nimerudi tena sasa baada ya kushiba sasa...
pale kibena hospital kumbe nililetwa na wanakijiji tu,kwamba imezoeleka wao wakisikia kelele toka kule msituni basi huwa wanajua lazima ni watu waliopotea pangoni sasa kuonekana kwao huwa kwa style hiyo,na baada ya hapo wengi huwa wanapata kichaa kiasi cha kushindwa kabisa elezea nini waliona kule pangoni...(mimi sikupata nitasema kwanini pia)
....nikiwa bado nauguza kidonda,hapo tayari wafanyakazi wenzangu na ndugu wameshafika,ndugu zangu ni wa njombe na wanajua habari kuhusu msitu,baada ya kuambiwa niliokotwa kule chap wakajua cha kufanya,walikuja na dawa kadhaa na MTAALAMU fulani tokea kijijini kuja kunitoa mkosi na laana zinazopatikana huko(hii huduma ndio aliikosa mangi kwa maelezo ya baadaye) ndio maana aliishia kuwa kichaa...baadae niliambiwa mambo ya mule hayapaswi simuliwa kwahiyo ukifanikiwa kutoka mzima ni aidha ufanyiwe UTAALAMU au uwe kichaa usiwe na kumbukumbu kabisa...
mguu uliendelea kutibiwa na na kuharibika kadri siku zinasonga na ule upele ukawa unazidi na nabadilika kuwa wa kijani mguu wote sasa...madaktari wakashauri unatakiwa kukatwa ili kuoza kusiendelee(hii issue ya matibabu siyo concern yangu haswa)...kwa kifupi ndio wakakata mguu ila with time nilifanikiwa kupata operesheni ya kipande bandia huwezi jua kabisa kuwa sina mguu.
nilikaa pale mwezi mzima ingawa siku za mwanzo zilikua ngumu,kumbukizi ya matukio haikua inakuja full yaani unakumbuka tu habari hadi kipindi fulani halafu hukumbuki nini kilifatia aidha unaishia kusinzia au kupata mawenge...wenge linakuja sababu ile sauti na mwanga vinakua vinaflash upya kichwani,yaani siku za mwanzo ilikua nikifika ile hatua ya mwanga na sauti ya jamaa kule chini kila kitu kinapotea hadi baadae sana ndio ikawa naweza kumbuka kila kitu na kusimulia kama hivi...
sasa turudi kuhusu wale jamaa zangu...hii habari ya jamaa kwakweli sijuagi nini kiliwapata kule,wale wawili wa chini ni mangi alifanikiwa kupata miili yao wengine haikuwahi patikana pamoja na kwamba zilifanyika mila kibao lakini wanachodai ni kwamba mtu akipotelea huko shimoni huwa ni sadaka kwa hiyo wanaita mizimu na hata msihangaike kutafuta ila ukitaka tu mabaki yake ndio kuna mahala wazee huwa wanaenda fata napo ni mifupa na hawaziki kikawaida inazikwa kimila ili kutosambaza wanachoita “tego”
mangi ndani ya ile wiki alifika hospitali na hata alikua na uwezo wa kuongea baada ya kuanza changanyikiwa na nilimuelewa mwanzoni ila kadri siku zinasonga akaacha hata kuwa anatimba kunipa gwala...natoka mimi keshakua chizi
kwa upande wake anasema alichoona kule chini ilikua ni ajabu(mangi alifanikiwa kupanda sababu anasema kwa bahati nzuri kamba yake yule jamaa wa juu alipata akili ya kuifunga kwenye mti kwa juu) kwa hiyo wakati yeye kapigwa mwanga na kuachia kamba bado mangi ilimshika sababu na yeye alikua kajifunga kiunoni akafanikiwa kupanda juu kwa kujivuta kwa ile kamba,anasema yeye alifanikiwa kutoka na pia aliokotwa na wanakijiji na ndio aliyewapa habari hadi ndugu zangu ndio kufanikiwa kunifanyizia dawa...sijui kwa mangi ziligoma labda sababu ya kuwa na damu tofauti na ya wabena,lakini sababu yeye alishawahi kuzama akatoka mzima naona akapuuza.
anasema alipigwa mwanga mkali na aliona kila kitu kule chini,kwa maelezo yake ni aliona masanduku makubwa sana yanaelea lakini sasa huko chini kuna majoka balaa,nyoka ni wengi sana(nahisi ndio hii wanayoita huku uraiani mizimu ya akina MKONGWA)...sasa huwa wanasema ukifika hatua ya kuona hawa ndio lazima ufe au uwe chizi...anasema struggle yake kutoka shimoni haikua rahisi alichoona kuhusu wake jamaa ni kwamba waliyeshuka naye alikamatwa na moja kati ya hao nyoka na kushushwa huko,pia ule mshtuko ulimvuta na aliyekua kamshikia kamba akaangukia humo,sijui kilimtokea nini yule watatu ila naye ilikuja thibitika kwamba alikufa na wazee wa mila...
nitakuja tena..