Baada ya heka heka ya kutwa mzima ya kuzikusanya kwa mafungu zile maiti, jioni iliingia na zoezi tukali simamisha.
Tukasogea pembeni na tukio, kama kawaida yetu, moto mkubwa ukalipuwa mwenye kulala ali lala, ila wengi hatukulala.
Tulibaki pale mpaka asubuhi, tukiwangoja wenzetu walio kwenda kijijini kununua petrol.
Kutokana na kijijini kua mbali ilikua ngumu kwa mtu kwenda leo kurudi leo leo.
Kwahiyo huku tukiwasubilia walio kwenda kijijini, tukaamua kuanza ujenzi wa Camp.
Tulijenga camps mbili, kwa haraka, ukizingatia miti imelewa, maturubai tuliyo yakimbia, ilikua ni kwenda kuamisha tu kwenye ma camp ya zamani.
Mpaka mida ya saa 8 mchana kazi ya kujenga camps ilikua ime kwisha, mavyakula yalikua ni yakusaza.
Maana ulikua unaingia tu ndani ya maduka yaliyo kimbiwa na wenyewe na kujichukulia unachotaka.
Kumbuka mpaka muda huu hakuna alie vuta bange, sigara wala pombe, japo tulivikuta.
Jioni ilipo ingia wale walio kwenda kijijini walirudi, na mungu ali saidia, jamaa walipata petrol.
Jamaa walirudi na kundi lingine la watu kutoka kijijini.
Hakuna alie thubutu kuwaeleza kua jana walivyo tuwacha tulizisachi zile maiti.
Siunajua mambo ya pesa.
Ukiwaambia lazima watataka mugawane.
Tukakubaliana usiku tukisha kula tuje tuzichome zile maiti.
Usiku ulipo fika watu wakaelea kuzichoma moto zile maiti.
Nakumbuka mimi nilibaki Camp, sikwenda kuzichoma moto.
Sikwenda kwa sababu mbili, kwanza kuchoka ukizingatia kuna mida kinyaa kinanijia.
Pili, muda mwingi nilikua nakaa peke yangu nikiangalia lile donge la dhahabu, akili ikiniambia, " nasubili nini hapa na ninacho kitafuta ninacho mfukoni"
(japo nilijipigilia mbeleni)
Wazo likaja kichwani, akija jamaa (Wamalawi) nilie sachi nae yule malehemu, nimshauri twende kijijini tukagawane ile dhahabu, kwakua pale polini hakukua na skeli (mzani wa madini).
Kuna kipindi akili inaniambia nimkimbie jamaa.
Yani pakikucha nimtoroke nirudi kijijini.
Kumbuka kazi zetu kudobana (kudhulumiana) ni kitu cha kawaida, ndio maana tulivyo fanikiwa kutoka na ile dhahabu nilijitahidi nibaki nayo mimi.
Kwanza huyu mwamba mwenyewe ni mtu na nusu.
Simuwezi kimapambano, labda nishike panga.
Nitarudi muda si mrefu.
Ila naapa kuimaliza leo.