Tukio kwenye mataa ya Mwenge: Tofauti ya Wazungu na Waafrika

Umetukuza wazungu sana kiasi ni kama unakufuru. Si kwamba wazungu walizaliwa hivyo. Homosapien alitokea Afrika na kwenda kumaliza kizazi cha Neanderthal ulaya. Baadae akaenea dunia nzima.
Ustaarabu wa wazungu umejengwa kwa miaka mingi iliyopita na sasa ni kama utamaduni tu. Hata sisi waafrika tulishastaarabika ila kwa vile mzungu alikuwa na nguvu akaja kumanipulate aina ya maisha yetu kiasi tumebaki na ushenzi mwingi.
Usimsifie sana mzungu kwa kutoa elfu 10 kama vile hakuna mtanzania ambae amewai kutoa kiasi kama hicho au zaidi na kama vile hakuna wazungu wanaokausha tu bila kutoa hata senti baada ya kusafishiwa vioo vyao.
Wewe unaabudu wazungu.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kuna siku nikikaa mahali akatokea mtu hata simjui jina kwa jinsi alivyoonekana ALikuwa na shjka Sana na Ni mlemavu .

Nikampa kiasi Cha kutosha kwa zaidi ya alichohitaji na sio kwamba Mimi sikuwa na shida nazo ...nilijisemea tu moyoni aaah nitapata Tena bwana halafu nikapotezea .

Nikakaa wiki mbili ndani ya huo huo mwezi Nikapata semina Fulani hivi huko mkoani walinijaza mapesa kwa siku chache tu na nilienda hio semina mwenyewe tu ofisi nzima [emoji1787].

Nikajisemea moyoni hizi ndio zile pesa bila shaka .

Vitabu vitakatifu vinasema "mjaribuni MUNGU kwa Mambo yaliyo mema muone Kama hatawalipa"

Yaani unabania hata buku mzee!! Aibu naona Mimi [emoji15]
Watu wana roho mbaya sana kaka. Mtu yupo radhi anunue pombe anywe na kimada kuliko kusaidia wasiojiweza. Kuna shida gani kumpa 1,000 au hata 5,000 kayika mamilioni ukiyonayo?!

Ubarikiwe sana mkuu.
 
Sijui hata niseme vipi?!.

Kwa lugha nyepesi tu naweza kusema wenzetu WAZUNGU wameumbwa tofauti kabisa na sisi (ngozi nyeusi) WAAFRIKA. Sitaki kutumia maneno yanayoweza kufanya nikufuru, lakini ninachoweza kusema ni kwamba Mwenyezi Mungu aliwaumba wazungu kwa namna ya pekee sana. Kusema hivi wala sio utumwa kama wengine mnavyoweza kudhani, bali ni ile hali ya kukubali (appreciating) jamii ya watu fulani pasi na kujali dini zao, rangi zao, wala asili zao. Kukubali katika jambo jema na zuri ni busara zaidi kuliko kukataa tu hata kama ni jambo jema na lina manufaa.

Ninapozungumzia wazungu simaanishi ngozi nyeupe, hapana. Sizungumzii waraabu, sizungumzii wachina, wala sizungumzii wahindi. Nazungumzia WAZUNGU, watu wenye asili ya kutoka bara la Ulaya wenye rangi nyeupe (the white people).

Kuna Kijana anafanya kazi ya kufuta vioo vya magari katika makutano ya barabara ya kutoka Tegeta kuja Mwenge. Ni pale kwenye taa za barabarani (trafic light). Gari zinapo simama tu kwenye foleni kijana huyu humwaga povu la sabuni kwenye kioo cha mbele, kisha hutumia kifaa chake maalumu kufuta lile povu ili kuondoa vumbi. Kazi hii huifanya kwa uharaka sana na kwa ustadi wa hali ya juu. Ndani ya dakika moja na sekunde kadhaa atamwaga povu, atasafisha kioo, kisha atafuta povu na kuacha kioo cha gari yako kikiwa kisafi.

