Tukio gani limewahi kukutokea mpaka ukajisemea kweli Mungu yupo?

Tukio gani limewahi kukutokea mpaka ukajisemea kweli Mungu yupo?

Yes.. according to Holly books There is hell.
That is a circular argument, your proof is based on it's own premises
_20230726_105312.JPG
_20230725_085125.JPG


hivyo vitabu uvisemavyo vitakatifu ni mkusanyiko wa hadithi za uongo za kutungwa tu na watu kama wewe,

Hadithi hata wewe ukiamua unajitungia unaziandika tu,

Uongo huo uliomo kwenye vitabu hivyo ni pamoja na mbingu na kuzimu/Hell.

Kama unabisha siyo hadithi za uongo hizo, thibitisha hell kama ipo kweli.
 
Sentensi ya " Mungu anaweza kuumba jiwe zito kiasi ashindwe kulibeba' haina logic kwa sababu ukishasema anaweza kuumba that means anao uwezo, Ukiendelea kusema kiasi ashindwe utakuwa umeondoa ule uwezo yaani ety Mungu awe na uwezo alafu uwezo wenyewe uwe wa kushindwa it doesn't make sense and no logic at all huwezi kusema mtu fulani anao uwezo wa kutokuweza
Mfano sentensi inayo sema" John Ni kipofu hivyo John anao uwezo wa kutokuona " sentensi hii sio sahii, Inatakiwa useme John Ni kipofi hivyo aoni.
Sijui umepata logic.
Hata hujanielewa na kunijibu kile nilichokuuliza mimi,

Kama umejibu ni kwamba umejibu kitu ambacho sijakuuliza mimi, na hakiendani na nlichokuuliza.

Kunauwezo wa kuumba, na kunakubeba.

Hizo ni dhana mbili tofauti.

Nakuuliza tena,

Je Mungu anaweza kuumba jiwe zito ambalo atashindwa kulibeba?

Anao uwezo wa kuumba jiwe la design hiyo?
 
Sawa ni dhana ya fizikia swali langu ni hiyo dhana haiwezi kuwa uongo?
Kwanza umeshasema dhana.
Dhana ndio inaunda dhanio na dhanio sio lazima liwe kweli
Hujaelewa hata neno dhana, wewe unaelezea dhanio
 
Hujaelewa hata neno dhana, wewe unaelezea dhanio

Hata hujanielewa na kunijibu kile nilichokuuliza mimi,

Kama umejibu ni kwamba umejibu kitu ambacho sijakuuliza mimi, na hakiendani na nlichokuuliza.

Kunauwezo wa kuumba, na kunakubeba.

Hizo ni dhana mbili tofauti.

Nakuuliza tena,

Je Mungu anaweza kuumba jiwe zito ambalo atashindwa kulibeba?

Anao uwezo wa kuumba jiwe la design hiyo?
Nimejibu swali ulilouliza, Read carefully the below reply.
Mungu ni muweza wa kila kitu.
Hiyo ndio sentensi iliyofanya ukauliza kuwa 'Je Mungu anauwezo wa kuumba jiwe zito ambalo atashindwa kulibeba?
Majibu ni kuwa..Swali lako kwanza halina logic at all, Ushasema kuwa Mungu ni muweza wa kila kitu sasa neno 'kushindwa kulibeba' ni kwamba Mungu hawezi hapa unakuwa umekataa kuwa hawezi sasa sentensi yako inakuwa imetoka kwenye mfumo wa swali inakuja kwenye mfumo wa hitimisho lako binafsi juu ya mungu.
Hivyo Mungu anaouwezo wa kuumba jiwe zito lakini hawezi shindwa kulibeba kwa sababu hakuna kinachomshinda ukisema kuwa aunde jiwe alafu ashindwe kulibeba huoni kuwa jiwe litakuwa limemshinda Mungu?
 
That is a circular argument, your proof is based on it's own premises
View attachment 2733997View attachment 2733998

hivyo vitabu uvisemavyo vitakatifu ni mkusanyiko wa hadithi za uongo za kutungwa tu na watu kama wewe,

Hadithi hata wewe ukiamua unajitungia unaziandika tu,

Uongo huo uliomo kwenye vitabu hivyo ni pamoja na mbingu na kuzimu/Hell.

