Tukio gani ulishawahi kufanya ukajiona mshamba sana?

Tukio gani ulishawahi kufanya ukajiona mshamba sana?

Mara ya kwanza kuoa, kwenye usiku wa kwanza wa fungate mke wangu alilala na kanguo kafupi kepesi...alinikwaza sana maana nilikua namheshimu sana na hakuwahi nivalia nguo fupi kabla.
[emoji1787]we itakua ni msabato haha usiulize nimejuaje
 
Nikikumbuka kadi yangu ilivyo mezwa pale ubungo centre/sheli

Kumbe ATM ni touch sio button nakaa nione inachoendelea

Dk tatu nyingi nasikia tiii tiii tiiiii tiii ndo akili inarudi hapo sina hata nauli acha kabisa
😀 ATM kamati ya roho mbaya
 
Habari wakuu
Mara ya kwanza kujiunga na huduma za kibenki nilienda kwenye tawi la benki wakanisajili ikafika mda wa kufanya kadi iwe active.
Nimeenda kwenye ATM na yule mhudumu akaiweka kadi ndani ya ATM ananiambia chagua lugha, me hapo hata sijui wanabonyeza wapi, akanionesha zile button za pembeni nikachagua, akanambia bonyeza hapa nikabonyeza, akasema weka namba ya siri nikaanza kuijaza.

Sasa yeye akatoka nimemaliza akakawia kuja. Namsubiri mara nashangaa kadi inamezwa nikamuita nikamuuliza mbona kadi imedumbukia tena, akasema aisee ungeitoa dah, me nikamwambia sasa hukuniambia, nilikaa pale saa zima nasubiri wailete dah!

Mara ya pili, nimeenda ATM pekeangu kufika kumbe ile ATM ni ya touchscreen haina buttons za pembeni zipo za namba tu maandishi yale ya pembeni kumbe unatouch, duh nikadata nje kuna bonge la foleni wanasubiri nitoke, naweka kadi naweka PIN nasubiri hola! duh nikaona nitoke hapa nishatolewa ushamba, hata nikaona kuuliza watanicheka nikaenda kutoa kwa wakala, haha dah!
ushamba mzigo
Kuweka KONYAGI kwenye friji
 
Back
Top Bottom