Pale nilipo kaa (kuwangoja washkaji) usingizi ulinipitia nililalaa mpaka nilipo amshwa na makelele ya washkaji.
Sijui nilitumia muda gani kwenye usingizi ule ila nilipo angalia saa ilikua ni saa 6 mchana.
Nilipo amka nilikutana na kijua kikali utadhani niko Sudan, yani mpaka nguo nilizo vaa zilishaanza kunyauka.
Chakwanza niliwauliza kuhusu yule mmalawi, nikaambiwa bado wako camp wanaendelea kungoja mvua iishe waanze kazi.
Nilipo wauliza vipi kama mvua imeisha huko walikotoka, wakaniambia mvua imenyamaza sasa hivi baada ya kuvuka lile korongo.
Yani kumbe mvua inaanzia kwenye korongo kwenda matandani, ila kulimaliza korongo mvua hakuna.
Tulitembea mpaka kijijini, hakuna alie jua kua mimi nina dhahabu mbeleni.
Tuliingia kijijini saa 2 usiku, hapo tukalala.
Ila kwakua tulisha fika kijijini, kila mtu aliendelea kimpango wake.
Pale kijijini kila mtu anaham ya kujua kulikoni huko porini.
Nakumbuka nilitulia kwenye kiosk cha jamaa flani hivi, kila mtu alikua ananiuliza kuhusiana na porini.
Usiku kucha nilikesha kwenye kile kiosk cha jamaa nikila Royal gin (hii ni pombe kali sana) mpaka kuna kucha.
Kwakua nilikua na pesa ya kutosha niliyo chukua kwenye lile duka la marehem, hivyo ilikua mwendo wa kujimiminia pombe.
Kuna dem alinitamani nika lale kwake, lakini nilikataa kwa kuhofea asiniibie dhahabu yangu.
Migodini wanawake ndio wanaongoza kutuibia wachimbaji.
Kilicho fanyika nikumpa pombe mpaka dem akakimbia.
Asubuhi, sikutaka kulemba, na pombe zangu kichwani, nikakamata piki piki mpaka Montepuez.
Montepuez, hapa ndio kuna soko la madini yote.
Nikaingia kwa msirilanka nikapima dhahabu.
Dhahabu ilikua na uzito wa gram 112, kila gram kwa kipindi kile ilikua 2000 miticais sawa na laki moja shilingi kwa wakati huo.
Nikachukua 224,000 miticais, hapo akili yote inamuaza mama Abuu (Shemeji yenu)
Nakumbuka nilinunua piki piki na mazaga mengine kama nguo.
Nikatuma kama 60,000 miticais (sawa na Milioni tatu kipindi hicho) kwa mama yangu Tanzania, maisha yakaendelea.
MWISHO.
Naahidi kuwahabarishine matukio mbali mbali yanayo / yatayo tokea hapa mgodini nilipo.
Kumbuka kwa sasa naishi Tete, Muatiz, ila kwa hizi mvua zilizo anza kunyesha, nategemea kurudi Cabo del Gado wilaya ya Montepuez, nikatafute Ruby.
Hapa nangoja hii kazi iishe, nione kama nitaokoa chochote kinisogeze kwenye Ruby.
Ahsanteni na kwaherini.