mimi miweke hapa hapa habari yangu kuhusu machimbo haya na actually siyo machimbo ni harakati za kusaka mali alizoacha mjerumani wakati wanaondoka kutuachia nchi
kuna kitu tunafumbwa sana tunafichwa ukweli,wakoloni walipanga kila kilichotokea kwenye makoloni yao na hata yanayotokea sasa yalipangwa na wanajua nini kitafatia baada hata ya miaka kumi kuhusu nchi hizi masikini za afrika
kwamba walijipanga kuondoka ni KWELI,na uhuru hatukupigania,ni wao walipanga sasa watatutawala kwa namna nyingine ili waende wakajenge nchi zao huku wakiendelea kututawala kwa mbali na kuchuma mali zao...viongozi wote wanaokuwa madarakani ni vibaraka wao,hakuna hata mmoja mzalendo wa kweli na nchi yake
nina ushuhuda wa kusema haya,moja kati ya makubaliano yao ilikua ni kuacha mali zao salama na jukumu la serikali ni kuzilinda na kuwaruhusu wakija zichukua hata baada ya miaka mia,haya yapo kimkataba na kila raisi anayeingia madarakani anaambiwa hizi siri....na waliacha mali kweli za kutosha
story yangu sasa inabase kwenye hizi mali,hapa ni madini waliyoacha kwenye misitu ya nyumbanitu huko njombe,safari ya kuzifata hizo mali zilifanya nipoteze ndugu zangu watatu na mimi kunusurika chupu chupu ila kubaki na ulemavu...sitasahau hii safari ya machozi,jasho na damu.
ngoja nikaoge nakuja...