Kazi hii imekuwa ikifanywa na vijana wengi katika miji mbali mbali hapa barani Afrika.

Akishafanya hiyo kazi, wewe dereva unampatia kipande kidogo cha pesa. Kiasi cha pesa cha kumpa unapanga wewe mwenyewe. Wengi waliopata huduma ya kijana huyu walikausha kimya bila kulipia chochote na wala haikuwa kesi. Na wapo baadhi yao (wachache) walilipia shilingi 100 hadi 200 hivi.

Kuna gari aina ya CROWN iliyokuwa ikiendeshwa na Mzungu. Alionekana kama sio raia wa Uingereza basi atakuwa anatokea Wiles au maeneo ya jamii hiyo.

Kijana ni kama alijua vile. Na inaonyesha ana uzoefu wa kutosha wa malipo ya wateja anao wahudumia. Alisafisha kioo cha ile gari chap chap, kisha akasogea dirishani kwa dereva ili apate ujira wake. Yule dereva Mzungu akatoa noti ya shilingi 10,000 na kumpatia yule dogo. Daaah! Dogo alimshukuru sana kana kwamba yule Mzungu alikuwa amemfanyia kitu kikubwa sana kwenye maisha yake.

Taa ziliporuhusu ile gari ilipokuwa ikiondoka bado dogo aliendelea kumshukuru tena kwa kumpigia "saluti" yule Mzungu kuonyesha ame-appreciate kile alichofanya. Kama ilivyo utaratibu, yule Mzungu nae alijibu ile saluti ya dogo nae kwa kupiga Saluti.

Lilikuwa tukio la kipekee sana lililo onyesha namna sisi watu weusi (waafrika) na wenzetu wazungu tulivyo tofauti. Ni tukio lililompa yule kijana FARAJA NDANI YA MOYO. Mbali na kiasi cha pesa alicholipwa na yule Mzungu lakini kwa kijana aliona thamani ya kile anachofanya (kazi yake). Thamani ya kazi ya halali inayofanywa na mikono yake. Pengine kijana yule angekuwa mwizi au kibaka akikwapua mali za watu kwenye yale makutano ya ile barabara, leo hii thamani ya kazi yake asingeiona. Na zaidi ya yote angekuwa adui mkubwa mbele ya jamii na hasa watumiaji wa ile barabara.

Ni kawaida kwa wenzetu wazungu ku-appreciate kazi ya mtu pasi na kujali ni kazi ya aina gani. Ikiwa ni kazi ya halali na unaifanya kwa ustadi basi ataiheshimu kazi yako katika kiwango kinacho stahili. Hii ni tofauti kabisa na sisi Wafrika.

Sisi waafrika ni watu ajabu sana. Mtu unafanya kazi ngumu, nzito tena inayo "RISK" maisha yako, inapofika wakati wa kukulipa anakulipa isivyostahili. Na pengine asikulipe kabisa, au akakudhulumu kwa kukulipa kidogo tofauti na ilivyopaswa. Kama huamini, mtazame Meneja au Muhasibu hapo ofisini kwako. Amepewa mamlaka ya kuwalipa mishahara yenu. Lakini swali ni Je, anawalipa kwa wakati? Na je, ikifika wakati wa malipo anawalipa tu, au anasubiri hadi usingizie mtoto au mke/mume kuugua ndio aidhinishe malipo yako?

Kwakuwa yupo kwenye mamlaka ya kukulipa basi atakulipa atakavyo yeye.

Nadhani hapo utakuwa umenielewa vizuri kile ninacho maanisha. Akiwa Muhasibu au Bosi anaye idhinisha malipo yenu kuna wakati atasubiri hadi ifike tarehe 38 ndio awalipe malipo yenu. Hatari sana.

