Tukio kwenye mataa ya Mwenge: Tofauti ya Wazungu na Waafrika

Leo nimepishana na mzungu anaendesha Premio.
 

Ungeenda Ulaya/Marekani ukaona waswahili wanavyo behave ungeelewa! Ni issue ya kuwa mbali na Nyumbani, na huyo ni Mzungu mmoja Kati ya mamilioni....

Pengine wewe hujawahi ona Mwafrika kafanya Hivyo, Mimi nishawahi mpaka mtu back in 2013 (50,000); baada ya kumuuliza maswali Mda mrefu!

Ulichoona Leo Hakuna sababu ya kutusema , simply umetuonea na ngozi, tembea tu sehem za San Diego, au CA kwenye slam utajua wazungu ni wenu na vichaa!

Wazungu si kitu si lolote!
 
Leo nimepishana na mzungu anaendesha Premio.
Wazungu wapo wa aina nyingi mkuu, nazungumzia kwa mzungu aliyemuongelea yeye. Wapo Hadi wanaoendesha bodaboda.

Soma uelewe.
 
Hapa kuna mambo mengi mzee. Umefanya haraka kufikia hitimisho la tukio hili. Kwanza unapaswa kufahamu tunatofautiana sana kitamaduni. Hii inakwenda mbali hadi kwenye masuala ya upendo na kujitoa. Sisi hatuna utamaduni wa tips, wala hatusaidiani kwa kulipana. Ndiyo maana unaona ukifa hapo ulipo unaweza kuzikwa na hao waliokuzunguka hata kama ndugu zako hawajulikani. Unaweza kuuguzwa na watu usiowajua... n.k. Uzunguni unaweza kufa ndani kwako ,nzi tu ndiyo itawajulisha kuwa kuna mzoga.

Hoja yangu ni kuwa sisi tuna namna tofauti ya kuonyesha upendo na huruma, tofauti na wenzetu. Ninaowalaumu ni wale ambao unakaa kimya, unaoshewa kisha hutoi kitu. Mimi ninadhani kama hutaki msimamishe mara moja. Na hata yeye kijana ajue kuwa binadamu tunatofautiana. Mwingine asingependa kuoshewa kioo chake hivyo maana hata hujui ubora wa sababuni , maji n.k. Kwa ninavyowafahamu wazungu, hiyo staili ya dogo hawaendani nayo kabisa. Ni kinyume na tamaduni zao. Wao utamamaduni wao ni wa uwazi na makubaliano.Baadhi ya wazungu, hata offer hotelini hakubali kama hajaamua ama kama inatoka mazingira ya kutatanisha. Wakati hapa kwetu mtu akikupa offer hujiulizi mara mbili. So, usishangae siku dogo akachapwa makofi na haohao wazungu unaowasifia hapa.

Kw akifupi , ninakiri na ninakuelewa unachotuambia na kutuonya. Lakini, mfano huu mmoja na namna ulivyoiwasilisha kuna mapungufu kidogo.
 
sasa hiyo screen ya gari itaoshwa mara ngapi wajameni? Mataa ya- fire ipigwe maji ya foma sabuni....magomeni junc. ....ivoivo Ioshwe !!... Hiyooo!! Morocco ipigwe maji...ok! Kuleee mataa ya reagent estate ivoivo!! Bado mwenge....kawe....ivoooo!! Wanajaza mipovu povu ya misabuni tyuuuuu!!!! Ndo maana rangi za Gari zina chujuka haraka.na kuchakaa. Kisa tu umfurahishe mtu...gari lazima ioshwe bila chemikali ya sabuni. Then inapigwa polish yake maalum kwa wakt maalum.na mtu maalum!!
Siyo kusafisha gari kihorera na njaanjaa zao tuuu!!
Then mnawalipa!! ...Mweee!!...wenye uelewa na magari yao wanamwambia achaaa...but anamlipa bure hela ni bora zaidi...
.lkn pia kusafisha screen ya gari ikiwa ya moto ni kosa...kwa wajuvi km mie gari kisheria inamwagiwa maji ikishapoa engine siyo hovyo hovyo tu! Popote Njiani.. ndo maana migari yenu ina mabaka mibaka.. . Unamwagia gari ya moto kunako mataa engine iko on!! Hee....mimaji jua kaliii yanateremkia chini kunako engine! Tena mivuke mnaiona kabisaaa Sometimes ile mifereji ya screen inazibaga kwa sababu mbali mbali. Sanasana majani ya miti. Sasa jiulize hilo povu la sabuni yenye kemikali lita churuzikia wapi? Na huko chini litasababisha nini hujui....
Wafokee tu waache km umewahurumia na una pesa wape tu kiasi chako....gari yako ni ya aina gani kwani!! Nikwambie kiwango cha uharibifu unachopata bila kujua...Tunza gari yako ikutunze wewe... Hizo huruma zako ni unaingia hasara maradufu tena usiyo ijua.... Af unalalamika vyuma vimebana?... haya yangu ni hayo
..
 
Wazungu wapo wa aina nyingi mkuu, nazungumzia kwa mzungu aliyemuongelea yeye. Wapo Hadi wanaoendesha bodaboda.

Soma uelewe.
lkn kumbuka zeruzeru siyo mzungu??
Mvaa wigi siyo mzungu pia!
Unajua watu wa mikoani mnajichanganya sana...
Hata wale watoto wa Remmy ongala ni weupe Peee! Hadi tako. ...Utawajua kwa meno yao...
 
Kwanza mleta mada kwa kuangalia haraka haraka hana gari huyu.....au ndo muosha magari mwenyewe!!!
Kwa sababu si kila aliyeko na mkoko barabarani ana hela waulize matrafiki uone.......
Mawazo tupu....huko barabarani.
Trafiki hakamati gari za raia hovyo hovyo saaana atamkuta na kiberiti..kuni au viji ndizi yeye anaangalia daladala...kirkuu!! Boda boda.bajaji...Magari ya mchanga tuuu!

Sasa hao wafuta vioo waende huko...lkn ujue wenyewe hao madreva wa vyombo hivi makauzu kinoma.....atakwambia zunguka kwa konda......ukienda kwa konda mlango umefungwa anakusanya nauli unarudi kwa dreva mataa yanaruhusu.....gari hiyoooooooo.....
......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…