Tukio kwenye mataa ya Mwenge: Tofauti ya Wazungu na Waafrika

Tukio kwenye mataa ya Mwenge: Tofauti ya Wazungu na Waafrika

Kuna wakati pesa inaweza kutafsiri thamanibya kile unachofanya. Waafrika tunapenda sana mseleleko, mtu akufanyie kazi kubwa then umlipe kidogo. Kwa dogo ni wazi aliona Mzungu amethamini kazi yake.
Anayependa mserereko ni huyo dogo anayetufanyia kazi bila makubaliano ili alipwe.
Kama ni hivyo,vijana wote wasio na ajira waende kwenye ofisi za watu wakapige kazi bila makubaliano halafu wadai mshahara waone Kama watapewa.
 
Nilitaka kuamini storry yako Ila nilipoona CROWN Nimesita kukuamini kwa kuwa Mzungu Kama Mzungu uliyemuongelea ni vigumu kuwa na hiyo Gari. Kwanza ni Saloon/Sedan, Mzungu hutumia SUV/WAGON.

Unless ungefunguka kuwa kuwa Kuna kamzunguko kapesa kameanza kuonekana mtaani ningekuelewa.

Mengine yote umefagilia wazungu kwa mtizamo wako, na hayaendani na Story yako ya Mwenge.

Nahisi hujawahi kuishi na wazungu na kuyajua maisha yao halisi kuhusiana na fedha unawaona tu barabarani. Sasa Kama hujui hakuna mtu mchumi kama Mzungu.

Hawajui wazungu huyo
 
Kama ni maamuzi kulipa hoja yako ni nini? Huyo dogo alichofurahia ni kupewa hela na mzungu na zaidi ya yote hiyo elfu kumi ambayo hajawahi pewa kwa mara moja.
Hoja yangu ni ugumu wa kazi anayofanya dogo. Mazingira ya kazi yenyewe. Hali yake ya kimaisha, lkn bado kuna watu walimpita bila kumpa hata 100 wakati mfukoni wana zaidi milioni moja. Hiyo ndio hoja yangu.

Ni sawa sawa na kutoa sadaka, ukiwa nacho unatoa. Na hata usipotoa hakuna wa kukulaumu. Lakinj je unamzungimziaje mtu ambaye ana laki tano mfukoni then kuna omba omba amemuomba shilingi 500 tu akale chakula na bado akamnyima, huyo unamzungimziaje?!
 
Anayependa mserereko ni huyo dogo anayetufanyia kazi bila makubaliano ili alipwe.
Kama ni hivyo,vijana wote wasio na ajira waende kwenye ofisi za watu wakapige kazi bila makubaliano halafu wadai mshahara waone Kama watapewa.
Daaah. DEMI unanichosha cos hajasome nichoandika. Tambua hao vijana wala hawakulazimishi kuwalipa.

Je umewahi pita sehem njia imeharobika then kuna vijana wanaijenga huku wakikusanya mia mia kwa walitaji?! Kwao wao ukiwapa ni sawa, na hata usipowapa bado ni sawa tu. Iko hivyo hata kwa hao madogo.
 
Hoja yangu ni ugumu wa kazi anayofanya dogo. Mazingira ya kazi yenyewe. Hali yake ya kimaisha, lkn bado kuna watu walimpita bila kumpa hata 100 wakati mfukoni wana zaidi milioni moja. Hiyo ndio hoja yangu.

Ni sawa sawa na kutoa sadaka, ukiwa nacho unatoa. Na hata usipotoa hakuna wa kukulaumu. Lakinj je unamzungimziaje mtu ambaye ana laki tano mfukoni then kuna omba omba amemuomba shilingi 500 tu akale chakula na bado akamnyima, huyo unamzungimziaje?!
Sasa suala la kutoa ni jambo lingine, Wewe umezungumzia mzungu, salute na 10,000.
Wapo wengi tu wana moyo wa kutoa sio lazima wampe huyo dogo lkn Kuna mahali wanatoa. Na pia utambue kuwa dunia haipo fair hatuwezi kufanana.
 
Nilishuhudia bosi mmoja na kitambi chake akiwa anataka kutoka kwenye gari yake ili amzibue kijana muosha vioo vya gari, kijana aliacha kila kitu na kukimbia. Alimfukuza kama mbwa!
 
