Cvez
JF-Expert Member
- May 19, 2018
- 4,405
- 13,411
Bold anaandika kipande kirefu. Jamaa anagusisha tuBold mwingine
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bold anaandika kipande kirefu. Jamaa anagusisha tuBold mwingine
Nimekuelewa mkuu.Sema mkuu wa kimwekumweku mi naona afadhali ungeandika kwanza ukimaliza ndio ujibu comment ili tuokoe muda
Stori yako inasisimua sema changamoto ni kwamba unaileta vipande vifupi fupi
Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Duh poleni sana,alipigwa shoka kisa nini?Nimekuelewa mkuu.
Tatizo maisha ninayo ishi ni mchaka mchaka kinoma.
Mfano jana usiku kucha tumekesha hospital, kuna mtanzania mwenzetu (mtoto wa songea) kapigwa shoka na mrundi.
Hivi ninavyo andika, mtanzania mwenzetu ishakula kwake, akipona sijui!!!
Kitacho tokea hapa, ni mapambano ya Wabongo na warundi hapo baadae, maana Wabongo wameapa kutokukubali.
Kwahiyo Kiufupi muda wa kukaa na kuandika kwa utulivu nakua sina.
Cha muhimu tuvumiliane.
Hii haiswii hata kidogo, vinginevyo hiyo iwe ajali ya kweli iliyotokana na "ugonjwa" kati mwenzako na mrundi!....
Nikipata wasaa nitakua nawachungulia humu.
Wakuu hii story nitaimalizia lkn nahisi sio leo.
Leo nitakua busy na swala la ajali ya mchimbaji mwenzetu kupigwa shoka na mrundi.
Chanzo cha ugonjwa wao, ni simu.
Jamaa yuko hospital ya Montepuez, hata hivyo kuna taratibu zinahitajika zifanyike mshikaji apelekwe hospital ya pemba.
Hali yake ni mbaya, sijui kama atatoboa.
Nikipata wasaa nitakua nawachungulia humu.
ukitukanwa unaanza kuita mods.wewe ni mbabaishaji kama wengine tu.
Mods waitwe hapa waifutilie mbali story yako hii.
Machimboni Kuna kuaga na mademu wa kila aina ase alaf wanaliwa kwa bei che , ukitaka kuonja kila rangi kila shepu utaonja kwenye mabanda ya batiSafari iliendelea huku kila mmoja sasa anamuogopa mwenzie, kila mtu anaamini kile ni kipindu pindu.
Baada ya mwendo mrefu Wamisunjo akaanza kukosa nguvu ya kutembea.
Tumbo lilianza kumuuma na kila baada ya hatua kadhaa jamaa alikua akituomba tumngoje akajisaidie.
Baada ya mwendo mrefu Wamisunjo alishindwa kutembea nakutuambia ambia tumuache yeye hawezi kutembea.
Kwakua kila mtu alikua na uoga wa kuambukizwa, hakuna alie thubutu kumbeba, tulimuacha hapo na sisi kuendelea na safari.
Tulifika kijijini usiku kama saa 6 usiku.
Kijiji kulikua kumejaa huzuni tupu.
Nakumbuka kuna brother mmoja wa kinyakyusa (jina nimelisahau) nyumbani kwake kulikua na maiti kibao (kitu kama 19 hivi) zilikua zime tandazwa barazani.
Nyingi ya maiti hizo zilikua za watoto wa Mbeya.
Hawa walikua wanamiliki vingwendu (mashine za kusachia dhahabu)
Tulikaa pale kijijini kama week hivi, mwenye bahati ya kuwaona ndugu zao waliwaona wasio na bahati ndio basi tena
Kwa upande wangu nilipotezana na wengi, wengine walikufa, wengine ndio kama huyu mshikaji nilie kutana nae leo asbuh.
Yani ni miaka 5 ndio kwanza nakuta nae leo, mshikaji alikua kwenye misele hii hii yakwangu sema sehem nyingine.
Ndani ya week ile wengine walirudi walikotoka, wengine tuliendelea kubaki kwa kukosa nauli.
