Acha uoga, mambo ya kawaida hayo.
Utandawazi, elimu& dini ndivyo vimetutenganisha na Asili ya kuujua UTU wetu, rudini kwenye asili yenu mtayajua mambo ambayo hamjawai kuyajua.
Haya maisha tunayoishi kimsingi yalishapita, iko hivi Mtu anaundwa na vitu3, (1) Roho, (2)Nafsi, (3)Mwili&akili za kimwili(ufahamu), na kila muundo hapo unaishi ktk ulimwengu wake.
Roho inaishi rohoni, nafsi inaishi ulimwengu wa nafsi, na mwisho ni mwili wenye ufahamu wa kimwili ktk ulimwengu wa mwili.
Ktk ulimwengu wa Roho huko hakuna nadharia ya Muda wala wakati, na kila jambo lifanyikalo huko hufanyika kwa tafsiri ya muda tuseme linafanyika kwa muda mfupi sana sawa na sekunde, ambapo muda huo ama tukio hilo ili litafsiliwe kimwili na liakisi uhalisia wa ufaham wa dunia ya mwili, tutautumia Muda(wakati) ili kufafanua tukio hilo, na muda unaweza kuwa mrefu kulingana na tukio lililofanyika rohoni.
Unatakiwa ujuwe kuwa matukio yanaanzia rohoni na kumalizilia mwilin ambako ndiko kuna mahesabu ya muda na matendo ya mwili, na ili tuyakamilishe matendo yaliyotendwa na Roho nilazima tutumie kanuni za Muda ambapo rohon hakuna muda, hakuna siku wala mwaka, huko kunahesabika ktk nyakati za "SASA" ambapo kidunia tuna nyakati "3" kama nyakati za sasa, zilizopita na zijazo, lkn rohoni kuna "Sasa" yaan tukio likifanyika rohon litajireflect mwilin kimuda.
Hivyo haya maisha tunayoishi yalishapita tupo ktk nadharia ambazo kiroho tunazitafsiri kama "PAST", roho zetu zilishayaish haya maisha na zinayareflect matukio kutoka Nyakati zao kurudi "PAST" ilipo miili,
Kiufupi Roho yako inaishi ulimwengu wa FUTURE ambao kila jambo limeshatendeka na Mwili wako unaishi Past, hivyo ni kawaida kuliona tukio na kukumbuka kama ulishalifanya, ni roho yako inapitisha kumbukumbu zake kuziingiza ktk nafsi na baadae zinakujia ktk Ufahamu wako, ndiomaana mchakato huu usababisha watu kutoelewa maana ya matukio ama kusahau.
Kuna namna nyingi za kuyaona matukio ambayo yalishafanyika na roho kwa kupitia Ndoto, maono na uhalisia unapoliface tukio.
Haya mambo wanayajua washirikina, wachawi, na watu wa sayansi wanaopambana na TIME TRAVEL, hii sio uchawi bali ni jambo la kawaida,
Tumepumbazwa na Elimu uchwara inayotufumba ufahamu wetu tusiyajue mambo muhimu kama haya kwa kutupandikiza mambo ya kijinga jinga na maarifa ya kishenzi huko mashuleni.
Kuna mengi sana ya kujifunza basi tu Ubishi wa watu kujifunza acha yabaki kuwa maarifa ya watu wachache, wengine mtaishia kubisha na kudhihaki.