Kama unabisha siyo hadithi za uongo hizo, thibitisha hell kama ipo kweli.
Hell haipo katika ulimwengu huu wa kwetu sasa unataka kuthibitishiwa kitu ambacho hakipo katika ulimwengu huu wa dunia.
Na ndio maana Mungu akaweka imani kwamba judgement zote about hell zitabebwa katika chombo cha imani, Imani ambayo inatokana na dini sasa labda uniambie wewe ni dini gani ili tupite katika mawanda hayo kuthibitisha hell.otherwise utabaki kusema kila kitu hakuna kwa sababu unataka vitu vya spiritually vithibitishwe physically.
 
Katika dunia tunapitia mambo mengi ya huzuni na furaha, ya amani na magomvi vipi katika maisha yako jambo gani limewahi kutokea na ukajisemea kweli Mungu yupo.

Binafsi ni jinsi nilivyo faulu kidato cha sita yaani daah!

Nikikumbuka naishia kusema kweli Mungu yupo na anatenda maana nilijua nikijitahidi sana ntakuwa na division 3 ila asilimia kubwa nilijua hii ni division 4 lakini matokeo yalivyokuja daah! Sikuamini niliishia kusema kweli Mungu yupo kwani nilifaulu vizuri.

Vipi wewe kwa upande wako please share experience.

ANGALIZO: Wale wazee wa Mungu hayupo tafadhali hii sio thread ya ubishani juu ya uwepo wa Mungu so pita kimya kimya tu.
Mimi matukio nimengi sana kiasi nathubutu kusema kwakuwa bado napua Mungu yupo nani Mwema sana
 
Nilikuta msg za mapenz anachat na rafiki yangu akaninyakua cm akafuta ushahidi akakataa hana mahusiano nae, Mungu alivyomkuu baada ya wiki 1, wakajirecord wanaongea mambo ya mapenz na jinsi mechi ilivyokua na hawakujua kama cm inarecord....nikaja sikiliza kilakitu
Sasa hapo shida iko wapi kama si ushetani wako wa kupekua cm za watu... Embu enjoy maisha yako acha kufuatilia mambo ya watu utakufa mapema
 
Hell haipo katika ulimwengu huu wa kwetu sasa unataka kuthibitishiwa kitu ambacho hakipo katika ulimwengu huu wa dunia.
Na ndio maana Mungu akaweka imani kwamba judgement zote about hell zitabebwa katika chombo cha imani, Imani ambayo inatokana na dini sasa labda uniambie wewe ni dini gani ili tupite katika mawanda hayo kuthibitisha hell.otherwise utabaki kusema kila kitu hakuna kwa sababu unataka vitu vya spiritually vithibitishwe physically.
Mkuu unaelewa maana ya imani?

Kwanini Mungu huyo akaweka mambo yake yawe kiimani tu siyo kwa hakika!?

Yaan unalazimisha tu Hell iaminike kuwa haipo, ilihali haipo kwenye uhalisia.

Dini ambazo zinabeba imani ndiyo uongo wa kutupwa.

Kuna Dini zaidi ya 3000+
Je dini ipi, ama hell ya dini ipi ndiyo ya kweli!??
 
Nimejibu swali ulilouliza, Read carefully the below reply.
Mungu ni muweza wa kila kitu.
Hiyo ndio sentensi iliyofanya ukauliza kuwa 'Je Mungu anauwezo wa kuumba jiwe zito ambalo atashindwa kulibeba?
Majibu ni kuwa..Swali lako kwanza halina logic at all, Ushasema kuwa Mungu ni muweza wa kila kitu sasa neno 'kushindwa kulibeba' ni kwamba Mungu hawezi hapa unakuwa umekataa kuwa hawezi sasa sentensi yako inakuwa imetoka kwenye mfumo wa swali inakuja kwenye mfumo wa hitimisho lako binafsi juu ya mungu.
Hivyo Mungu anaouwezo wa kuumba jiwe zito lakini hawezi shindwa kulibeba kwa sababu hakuna kinachomshinda ukisema kuwa aunde jiwe alafu ashindwe kulibeba huoni kuwa jiwe litakuwa limemshinda Mungu?
Maana yake ni kwamba hawezi kuumba jiwe lililozito lenye kumshinda kulibeba?
 
Mkuu unaelewa maana ya imani?