Naomba leo niwakumbushe kitu muhimu. Ni dhambi kubwa sana mbele ya dunia na mbele ya Mungu kudhulumu jasho la anaye pigana kwa haki. Jasho la mpiganaji daima huwa halipotei bure. Mungu wetu mlezi anasema "walipeni watumishi ujira wao kama vile inavyo stahili". Tambua kuwa athari za kuchelewesha mshahara wa mfanyakazi wako zinaumiza watu wengi sana. Kuchelewa kumlipa mfanyakazi wako kunaumiza watoto wake, mke/mume wake, wazazi wake, ndugu zake na hata jamaa zake. Anapochelewa kupata malipo yake hata Mangi dukani anakosa pesa, kwani pengine huyo ni mmoja katika wateja muhimu sana pale dukani.

Ndugu yangu, ikiwa umepewa dhamana ya kulipa ujira wa mtu anayemwaga jasho lake, basi mlipe katika wakati sahihi. Na ikiwa unadaiwa, basi lipa deni lako katika wakati mliokubalina.

Mwenyezi Mungu awabariki sana.

Na Hilal Kanal
0718022322
Dar es Salaam

View attachment 1858654
Hawa madogo nilikuwa nawapenda zamani, ila baada ya kuniibia wiper ya dirisha la boot (nyuma), nikawa nimewachukia.

Wiper zote wanazotumia, uwe na uhakika wamekuwa wameng'oa kutoka kwenye magari ya watu na hasa viwiper vya nyuma ya gari.
 
Watu wana roho mbaya sana kaka. Mtu yupo radhi anunue pombe anywe na kimada kuliko kusaidia wasiojiweza. Kuna shida gani kumpa 1,000 au hata 5,000 kayika mamilioni ukiyonayo?!

Ubarikiwe sana mkuu.
Nadhani wengi awaelewi kanuni za dunia thus ufanya hivi
 
Wakati mwingine uchumi ni tatizo unataka umpe pesa ukicheki mfukoni unabalance ya mkate tu kwa mangi unaitoaje si kila anayendesha gari anaweza kuwa na akiba mfukoni.mbaya ni kumtukana na kumdhalilisha.
 
Sumtime muache kuchemkia Watu,Habari ndeefu Sijui Mzungu wa wapi mara mzungu kafanya nini Acheni kushobokea Wazungu,Usipojithamini wewe mwenyewe ujuwe hakuna atakayekuthamini.
 
Uwezo wako wa kufikiri unafanana kabisa na uwezo wa binti yangu, yule anaesoma darasa la Pili C.
 
Mimi naahidi kulifanya hili

Nilinunua tenzi za Rohoni hapo hapo mwenge kwa mchungaji,, nikatoa 10,000 sasa jamaa alikua ananipa chenji 8'500 nikamwqmbia sadaka

Aisee aliniombea yule mchungaji mpaka taa zinawaka
 
Watu wana roho mbaya sana kaka. Mtu yupo radhi anunue pombe anywe na kimada kuliko kusaidia wasiojiweza. Kuna shida gani kumpa 1,000 au hata 5,000 kayika mamilioni ukiyonayo?!

Ubarikiwe sana mkuu.
Amina mkuu
 
Kwanza hao watu wanaofanya kazi za hivyo ni kupoteza muda. Waje huku mikoani kuna mashamba kibao waje walime. Waache uvivu, na kupenda kukaa mijini.
 
Nilitaka kuamini storry yako Ila nilipoona CROWN Nimesita kukuamini kwa kuwa Mzungu Kama Mzungu uliyemuongelea ni vigumu kuwa na hiyo Gari. Kwanza ni Saloon/Sedan, Mzungu hutumia SUV/WAGON.

Unless ungefunguka kuwa kuwa Kuna kamzunguko kapesa kameanza kuonekana mtaani ningekuelewa.

Mengine yote umefagilia wazungu kwa mtizamo wako, na hayaendani na Story yako ya Mwenge.

Nahisi hujawahi kuishi na wazungu na kuyajua maisha yao halisi kuhusiana na fedha unawaona tu barabarani. Sasa Kama hujui hakuna mtu mchumi kama Mzungu.
Acha kukariri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom