Nisahihishe jambo moja, maranyingi huwa sipendi kuandika kutokana na kazi zangu.
Mimi sio muajiliwa, mimi ni mchimbaji, kwa hiyo maisha yangu ni yakushea na washkaji.
Some time naweza nikawa naandika jambo mala anatokea mtu (rafiki) anaanza kuniongelesha, kwa hiyo inanibidi niache kuandika nimalizane nae kwanza.
Kwahiyo munisameh kwa hilo.
************************************************************************,,*************
Kwenye safari ile nakumbuka niliongozana na mdogo wangu (Mtanzania mwenzangu pia kabila letu ni moja ) Dogo Chiko.
Tulitoka Nanhupo kuelekea nairoto kwenye dhahabu.
Tulifika Nairoto kijijini kisha pakesho yake tukaelekea polini (machimbo)
Kwanza pale kijijini tulikutana na umati wa watu usipime.
Kila mtu akiwa na shauku ya kufika polini.
Kesho yake palipo pambazuka kila mtu alikua tayari kwa safari ya kuelekea polini, me na chama langu (dogo Chiko ) tuliukanyaga kwa mguu kutokana na kutokua na nauli ya piki piki.
Nauli kwa mtu mmoja kutoka pale kijijini kwenda polini ilikua 500 quinhento miticais sawa na 25000 ishirini na tano shilling.
Tuliukanyaga mwendo wa masaa 12 kwa mguu, nakumbuka tuliingia matandani kama mida ya saa moja usiku hivi.
Lakini kwa mgodini (japo ni polini) tulikuta kama tuko mtaa wa kongo.
Watu ni wengi mno, vijana wa kiume na wakike, mabibi na mababu, mpaka watoto wa miaka 7.
Kila aina ya laana ilikua inapatikana huku, Vifo (kuuana) ubakaji, kutiana vilema yani ni kama kupakaa mafuta tu.
Pombe gani unayo itaka utaikosa, Heineken,Savana, breezer na mapombe kibao ya gharama.
Malaya kutoka kila pembe ya Africa.
Wamalawi, Watanzania, na wenyewe Mocambique.
Kiufupi huu ulikua uwanjani wa madhambi.
Nakumbuka nilifanya kazi kama week mbili tu, mala ghafla ukaibuka ugonjwa wa ajabu matandani pale.
Watu walikua wakibadilika rangi na kuharisha mwisho kifo.
Yani unaweza kukaa na mshikaji mala ghafla akaanza kubadika rangi ya macho yake, akienda kujisaidia akirudi (wengine walikua hawarudi) unamuona mwili wote ume badilika rangi kawa wanjanoo, hapo amalizi saa munamkimbia.
Halii hii ilitamba siku mbili tu, siku ya tatu matanda yote nyeupe.
Watu wote tulikimbia kurudi kijijini, sasa balaaa lilikua njiani.
Watu wengi walifia njiani, tulio tusua ni wachache sana.
Nakumbuka msafara wetu (wakurudi kijijini) ulikua na watu 8, kati ya hao wawili tuliwaacha njiani, (walifia njiani).
Moja kati ya watu hao ni Rafiki yangu kipenzi (mdogo wangu) Dogo Chiko, na mshikaji alieitwa Wamisunjo (Mateas)
Nakumbuka tulikiamsha kutoka matandani pale mida ya saa4 asbuh, tulitembea umbali mrefu, mdogo wangu Chiko akatuambia tumngoje anaenda kukata gogo (kunya)
Tulimngoja, tulikaa chini mwenye sigara aliwasha, mwenye bange lake alilipua, mwenye maji alikunywa.
Muda ulipita mara Chiko akarudi, na safari kuendelea.
Lakini kila tulipo muangalia usoni, macho yote yame badilika rangi nakua yanjano.
Tukampa maji na safari ikaendelea.
Hatukufika mbali sana, Chiko akaomba tumsubiri anakwenda tena kujisaidia.
Tilipu hii tulimngoja bila dogo kurudi, ikabidi mshikaji mmoja amfuate.
Alipo fika kule alimkuta chiko kesha kufa.
Jamaa akatuita tuje kumcheki, nikiwa mingoni mwao nilimkuta dogo amesha kauka pale alipo kaa.
Kwakua tangu tuna toka matandani tulishaambiana kua ugonjwa huu ni kipindu pindu, hivyo ukifa hakuna mtu alie thubutu kukushika.
Kwahiyo Dogo Chiko tulimuacha hapo na sisi kuendelea na safari.
Nitarudi muda si mrefu.