Pole sana!
Najua sio kumbukumbu nzuri, ila inakubidi uiongelee hiyo hali, ili ifike mahali uione kawaida, hata utakapomaliza kuisimulia kuna ahueni utaipata, na with time hiyo hali itakuwa normal tu wala haitakuwa ya kushtua tena
Hata dhahabu pia anza kuziona kawaida tu ili uondokane na ile hali ya ukiziona tu unaanza kukumbuka tukio zima,
Mi nna pete moja ya gold na naivaa sana ila sijawahi kuona mauza uza ya aina yoyote ile hivyo naomba uanze kuiona dhahabu kwa namna ya kawaida, pengine ingewezekana hata silver kuwa na mauza uza uliyopitia,
Nnachojaribu kusema hapa ni kuwa, tatizo sio dhahabu, tatizo sio pete, tatizo sio kito chekundu (ruby) tatizo lilikuwa kwa mmiliki wa hiyo pete, Nadhani yeye ndio alikuwa na mambo yake kuhusiana na hiyo pete,
My mom aliwahi kuibiwa hereni zake za dhahabu pale mkwajuni, tena alivuliwa mchana kweupe na hatujawahi kuziona zikirudi mpaka leo hii[emoji2][emoji2]
Sanasana ilimbidi tu yeye kununua hereni nyingine!!!
Nakusubiria uje kumalizia stori yetu ili nasi tujifunze zaidi (maji ukiyavulia nguo huna budi kuyaoga)
Wewe ni msimuliaji mzuri sana mwandiko umenyooka, tupe tu haki yetu