Kwanini Mungu huyo akaweka mambo yake yawe kiimani tu siyo kwa hakika!?

Yaan unalazimisha tu Hell iaminike kuwa haipo, ilihali haipo kwenye uhalisia.

Dini ambazo zinabeba imani ndiyo uongo wa kutupwa.

Kuna Dini zaidi ya 3000+
Je dini ipi, ama hell ya dini ipi ndiyo ya kweli!??
Unataka ni kuthibitishiwa hell ipo kwa logic sio ..ok Jibu hili swali kubaka ni jambo nzuri au baya?
Nijibu alafu twende kwa logic Sasa kama unavyotaka.
 
Kulishwa kitu chenye madawa then kukaa unconscious kwa masaa 48 kisha kuamka na kupona kabisa though watu wengi walijua ndo mwisho wangu... Kwangu hapa ukuu wa Mungu ulijidhihirisha.
 
Ni Mengi Mungu ametenda kwangu ila kwa hil tukio huw nawaza na kushkuru mpaka kesho. Kuna siku nilipigika yaani niliwamba na na kuchakaa sina pesa kabisa. Na wakati huo kodi ya kijiofisi changu na sehem ninayoishi zimebakiza siku moja ziishe, ukichek harakat zangu sina hata dalili ya kupata pesa nilipe kodi wenye nyumba tayari washaanza kunipigia simu, huyu wa Ofsi ambapo nilikuwa nalipa 210,000/= kwa miez mitatu anadai anaomba niwaishe kodi maana mtoto katimuliwa ada shuleni hvyo siku mbili zijazo anatakiwa kurud shule maana kule shule kuna zoez la ujazaji fomu flan zitafanyika siku hiyo maana alikuwa darasa la mitihani. Huyu ninapoishi yeye ni mfugani pia anadai vifaranga vya kuku tayari viko njiani vinakuja hvyo anategemea kodi yangu anunulie chakula cha kuku yeye nilikuwa nalipa 180,000/= kwa miez sita.

Ukweli nilikaa moyoni ile siku huk nikijisemeza Eeh Mungu kama upo kweli naomba uonekane sasa, niliendelea hvyo na ukweli sikuwa na tumain lolote la kibinadam maana nikiwaza kuipata hiyo pesa kwa pamoja bdo naona ni mtihani mkubwa sana nimeupata. Kama wasemavyo wengine kuwa matendo ya Mungu ni ya ajabu na hayaelezeki bas katika hili nilishindwa kueleza. Ikafika sik ya kulipa kodi na kuna kijimvua kilikuwa kinanyesha toka mida ya saa 11 alfajili na tayar saa tatu ila bado mvua inanyesha. Ikaingia namba mpya kwenye sim yangu ikawa inaita, naipokea alikuwa ni mdada akajitambulisha kuwa ni muasibu wa taasisi X na hii taasisi naifahamu maana nimewah fanya kazi kwao kwa mkataba na tayari mwaka ulikuwa umepita tangu niachane nao. Huyu mhasib aliniuliza kama mim ndiye anayenitafuta kwa kutaja majina yangu yote matatu, nikajibu kuwa mim ndimi haswaa, basi akanieleza kuwa anatambua kuw mkataba uliishia kipind flan lakin wao kuna makosa yalifanyika walikuwa wanaendelea kuniwekea mshahara wangu hivyo anaomba kama nina taarifa bas nimsaidie namna y kurudisha zile pesa, Nikil kuw sikuwa na faham chochote maana ile acount nilifungua kwa ajil ya kupokelea mshahara tu na sikuwa nimeunganisha kwa sim zangu kuw mshahara ukiingia bas niwe napata notifications flani hivyo baada ya kumaliza mkataba wangu na kupata mshahara wangu wa mwisho nilienda nikakomba wote na ATM CARD nikaitelekeza. Kwa maelezo ya yule dad nikamwambia kuw inawezekana ila naomba niende benk kuhakik maana sijui lolote, ilibid nitoke na mvua mpak bank na nikaomba statement, ni kweli nikakuta kuna tumilion kadhaa, nikampigia yule dada kumjuza kuwa ni kweli pesa ipo ila nina ombi kwake..

