wenye kuruhusu mabaya!?
 
Mkuu bottom line ni imani.
Usipokuwa na imani huoni, hatakama unatazama.
Imani hiyo siyo ya kweli katika uhalisia.

Ingalikuwa ni kweli ingewezekana kuthibitika kwa Mungu huyo.

Kwanini unadhani kuamini ni muhimu sana kuliko kujua!?
 
Natamani Jf waweke option ya muanzisha thread kuweza kublock wachangiaji asiowataka katika thread yake. kuna baadhi ya mada huwa zinaanza vizuri, ila bahati mbaya ikiambukizwa virus wa ubishani hufia njiani, na hali hiyo inapunguza wingi/uwanda wa maarifa ambayo yalitegemewa kupatikana.
Mguse muhusika tu alafu kuna option ya ignore gusa pale utakuwa umemaliza kazi
 
Imani hiyo siyo ya kweli katika uhalisia.

Ingalikuwa ni kweli ingewezekana kuthibitika kwa Mungu huyo.

Kwanini unadhani kuamini ni muhimu sana kuliko kujua!?
Mkuu imani ni kila kitu.
Imani ni nguvu ya kiroho.
Hata ukiwa na uwezo wa kujua su kuona, bila imani katika uwezo wa Yesu Kristo, kuona kwako ni bure.

Baadhi ya maneno ya Yesu;

Luka 17:

1 Akawaambia wanafunzi wake, Vikwazo havina budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye vinakuja kwa sababu yake!

2 Ingemfaa zaidi mtu huyo jiwe la kusagia lifungwe shingoni mwake, akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmojawapo wa wadogo hawa.

3 Jilindeni; kama ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe.

4 Na kama akikukosea mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe.

5 Mitume wakamwambia Bwana, Tuongezee imani.

6 Bwana akasema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng'oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii.

7 Lakini, ni nani kwenu mwenye mtumwa alimaye au achungaye ng'ombe, atakayemwambia mara arudipo kutoka shambani, Njoo upesi, keti, ule chakula?

8 Je! Hatamwambia, Nitayarishie chakula, nile; jifunge unitumikie, hata niishe kula na kunywa, ndipo nawe utakapokula na kunywa?

9 Je! Atampa asante yule mtumwa, kwa sababu ameyafanya aliyoagizwa?

10 Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya.

Yesu awaponya watu kumi wenye ukoma

11 Ikawa walipokuwa njiani kwenda Yerusalemu, alikuwa akipita katikati ya Samaria na Galilaya.

12 Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye ukoma; wakasimama mbali,

13 wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu!
14 Alipowaona aliwaambia, Nendeni, mkajioneshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika.

15 Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti kuu;

16 akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria.

17 Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale tisa wako wapi?
18Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu?
19 Akamwambia, Inuka, nenda zako, imani yako imekuokoa."

Mkuu, soma Neno kwa faida ya roho yako.
 
Katika dunia tunapitia mambo mengi ya huzuni na furaha, ya amani na magomvi vipi katika maisha yako jambo gani limewahi kutokea na ukajisemea kweli Mungu yupo.

Binafsi ni jinsi nilivyo faulu kidato cha sita yaani daah!

Nikikumbuka naishia kusema kweli Mungu yupo na anatenda maana nilijua nikijitahidi sana ntakuwa na division 3 ila asilimia kubwa nilijua hii ni division 4 lakini matokeo yalivyokuja daah! Sikuamini niliishia kusema kweli Mungu yupo kwani nilifaulu vizuri.

Vipi wewe kwa upande wako please share experience.

ANGALIZO: Wale wazee wa Mungu hayupo tafadhali hii sio thread ya ubishani juu ya uwepo wa Mungu so pita kimya kimya tu.
Kuacha kutoa sadaka kanisani na kutohudhuri kanisani.

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Katika dunia tunapitia mambo mengi ya huzuni na furaha, ya amani na magomvi vipi katika maisha yako jambo gani limewahi kutokea na ukajisemea kweli Mungu yupo.

Binafsi ni jinsi nilivyo faulu kidato cha sita yaani daah!

Nikikumbuka naishia kusema kweli Mungu yupo na anatenda maana nilijua nikijitahidi sana ntakuwa na division 3 ila asilimia kubwa nilijua hii ni division 4 lakini matokeo yalivyokuja daah! Sikuamini niliishia kusema kweli Mungu yupo kwani nilifaulu vizuri.

Vipi wewe kwa upande wako please share experience.

ANGALIZO: Wale wazee wa Mungu hayupo tafadhali hii sio thread ya ubishani juu ya uwepo wa Mungu so pita kimya kimya tu.
Nilipo Pona kifo. Nilimuona Mungu
 
Mkuu imani ni kila kitu.
Imani ni nguvu ya kiroho.
Hata ukiwa na uwezo wa kujua su kuona, bila imani katika uwezo wa Yesu Kristo, kuona kwako ni bure.

Baadhi ya maneno ya Yesu;

Luka 17:

1 Akawaambia wanafunzi wake, Vikwazo havina budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye vinakuja kwa sababu yake!

2 Ingemfaa zaidi mtu huyo jiwe la kusagia lifungwe shingoni mwake, akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmojawapo wa wadogo hawa.

3 Jilindeni; kama ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe.

4 Na kama akikukosea mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe.

5 Mitume wakamwambia Bwana, Tuongezee imani.

6 Bwana akasema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng'oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii.

7 Lakini, ni nani kwenu mwenye mtumwa alimaye au achungaye ng'ombe, atakayemwambia mara arudipo kutoka shambani, Njoo upesi, keti, ule chakula?

8 Je! Hatamwambia, Nitayarishie chakula, nile; jifunge unitumikie, hata niishe kula na kunywa, ndipo nawe utakapokula na kunywa?

9 Je! Atampa asante yule mtumwa, kwa sababu ameyafanya aliyoagizwa?

10 Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya.

Yesu awaponya watu kumi wenye ukoma

11 Ikawa walipokuwa njiani kwenda Yerusalemu, alikuwa akipita katikati ya Samaria na Galilaya.

12 Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye ukoma; wakasimama mbali,

13 wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu!
14 Alipowaona aliwaambia, Nendeni, mkajioneshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika.

15 Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti kuu;

16 akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria.

17 Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale tisa wako wapi?
18Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu?
19 Akamwambia, Inuka, nenda zako, imani yako imekuokoa."

Mkuu, soma Neno kwa faida ya roho yako.
Hizo ni hadithi kama hadithi zingine.

Imani sio kila kitu.

Right kama imani ingalikuw kila kitu bhasi mngeombeana kansani mkapona bila kwenda hospitalini.

Imani za kidini ni mauongo tu hayo yametungwa na watu tu,
Ukibisha nieleze hiyo roho ni kitu gani.

Imani za kidini ni shambulio la akili.
 
Kua uyaone.
Mungu yupo, alikuwepo na ataendelea kuwepo milele!
 
Mungu mnae sema kila siku kwamba ni mwema ana upendo na huruma, Alishindwaje kuumba Dunia isiyo na majanga kama haya?

Ona sasa tetemeko la ardhi kama hili lina angamiza watu wasio na hatia wakiwemo watoto wachanga.

Je Mungu huyo hakujua kwamba tetemeko hili litatokea alidhibiti na kulizuia?

Tunaposema kwamba Mungu hayupo muwe mna elewa.

Mungu mwema mwenye upendo na huruma, HAYUPO.
FB_IMG_1694257788831.jpg
 
Back
Top Bottom