Mtoa mada amekufa ameoza kwa "Wazungu"! Nadhani huyu wazazi wake walikuwa wanafanya kazi (upishi) kwa wamisionari akawa anaaminishwa kuwa " wazungu" ni malaika flani.

Vijizawadi vya maziwa, pipi na mitumba vilikjula akili yake mpaka akasalimisha (surrender) mwili wake kwa "wazungu" wambariki!
 
Kumlipa mtu pesa nyingi kwa kazi ndogo inategemea na kipato chako. Huyo mdosi unaweza kukuta hiyo 10k aliyotoa ni kama 100 kwake. Lakini mwingine hata hela ya mafuta inamsumbua aje akulipe shs 10 elfu kwa kufuta kioo vumbi!

Kwanza hao watu wanaofanya kazi za hivyo ni kupoteza muda. Waje huku mikoani kuna mashamba kibao waje walime. Waache uvivu, na kupenda kukaa mijini.
Muongo inatokana na moyo wa mtu,Kuna mtu kaumbwa na roho ya ubinafsi tu,Wala usisingizie kipato
 
Sidhani kama u a uhakika na unachoongea.
wakati hawa jamaa mi nimeishi nao na nafanya nao kazi. ingia kazini na uzoefu wako mkubwa alafu aje freshe mzungu uone kama mtalipwa sawa. tatizo mnachukua vi senario vidogo na kuwapongeza hawa watu. hawa jamaa sio kabisa, wana ubaguzi kama wengine tu
 
Mtoa mada amekufa ameoza kwa "Wazungu"! Nadhani huyu wazazi wake walikuwa wanafanya kazi (upishi) kwa wamisionari akawa anaaminishwa kuwa " wazungu" ni malaika flani.

Vijizawadi vya maziwa, pipi na mitumba vilikjula akili yake mpaka akasalimisha (surrender) mwili wake kwa "wazungu" wambariki!
Uwezo wako ni mdogo sana katika kufikiri. Ni sawa na uwezo wa ubongo wa kuku tu.
 
Mzee hutaki kutoa riziki hata kwa watoto wanao hustle kupata chochote kitu? Najua sio lazima ila atleast they are trying to make ends meet bruh!

Mie ikitokea hivyo huwa nawapa coins zozote zilizopo mfukoni. Its not that i’m that rich but atleast i provide a little support kiungwana!
Wewe utaiona pepo mkuu.

Kusaidia random people at random incident inakuongezea Sana baraka kuliko kusaidia mnaofahamiana.

Nimeshawahi kuprove hii
 
Kuna siku nikikaa mahali akatokea mtu hata simjui jina kwa jinsi alivyoonekana ALikuwa na shjka Sana na Ni mlemavu .

Nikampa kiasi Cha kutosha kwa zaidi ya alichohitaji na sio kwamba Mimi sikuwa na shida nazo ...nilijisemea tu moyoni aaah nitapata Tena bwana halafu nikapotezea .

Nikakaa wiki mbili ndani ya huo huo mwezi Nikapata semina Fulani hivi huko mkoani walinijaza mapesa kwa siku chache tu na nilienda hio semina mwenyewe tu ofisi nzima [emoji1787].

Nikajisemea moyoni hizi ndio zile pesa bila shaka .

Vitabu vitakatifu vinasema "mjaribuni MUNGU kwa Mambo yaliyo mema muone Kama hatawalipa"

Yaani unabania hata buku mzee!! Aibu naona Mimi [emoji15]
 
Kutoa ni moyo hakuna cha mzungu wala muafrika. Kuna watu kiasili wamezaliwa na moyo wa kutoa hata kwa kidogo unachowafanyia.
 
Mkuu. Hata trafiki nao hufanya kazi barabarani tena all the time na luna wakati ajali huwakuta vile vile, lkn bado hilo haliwafanyi kuacha kufanya kazi yao. Vijana hawa wapo makini sana na wanatambua kuwa kuna ajali, ndio maana hufanya kazi zao wakati taa nyekundu zimewaka na gari zimesimama. Taa zinaporuhusu tu utaona wakikaa kando ya barabara.
Mkuu achana nao Kuna watu Wana za korosho kiasilia.

Huwezi washauri wakakuelewa.
 
Back
Top Bottom