Mala zikaanza story za chini chini kutoka kwa wanakijiji wapale (nairoto)
****************************************************************************************
Wachimbaji wa mwanzoni kabisa baada ya kugundua dhahabu kwenye korongo lile, walienda mpaka kwa mwenye (chifu) wa kijiji kile na kumueleza azma yao ya kuchimba.
Chifu akawakubalia, ila kwa masharti ya kutovuta bange, sigara, pombe, wanawake wawapo polini.
Wachimbaji walikubali japo walijua kua masharti hayo kwa mchimbaji ni magumu na hayawezekani tu.
Jamaa wale walichimbaa na kila siku dhahabu ndio zilikua zikohowa tu.
Dhahabu zilitoka ile mbaya mpaka sisi wa mbali mlio ukatufikia.
Kama desturi ya mchimbaji, bila vileo (bombe, sigara, bange, wanawake) haendi.
Ikabidi washauriane kwenda kuomba kwa Mwenye, waruhusiwe kuishi maisha yao.
Walivyo fika kwa mwenye, Mwenye akakataa.
Akawaambia mizimu ya huko haitaki vitu hivyo, kwahiyo yeye haruhusu ila kama wanataka kutumia vitu hivyo ni hiari yao.
Wachimbaji walivyo rudi polini wakaanza kutumia vitu vyote.
Sigara, bange, gongo ndio vitu vya mwanzo kuingia.
Lakini kadili siku zilivyo kua zina songa ndio laana ikawa inaongeza polini.
Wanawake wakawa wengi, biashara ya ngono ikawa rasmi polini.
Polini kukawa mjini na kijijini kukageuka mstuni.
Ilifikia hatua mtu wa kijijini anakuja kutumia polini.
Baduka yakafunguliwa, bar zikawa zimezagaa.
Polini lakini mziki unagongwa utadhani uko lidas.
Mabanda ya video kama kawa.
Kiufupi poli liligeuka uwanja wa laana kwa muda mfupi tu.
Mpaka nafika mimi pale polini nilikuta kila kitu cha mjini kiko kule.
Nakuja kidogo.
Anacho kisimulia jamaa ni story ya kweli kabisa mm nmeshatembea baadhi ya machimbo kule Kuna vitu vya kutsha sana, kule maiti zinapitwa kama kafa kuku tu hakuna anae jali ni unyama unyama kama hujapata nafas ya kuish mazingira ya migod ya dhahabu unaweza kudhani hizi ni strori za kusadikika , tembea uone hii dunia haipo Kama unavyoiona hii dunia ina visa zaidi ya movie unazo zionanilichogundua jamaa ana i copy mahali ana paste huku kuna mahali itakua inasimuliwa so na yeye anapata kitonga hapo hapo all in all story nzuri
mkuu tukiachana na hadithi nimeupenda mwandiko wako.....na sina sababu ya msingi..turekodie voice note tuwekee tudownload tuskilize maana kuandika si umesema hupendi
Pole sana mkuu, habari za migodini sitakuja kuzisahau, kule binadamu mnakuwa na tabia kama nyoka, yaani kumua au kumzulumu mwingine ni kama ndo style ya maishaWakuu hii story nitaimalizia lkn nahisi sio leo.
Leo nitakua busy na swala la ajali ya mchimbaji mwenzetu kupigwa shoka na mrundi.
Chanzo cha ugonjwa wao, ni simu.
Jamaa yuko hospital ya Montepuez, hata hivyo kuna taratibu zinahitajika zifanyike mshikaji apelekwe hospital ya pemba.
Hali yake ni mbaya, sijui kama atatoboa.
Nikipata wasaa nitakua nawachungulia humu.
Hata Mimi ninajiuliza swali hilo na amesema kwamba walipo rudi porini walikuwa wakizipekua maiti na kupata madonge ya dhahabu,Sasa hizo dhahabu hazikutosha kuwatajirisha?vinginevyo hii ni hadithi ya kutunga.Duh poleni sana,alipigwa shoka kisa nini?
Mbona huko ugenini mnaishi maisha ya hatari sana.
Hivi kwa miaka yote mliyokaa huko kutafuta maisha bado hamjafanikiwa kuipata dhahabu muuze mpate pesa na kuja bongo kuwekeza biashara zenu mtulie?
Samahani lakini sijauliza kwa ubaya