Ombi langu kwake lilikuw hvi. Huu ni ukwel mtupu wakati nafanya kazi kwenye taasisi ile kuna kipind ilitokea tatizo la kufanya malipo ya mishahara hivyo kuna watu wacheche mshahara haukuingia kabisaa kwa mwezi ule na mim nikiwa mmoja wa wahanga, nilifuatilia sana mpaka mwez ukapinduka ila sikuwa nimelipwa pesa yngu, mwez uliofuata ukaingia mshahara wa mwez husika na ikaendelea hvyo kwa miez mingine.. mpaka namaliza mkataba wangu niliendelea kufuatilia lakin sikupata majibu. Sasa ilipotokea hii nikaona ni sehem sahih ya kudai haki yangu. Nikamueleza kila siku kilivyotokea kule nyuma akaomba afuatilie atarud kwangu kunipa jibu. Ndugu msomaji pesa yangu wala sikuifikilia mara mbil nikaitoa na kwenda kulipa madeni yanyu ya kodi na nilifanya hvi kwa ujasili maana ile ilikuwa pesa yangu halali kabisaa na kuwa simzurum mtu, pesa yangu nilitoa na y kwao nikabakiza nikisubir maelekezo yke.

Toka siku amenipigia sim na kusema ngoja afuatilie zilipita siku mbil kimya, ikaj y tatu mara week ikabid nimpigie, nilimpigia sana na sim haikupokelewa nilipiga tena na tena takribani miez mitatu ila sim hazipokelewi, natuma text kuomba kupewa muongozo namna y kurejesha hzo pesa ila sikupata majibu yoyote chanya.. Hvyo baada ya takribani miez sita kupita bila majibu niliamua kuzitumia zile pesa na sasa ni miaka mitatu sijawah pokea sim yka. Hili tukio huw linakumbusha juu ya uwepo wa Mungu na naamin Mungu yupo.
Ni watu wasio na ufahamu wa uwepo wa Mungu ndio watabisha.
Mungu yupo, alikuwepo na ataendelea kuwepo milele na milele.
Maajabu yake yapo ni kila siku na kila wakati.
Mimi niliajiriwa shirika la serikali, mshahara mzuri, nyumba, gari na marupurupu kibao.
Kumbe kuna wakubwa wana kitaka kiti changu.
Nimekaa hapo shirikani miaka mitatu tu, nikaundiwa zengwe na nisijue linatoka wapi.
Zengwe halina kichwa au miguu, lakini serious.
Kwa cheo changu bodi ilibidi ihusishwe.
Kumbe aliyekuwa nyuma ya yote ni Mkurugenzi Mkuu aliyekuwa anaona siye vijana tuko overqualified na twaweza kuchukua kazi yake.
Nilijitetea kwa nguvu zangu zote pamoja na viambatanisho, lakini wapi.
Nilishakuwa sikio la kufa.

Kweli nilitimuliwa kwa mashtaka ya uongo na kutunga.
Nilifungua kesi mahakamani.
Muajiri akamuwahi advocate wangu na kumjaza minoti, naye akayeyuka.
Nilisononeka sana kiasi cha kutaka kulipa kisasi, lakini namkumbuka sana marehemu baba yangu , Mungu amrehemu, alinituliza sana na kusema niachilie suala na lipite na Mungu atalipa.
Kweli Mungu ni wa ajabu, kuna ndugu wa cheo cha juu ambaye hatukumfikiria mwanzoni tulimpa habari.
Yeye aliposoma matatizo yote aliona ni michezo inayofanyiwa watu serikalini.
Akamwita huyo Mkurugenzi Mkuu na kumuonya vikali.
Kumbe huyo Mkurugenzi Mkuu alisha andaa hadi mashtaka ya kunibambika.
Huyo Mkurugenzi Mkuu kumbe ana godfather sehemu moja nyeti sana, na ndio aikuwa akimungoza nana ya kueliminate potential threats kwa kazi yake.
Mimi kwa ushauri wa baba yangu nikaanza na mishe zangu za kimaisha kutafuta noti, na Mungu ni mwema zilikubali.
Haikupita muda huyo godfather wa MD akauwawa katika mazingira tatanishi.
MD akadumu muda kiasi kimang'amung'amu halafu akastaafishwa.
Tukawa tupo sote mitaani.
Aliyenifukuza na niliyefukuzwa sote tupo kitaa.
Ex MD baadaye akapata mazonge ya kutisha kifamilia na mwishowe akapata kansa.
Baada Ex MD kuugua sana, kuna mchungaji wa kanisa aliyelifahamu sakata langu alienda kumuombea, nami aliniomba nimsamehe.
Haikuwa taabu kwangu maana tayari mimi nilikuwa katika mishe mishe zangu.

