Tukio gani ulishawahi kufanya ukajiona mshamba sana?

Tukio gani ulishawahi kufanya ukajiona mshamba sana?

Hakuna aliyewahi kujipulizia Dawa ya Mbu akijua Ni pafyumu Kubwa ?
Kaka yangu mtu mzima ameia kwa kuchelewa. Sada kajiopolea mtu mzima mwenzake,
Mimi na ndugu wengine baada ya kuoa tukaenda msalimia na kuvunja kamati mara moja.
Kufika pale shemeji kapika machopo chopo kibao wageni upande wa mume wamekuja.
Moja la pishi alilopika ni samaki. Wageni tumekula tumeshiba tukaletewa maji ya kunawa na sabuni(1a magadi).
Sasa kuna mtu akanawa akanusa mikono kawaida., biharusi mpya akajichukulia point 3 chap, c akachukua air fresh akupulizia watu mikononi ili kukata shombo la samaki.
Aisee tulijibana kucheka pale ila tulivyokuwa tubaondoka njia nzima ni kicheko balaa.
MWenye mke kainama kwa aibu
 
VYoo vya kisasa vile vinaflash maji ukitoka, ndugu yangu mkinga katoka mang'oto aje asafishe macho mjini,
Tukaenda kwenye hotrl kubwaile anamaliza kukojoa akasikia pyaaaaa, wacha asituke aseme lukolo mjini ukikojoa na choo kinajibu mapigo aisee....
[emoji1787][emoji1787] πŸ˜€ πŸ˜€ Dah nimecheka
 
Kaka yangu mtu mzima ameia kwa kuchelewa. Sada kajiopolea mtu mzima mwenzake,
Mimi na ndugu wengine baada ya kuoa tukaenda msalimia na kuvunja kamati mara moja.
Kufika pale shemeji kapika machopo chopo kibao wageni upande wa mume wamekuja.
Moja la pishi alilopika ni samaki. Wageni tumekula tumeshiba tukaletewa maji ya kunawa na sabuni(1a magadi).
Sasa kuna mtu akanawa akanusa mikono kawaida., biharusi mpya akajichukulia point 3 chap, c akachukua air fresh akupulizia watu mikononi ili kukata shombo la samaki.
Aisee tulijibana kucheka pale ila tulivyokuwa tubaondoka njia nzima ni kicheko balaa.
MWenye mke kainama kwa aibu
haha πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€
 
Siku moja nilienda baa fulani kubwa sana ,nikavuta kiti nikaa, ,baada ya muda kidogo,akaja mrembo akachagua meza ya peke yake ,akatoa laptop kwenye mkoba na kuanza kubofyabofya ,kipindi hicho mtu kutembea na PC anaonekana maisha fulani ya kishua.

Mimi nikajiongeza nikamuita muhudumu ,nikamwambia qkamwabie Yule dada akimaliza shughuli be zake Kwa PC naomba nimjoin. Dada wa watu hakuwa na shida akaenda Kwa Yule demu akamwambia kisha akarudisha jibu kuwa dada kasema hayupo bize ,ukitaka mjoin ti,ila wewe ndiyo ukakae pale.

Nilifurahi kinoma nikajikuta mwanaume ni Mimi tu mle ndani, nikamsalimia ,demu akajibu Kwa sauti ya chini huku macho yakiwa kwenye PC.

Wakati huo Yule demu kaagiza maji madogo,nikamwambia unakunywa kinywaji gani (pombe) akadai alcohol hatumii alishaachaga kitambo,na akasema hatumii chochote. Nikatoa burungutu la pesa tena za watu nilitumwa na mwarabu fulani nikamnunulie vifaa vya ujenzi nikiwa kama mtoto wake maana zamani nilikuwa dereva wake hivyo akaendelea kuniamini

Demu hanywi pombe,hatumii hata soda
Nikaona sasa demu si huyu kuliko Yale mapaka yanayotumalizia pesa,Bora huyu hataki chochote,nikamshawishi basi ale chakula akadai hajisikii njaa kwani ana Mawazo Sana hapo ndipo nilipojikanyaga.lakini Ile pesa ilimtamanisha akanifanyia mchezo.

Wakati natoka nje nikaangalie nilipopaki butterfly yangu,ili nijilidhishe na usalama kuna mshikaji alinifuata akionekana ni mtu wa jikoni ,mazungumzo yakawa hivi,

Vipi kiongozi" alisalimia Jamaa.

