Tukio la kusisimua nililolishuhudia kwa macho yangu katika msitu wa Nairoto

Tukio la kusisimua nililolishuhudia kwa macho yangu katika msitu wa Nairoto

Wakuu hii story nitaimalizia lkn nahisi sio leo.
Leo nitakua busy na swala la ajali ya mchimbaji mwenzetu kupigwa shoka na mrundi.

Chanzo cha ugonjwa wao, ni simu.
Jamaa yuko hospital ya Montepuez, hata hivyo kuna taratibu zinahitajika zifanyike mshikaji apelekwe hospital ya pemba.

Hali yake ni mbaya, sijui kama atatoboa.
Nikipata wasaa nitakua nawachungulia humu.
2015 nilikuwa masasi vijiji vya mpakani na msumbiji,,story kama hii nadhani nilisikia sikia kuna watu wamekufa msumbiji...pole sana mkuu
 
Naandika habari hii nikiwa na kumbukumbu ya kuwakumbuka marafiki zangu dogo Chiko, Wamisujo, pamoja na Topha.
Hii ilikua 2015, leo ni zaidi ya miaka 5 imepita tangu washkaji zangu hao watangulie kuzimu.

Utashangaa kwanini leo nimekaa nikawakumbuka machizi boti wangu hawa.

Leo Asbuhi nimekutana na mshikaji flani hivi ambaye tulipotea takriban miaka 5 iliyo pita, huyu mshikaji tulikuwa wote NAIROTO, tulipoteana kutokana na masahibu ninayo taka nikueleze hapo baadae.

Tulipo kutana leo kila mtu alikua akimshangaa mwenzie. Mimi ndie nilie kuwa wakwanza kumuita jina lake, alipo itika tulikumbatiana na kila mmoja kutaka kujua mwenzeke ilikua wapi baada ya tukio lile.

Kwa upande wangu nilijua mshikaji alisha kufa kwenye tukio lile.

****************************************************************************************
Nakumbuka ilikua 2015 kipindi Nanhupo madini (Ruby) yanatoka kinoma. Nakumbuka ndio mbuyuni ingali mbichi watu kila siku ni mwendo wa Dollar tu.

Mara mzungu akaongeza ulinzi porini (kukabiliana na wachimbaji) police wakawa wengi, kila askali ana mbwa, watu wakawa wanapigwa Risasi wengine wanang'atwa na mbawa.

Wachimbaji uoga ukatuingia, kila mtu akawa amepagawa, ukizingatia wengi wetu tumetoka Tanzania.

Mungu si John wala Kasim, akaonyesha makudula yake.....
Tukasiki kuna kijiji kinaitwa nairoto kuna dhahabu inatoka kwa wingi.

Kama kawaida ya wachimbaji (kuhama hama) safari zikaanza za kwenda Nairoto.

Nitarudi muda si mrefu.
Bado hujamaliza tu, kukata gogo?
 
Haya machimbo ya kuibuka tu wanayaita RUSH..

Yani mzigo ukisoma ndani ya masaa mawili huezi amini kama lilikua pori utakuta Gest, baa, malaya washatimba, mama ntilie, soko, maduka na kila kitu....

Na ndani ya masaa kadhaa pia unaweza kupakuta peupe likiibuka chimbo jipya linalotema.... Watu wa GEITA wanayajua haya mazingira na rush ikidumu miaka minne vijiji vya pembeni kutakua nawatoto wengi balaaaaaa na hawana baba na hawa hua hawaendi shule....
Umesahau na ukimwi mzee.
Popote palipo na machimbo ukimwi ndio nyumbani kwake.
 
Nimekuelewa mkuu.
Tatizo maisha ninayo ishi ni mchaka mchaka kinoma.
Mfano jana usiku kucha tumekesha hospital, kuna mtanzania mwenzetu (mtoto wa songea) kapigwa shoka na mrundi.

Hivi ninavyo andika, mtanzania mwenzetu ishakula kwake, akipona sijui!!!

Kitacho tokea hapa, ni mapambano ya Wabongo na warundi hapo baadae, maana Wabongo wameapa kutokukubali.

Kwahiyo Kiufupi muda wa kukaa na kuandika kwa utulivu nakua sina.

Cha muhimu tuvumiliane.
Sawa mkuu

Kwanza hatuna chaguo lingine isipokuwa kuvumilia tu

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23]

Hata Mimi ninajiuliza swali hilo na amesema kwamba walipo rudi porini walikuwa wakizipekua maiti na kupata madonge ya dhahabu,Sasa hizo dhahabu hazikutosha kuwatajirisha?vinginevyo hii ni hadithi ya kutunga.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Tumefanana mawazo
 
Nimekuelewa mkuu.
Tatizo maisha ninayo ishi ni mchaka mchaka kinoma.
Mfano jana usiku kucha tumekesha hospital, kuna mtanzania mwenzetu (mtoto wa songea) kapigwa shoka na mrundi.

Hivi ninavyo andika, mtanzania mwenzetu ishakula kwake, akipona sijui!!!

Kitacho tokea hapa, ni mapambano ya Wabongo na warundi hapo baadae, maana Wabongo wameapa kutokukubali.

Kwahiyo Kiufupi muda wa kukaa na kuandika kwa utulivu nakua sina.

Cha muhimu tuvumiliane.
Ohooo mmnaenda kuingia kwenye vita nyingine baada ya kusurvive vita vya ugonjwa (laana)?
Aisee angalia tusije kukosa mwendelezo wa story. Hivi hakuna vituo vya ulinzi na usalama hilo eneo?
 
Wakuu hii story nitaimalizia lkn nahisi sio leo.
Leo nitakua busy na swala la ajali ya mchimbaji mwenzetu kupigwa shoka na mrundi.

Chanzo cha ugonjwa wao, ni simu.
Jamaa yuko hospital ya Montepuez, hata hivyo kuna taratibu zinahitajika zifanyike mshikaji apelekwe hospital ya pemba.

Hali yake ni mbaya, sijui kama atatoboa.
Nikipata wasaa nitakua nawachungulia humu.
Poleni sana. Huyo mrundi bado yupo hapo polini?
 
Duh poleni sana,alipigwa shoka kisa nini?
Mbona huko ugenini mnaishi maisha ya hatari sana.
Hivi kwa miaka yote mliyokaa huko kutafuta maisha bado hamjafanikiwa kuipata dhahabu muuze mpate pesa na kuja bongo kuwekeza biashara zenu mtulie?
Samahani lakini sijauliza kwa ubaya
Wanagombea simu ya wizi.
Alie umizwa alienda kudai ganji kuona kwa mtuhumiwa, hivyo walikosana kuelewana nakupelekea mapigano ya kawaida tu.

Mrundi alivyo ona kazidiwa akaenda kuchukua shoka, na majeuri akaenda kuchukua panga.

Hiyo ilikua asubuhi ya jana.
Kufika jioni wakakutana kila mmoja akiwa na silaha, ila mrundi aliwahi kurusha shoka lililo mpata mshikaji mbavuni.

Nakuna wengine wanadai mshikaji kapigwa kisu nasio shoka, kwani inadaiwa shoka walisha nyang'anywa.

Kwahiyo mpaka sasa sina habari kamili, maana kwenye tukio sikuwepo, na mpaka sasa sijafanikiwa kumuona mgonjwa.

Ila jamaa mpaka sasa hali yake si nzuri.
 
Back
Top Bottom