Tukio la kusisimua nililolishuhudia kwa macho yangu katika msitu wa Nairoto

kubeba sio kunywa. walibeba ili wanywe wakitoka porini. nadhan alimaanisha hivyo
 
Ungeachana nae kimya kimya tu sio lazma uonekane umeandika na wewe. Story iwe ya kweli au ya uongo, kama imepangwa vizuri na inavutia watu lazma wawe tayari kuisikiliza

nimemwandikia mleta story,sasa sijui umejibu kama nani yake!!!
 
Kuna dragon nyingine ni energy drinks tu
 
mlio ndo baruti au?
 
We jamaa mbona stori zako za Moto ivi
 
Mchimbaji maisha yake anatembea na sururu ndogo tu wanaita MOKO hivyo akiambiwa ahame au Kuna machimbo mapya yanatema dhahabu wala hana cha kubeba zaid ya sururu yake na kusepa, wengi wao hawajarudi nyumban kwao kwa miaka mingi sana maisha yao yamekua ni ya kuhama hama kwenda machimbo mapya sehem anaposikia dhahabu imetema.

Mchimbaji akipata hela huwa anaitumia kwa fujo kunywa pombe, kulala na wanawake tofautitofauti wanaojiuza maeneo ambayo yako pemben na machimbo ambapo huwa wanaanzisha mji wa dharura ambapo panapatikana kila kitu, gesti za mabati,bar za mabati zenye mziki mzito kama upo town kumbe uko porini , na migahawa kwaajili ya chakula maeneo wanapo pata huduma hizo ndo hayo wao wanaita MATANDA .

Ukikuta Hawa jamaa wanakula pesa zao we waache tu wale wanazipata kwa mateso makubwa sana, mfano... Kuna maeneo ya shinyanga watu walifunikwa na udongo wakiwa ndan ya mashimo walikaa siku 42 wakiwa ndan ya ardhi lakin baadhi wengi walifariki na walipona watatu tu baada ya kuchimba kwa siku 41 ndo wakapata maiti na watu wa3 waliokua kwenye Hali mbaya Sana, wao wanasema walikua wanakula mende na baadhi ya wadudu kwa muda huo wote, lakin baadhi ya story inasemekana ilifika hatua wakaanza kula nyama za wenzao waliokufa ili wasife, nafikiri habri ya watu kufukiwa shinyanga ipo hadi YouTube..

Story za machimbo ukiambiwa unaweza kudhani ni movie au unadanganywa ila watu wanapambana sana na maisha
 
Hao ni wale waliokua hawajielewi,wachimbaji wenye akili wamefanya mengi ya maendeleo.
Kuna mitaa kama ngulelo,kwa mrefu,moshono,sakina nyumba nyingi zinamilikiwa na wachimbaji
 
We jamaa kama ni kweli yote haya na unayashuhudia, basi ni miongoni mwa watu majasiri sana hapa duniani.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Hata Mimi ninajiuliza swali hilo na amesema kwamba walipo rudi porini walikuwa wakizipekua maiti na kupata madonge ya dhahabu,Sasa hizo dhahabu hazikutosha kuwatajirisha?vinginevyo hii ni hadithi ya kutunga.
Mkuu itoshe tu kusema hela za masimboni zina laana . hao jamaa hata wakipata hela nyingi zinaishia kwenye starehe ya wanawake na ulevi
 
Mkuu huyu jamaa kaongelea dragon energy siyo hiyo ya kilevi, dragon energy zinatumika sana kwa madereva na watu wanaofanyakazi ngumu hasa za kukesha..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…