Kwema niambie Kaka" nilimjibu

Yule uliyekaa naye ,mnafahamiana naye?
aliuliza.

Hapana ,sifahamiani naye,nimemuona hapa hapa,si unajua tena mambo ya kampani (huku nikijichekesha)

Yule demu jau,ni tapeli ,ni mlevi halafu anawaibia sana wanaume.aliongeza

(Huku nikichukia)
Weee dili na jiko bro,habari zingine achana nazo.kama hunitaki nihame baa,nilitishia

Samahani bro ,nisamehe sitarudia tena .alijibu Yule jamaa huku akiondoka .

Nilirudi nikakuta dada yupo kashika Tama huku akionekana mwenye Mawazo.

Pisi Kali ,pua ya kisomali ,nywele zimchanwa saaaafi kabisa nikaona huyu mbona mzuri, halafu hanywi pombe halafu boya mmoja analeta wivu na kudai pisi hii ni tapeli.

Vipi mbona ni mwenye Mawazo shida ni mrembo,niliuliza Kwa sauti ya kiume yenye mahaba.

Weee Acha tu nawaza hivi ni lini nitapata mpenzi wa kweli ,na nipendwe kama wengine.alijibu.

Wee usinitanie binti mrembo hivi huna mpenzi,sema unachagua Sana Sisi masikini mnaona tutawapa nini ,.niliongeza

Weee Bora mwanaume masikini lakini mwenye mapenzi ya dhati. alijibu.

Naitwa Daniel ,nimependa kampani yako sana,naenjoy naomba tafadhali niagize chochote,ule walau nafsi yangu itatulia.
Niliongea Kwa hisia.

Sasa Daniiiiiii(akiongea Kwa kudeka kama vile ananijua siku nyingi )

Hapa kuna makelele sana kwanini tusitafute sehemu nzuri,tutakapokuwa comfortable na mazungumzo yetu.demu alishauri.

Sikupinga nilitafuta nilikabidhi pikipiki yangu Kwa mlinzi nikimwambia nitairudia.(unapakiaje mtoto mzuri kwenye pikipiki?)

Nikaita taxi hao tunaenda location nyingine demu akawa anaonekana mwenye Mawazo kiasi cha kudondosha machozi .nikawa na kazi ya kumbembeleza.

Hatimaye tukafika sehemu husika Ile nashuka na watu wengine wanashuka kwenye taxi nyingine huku jamaa mmoja akiwaambia wenzie aliokuwa nao kuwa Yule demu ni mke wake na sikuzote wanagombana kisa Mimi ,nikaanza shushiwa kichapo .huku wakidai nipelekwe polisi ,nikaona polisi itakuwa soo Bora tulimalize tu tunamalizaje nikatoa kiasi cha laki sita na thelathini,hii thelathini elfu nilimpa Mzee mmoja aliyenishauri ni Bora nikubali kumalizana nao kuliko mambo Yale kufika mbali. Nilijiona mshamba Sana yaani baada ya kujua Yule demu alinichoresha
Chai
 
Hahaha wakunong'onezana jau sana.

Kuna mwanetu mmoja alisinzia class, Madam wa Kiswahili akampoint ghafla asimame ataje aina ya kitenzi kilichoandikwa pale ubaoni. Kuna jamaa bila huruma akamnong'oneza "Sema Kitenzi Kinomino.." jamaa akaitaja kama ilivyo ikawa vicheko tu...

Mwingine alikua madam mmoja wa Physics huwa mkifanya test siku inayofata anaingia na ile pepa anawasimamisha wote anauliza maswali anayejibu vizuri anakaa chini. Sasa wale wenzangu na mimi maswali ya True and False yalikua yanatubeba sana maana akikosa mwenzako kasema True we unasema False chapu kwa haraka unakaa chini.

Sasa bwana ndugu yetu mmoja asijue kwamba maswali ya True or False yameisha likaulizwa swali la kudefine asee. Kuna jamaa likamnong'onza "Semaa TRUE". Tukasikia TRUEEEEEE......Ikawa full vicheko na kipindi kikaishia hapo hapo..

Toka kipindi hicho niko makini sana na watu wanaonong'oneza.
Mwaka gani huo?
 
Back
Top Bottom