Haikupita muda tena yule ex MD akafariki.
Kwa alivyonifanyia watu walishangaa nilipohudhuria mazishi yake.

Nilimshangaa sana Mungu, yule aliyenitendea mabaya kachukuliwa, niliyetendewa mabaya nimesalimika.

Kwa viwango vyovyote wacha Mungu aitwe Mungu.
 
Ni mengi sana Mungu amanitendea,lakini kwa haya nashuhudia uwepo wa Mungu kuwa Yu hai na anatenda.

1: Wakati namaliza darasa la Saba sikufaulu,nilikaa almost two yrs,then after nikarudia la Saba tena,ikiwa imebaki miezi miwili tufanye mtihani wa mwisho,you can't imagine,baada ya kukaa miaka miwili home nakuja kufanya mtihani ndani ya miezi miwili na nikafaulu vizuri kwenda kidati Cha kwanza,Mungu huyu acheni aitwe Mungu.

2: Nikiwa kidato Cha sita kuna wakati niliishiwa kabisa na pocket money,nikawa nimebakiwa na miambili tu.Nakumbuka ilikuwa siku ya j mosi,na kesho yake ni jumapili kanisani. Nikawa najiuliza nitatoa Nini sadaka? Basi usiku ule wa j mosi niliwaza sana juu ya kesho jumapili.

Asubuhi kumepambazuka nimeoga vizuri naelekea kanisani kwa mara ya kwanza naenda bila sadaka. Basi nilipofika mlangoni mwa kanisa nikawa nafikiri sana nikashindwa kuingia kanisani,nikarudi bwenini nikachukua ile mia mbili niliificua kwenye tranka nikaenda kanisani nikatoa sadaka,hivyo nikabaki mweupe.

Jumapili Ile iliopita vibaya nilikuwa tu nawaangalia wezangu wakipanga foleni ya kununua vitu dukani. Usiku uliingia tukala msosi wa shule tukalaa kwa ajili ya kesho yake j3. Basi kama kawaida j3 Huwa tulikuwa na pared,asubuhi then tukaenda class. Mida kama ya saa nne hivi asubuhi mwanafunzi mmoja wa combi nyingine akaja akaniambia unaitwa na madam Fulani ofisini,nikaogopa nikajisemea kwani nimefanya kosa gani,but nikaenda,kufika ananiambia dada yako alikutumia 30000,hii hapa chukua. Loh,sikuamini macho yangu na hapo ndipo nilijua Mungu yupo na anatenda

3: Wakati wa kwenda chuo kwangu ulikuwa mgumu sana,kwanza nikichelewa kwenda kwa sababu ya Hali haukuwa nzuri.Ila nilijitahidi nikaenda hivyo hivyo,pasipokujua kuwa nitaanzaje.Niliamini sana mdomo wangu,wakati wa kusajiliwa tulikuwa tunatakiwa tulipe 480000 ndo usajiliwe bila hiyo husajiliwi,tena unatakiwa uje na pay in sleep sio cash. Sasa kuna mwenzangu tulikuwa nay yy alikuwa na laki 2 ,alivyoingia kwenye chumba Cha kusajiliwa akagimbezwa sana akaambiwa cash haihitajiki inatakiwa ilipwe bank,na hawahitaji Hela nusu,wanataka yote,basi bwana mi hapo Sina hata mia mfukoni nipo empty,so yule mwanzangu alivyotoka akaniambia mi nimekataliwa,nilipata uchungu sana lkn nikajipa moyo nikaingia.

Nilianza kutoa maelezo huku machozi yakinilenga yule father akaniambia sisi tunachotaka ni pesa,we unakujaje chuo bila Hela? Nikazidi kumueleza basi akaniandikia ki memorandum,nikaenda nikasajiliwa pasipo kulipa ada,nilikuja kulipa badae kabisa,hapa ndipo ninapoamini ukuu wa Mungu.
 
Back
Top Bottom